Friday on Star TV: Tathmini ya Viongozi wa Bunge 2011

kaka Yahya kama kuna janga la kitaifa kwenye nchi hii ni Job Ndugai. Tangu alivyofanya mdahalo na Lissu na kushindwa saaaaana, amekuwa ana maamuzi ya ooovyo. Yeye ni refa mwenye kadi nyekundu ambayo ni kwa ajili ya upinzani tu

Kwani Dr. faustine Ndugulile aliyetolewa jana naye ni upinzani?
 
Kimsingi Bunge la sasa limekuwa ni kijiwe kama cha Yanga na Simba na vongozi wake wanaliongoza kwa hofu ya kutokiudhi chama chao. Iweje kosa mmoja lipate hukumu tofauti kutoka kwa kiongozi huyohuyo? Mh Manyanya alitoa tuhuma inayofanana na ile ya Mh Mnyika lakini mmoja akaambiwa alete ushahidi (Chadema) lakini wa wa CCM akaachwa tena bila aibu mbele ya umma.
 
siafiki hata kidogo Ndugai kuwa namba 1, hapo dodoma kwa nini nyie star tv kuna siku kama nne au tano hakuna wabunge wa chadema, ndugai anaupendeleo wa dhahiri kama hao wengine,la msingi mtu akichaguliwa kuwa speaker ajiuzulu ubunge na nafasi kwenye chama chake.
 
Salaam WanaJF
Taasisiya kiraia ya CPW (Citizen's Parliament Watch) Kesho itatoa matokeo ya Utafiti wake mwenendowa Viongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzaniakatika kusimamia jukumu hiloAdhimu kwa Kipindi cha Mwaka 2011. Vi

gezo kadhaa vimetumika katika kupima ufanisi wao katika kuongozashughuli za Bunge. Matokeo haya yataanikwa kesho saa 1 na dk 30 asubuhi kupitiakipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star TV.

Utafiti huu unawahusisha (Mh.Mama Makinda, Mh.Jenista Mhagama, Mh.Mabumba, Mh.G.Simbachawene na Mh. Job Ndugai)
Karibunikwa Mjadala
CPW nifadhiliwa na nani? maana taasisi nyingi tunashuhudia kwa sasa hivi ni zile ambazo ziko sponsored kwa malengo mahsusi na watu wenye mtazamo fulani fulani. ni vizuri kabla ya kutoa tathimini wakaja na background yao na walikotoa pesa ktk maana ya wanyemtumikia.

kwa tathimini yangu Bunge la sasa wananchi tulitegemea utetezi mkubwa ktk kusimamia raslimali zetu na haswa kwa kuwa limeundwa zaidi na vijana wengi na wasomi wazuri lakini hovyo, wamejaa jazba na maneno ya mitaani na magazetini, ukiachilia mbali wabunge wachache kama mh zitto, anaeoneka kusoma na kufanya utafiti wa kutosha ktk hoja zake. lakini hawa wengine ni matatizo tu na wanajitahidi kujustfy allowances tu na kuwawini wananchi chukulia mfano mbunge wa kigamboni jana, ni kielelezo kidogo cha wabunge wetu wanavyoishi na watu huko watokako (wakikuona umesimama na kiongozi mkubwa wanajenga imani ya kuzungunkwa
 
StarTV, safari ijayo mlete watu wenye akili timamu zenye uwezo wa kuchambua na kuelewa mambo vizuri na kwa haraka. haingii akili Marcu alishasema vigezo vilivyotumika ktk utafiti lakini hao waliopo dodoma wanadai eti hawajui. Kwani walifika hapo studio ya Dodoma straight from their hotels au walikuwepo tangu Marcu alipoanza?

Mngejaribu kuleta watu wa vyama 'halisi' vya upinzani sio hivi viwili ambavyo vimefunga ndoa na CCM. Matokeo yake ndo hayo, hao wabunge wamegeuza studio ya Dodoma kuwa ni sehemu nyingine ya kuvishambulia vyama 'halisi' vya upinzani. Mjadala unaoendelea sasa studi ya Dodoma unaelekea kwenda nje ya mada na muongozaji nao anaonekana amesombwa na hao waongeaji wa Dodoma.

Please Mhata, rekebisha hilo mapema!
 
Mheshimiwa Kessy yuko nje ya mada anaendeleza malumbano kama yuko mjengoni...Tafiti inapingwa kwa tafiti sio kupiga domo tuu.lengo la tafiti ni kuboresha utendaji kazi wa viongozi wa bunge.
 
Narudia tena, wageni wenu studio dodoma ni mabom!!!!
Mngewaalika chenge kwa upande mmoja na mch. Msigwa, hapo tungepata picha nzuri.
 
Mhata rekebisha, mjadala uliopo mezani hauhusiani na suala la muda! Huyo mtu wenu hapo Dodoma vp? Mwambieni aturudishe kwenye hoja! My day has turned out boring! Niliacha kwenda kuwahi kazini nikitegemea michango ya maana sio hii ya kutoka dodoma. Kule dodoma mlipaswa kuleta wabunge wenye upeo wa mambo sio hao 'vituko' Mhata, agrrrrrrrrrrr!
 
Kwa sasa sifatilii bunge wala mijadala kuhusu bunge,,,,,,wooooote vihiyo,wanageuza bunge kuwa kama show ya komedi,tafuten na wadhamini ili tujue kuwa KIPINDI HIKI CHA BUNGE KIMELETWA KWENU KWA HISANI KUBWA YA............
 
Kwa sasa sifatilii bunge wala mijadala kuhusu bunge,,,,,,wooooote vihiyo,wanageuza bunge kuwa kama show ya komedi,tafuten na wadhamini ili tujue kuwa KIPINDI HIKI CHA BUNGE KIMELETWA KWENU KWA HISANI KUBWA YA............
 
kipindi chetu ni siasa mods what happened. mmenipa pia wakati mgumu kuitafuta hii thread. disappointing
agree with you Yahya, wakati jukwaa la Siasa kumejaa upu pu tupu, thread kama kamati kuu CDM siri za vuja, binafsi nimesikitika sana kwa kukubania... kwani wakati wote katika vipindi vyako huweza kuimarisha JF miungono mwa wanajamii. very very disappointing
 
Tathimin kama hizi ziwe zinafanyika mara kwa mara kwani zinajenga na kuwarekebisha viongozi wetu,
 
Ni nani anafadhiri tafiti hizo? Ili kujua objectivity ya matokeo yake, tafadhali tupate jibu hilo

Taarifa tulizopata ni kuwa utafiti huu ni huru na haukutumia gharama zozote za ufadhili. Watafiti walijitolea kwa gharama zao na walitumia VOLUNTEERS wa kitanzania kuendesha zoezi hili. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom