Friday on Star TV: Tathmini ya Viongozi wa Bunge 2011

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Salaam WanaJF
Taasisiya kiraia ya CPW (Citizen's Parliament Watch) Kesho itatoa matokeo ya Utafiti wake mwenendowa Viongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzaniakatika kusimamia jukumu hiloAdhimu kwa Kipindi cha Mwaka 2011. Vi

gezo kadhaa vimetumika katika kupima ufanisi wao katika kuongozashughuli za Bunge. Matokeo haya yataanikwa kesho saa 1 na dk 30 asubuhi kupitiakipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star TV.

Utafiti huu unawahusisha (Mh.Mama Makinda, Mh.Jenista Mhagama, Mh.Mabumba, Mh.G.Simbachawene na Mh. Job Ndugai)
Karibunikwa Mjadala
 
Ahsante yahya..kusema ukwel bunge la sa hizi limekosa uelekeo kutokana na uongozi mbovu ambao uko biased..viongozi wa bunge sasa hivi hawaangalii maslahi ya nchi bali wanaangalia maslahi ya CCM...mfano mwenyekiti.wa bunge kama Mabumba haelewi chochote kuhusu kanuni na sheria za bunge....wapo kwa ajili ya kuwagandamiza wapinzani..malumbano yasiyo na tija bungeni yanasababishwa na uongozi dhaifu wa bunge uliotokana na chama dhaifu na kilichochaguliwa na wananchi dhaifu.
 
Ahsante yahya..kusema ukwel bunge la sa hizi limekosa uelekeo kutokana na uongozi mbovu ambao uko biased..viongozi wa bunge sasa hivi hawaangalii maslahi ya nchi bali wanaangalia maslahi ya CCM...mfano mwenyekiti.wa bunge kama Mabumba haelewi chochote kuhusu kanuni na sheria za bunge....wapo kwa ajili ya kuwagandamiza wapinzani..malumbano yasiyo na tija bungeni yanasababishwa na uongozi dhaifu wa bunge uliotokana na chama dhaifu na kilichochaguliwa na wananchi dhaifu.

Asante kwa kutuandalia kipindi hicho. Tatizo la bunge letu ni partisanship ya viongozi wake. Hatukatai kwamba wana vyama vyao, lakini mapenzi kwa chama chao yamekuwa makubwa kupita kiasi. Matokeo yake ni kwamba demokrasia ndani ya bunge hamna, watu wanatumia Bunge kama jukwaa la kurushiana makombora nk. Kiongozi mwingine amabye ni kikwazo ni LUKUVI, ile kofia yake ya kuwa waziri wa mambo ya Bunge haina mpaka? Mara nyingi sana hoja zake zimekuwa zinakwamisha demokrasia ndani ya bunge. Yeye mwenyewe ajitathmini.
 
kaka Yahya kama kuna janga la kitaifa kwenye nchi hii ni Job Ndugai. Tangu alivyofanya mdahalo na Lissu na kushindwa saaaaana, amekuwa ana maamuzi ya ooovyo. Yeye ni refa mwenye kadi nyekundu ambayo ni kwa ajili ya upinzani tu
 
Nilidhani kutakuwa na maswali toka mitandao ya kijamii,

Ningeuliza hivi:
wananchi tunafaidika nini na spika wa bunge kuegemea upande wa serikali kwa kuwabana wabunge wasiielekeze serikali.

Mfano, iliposhindwa kupata ufumbuzi wa mgogoro na madaktari ilipaswa kuelekezwa ni nini wenyenchi wangetaka kuwatendea madaktari!!! Kwani fedha zingine wanapataje hata wakose za madaktari tu. WABUNGE WANGEJADILI KWA SABABU SERIKALI, MAHAKAMA NA BUNGE NI VYA WANANCHI.
 
Bunge la sasa ni zaidi ya Comedy, Mabuba hafai hata kuongoza kikao cha kijiji uwezo wake ni mdogo sana katika kuongoza bunge la vyama vingi. Viongozi waliobaki ni wazuri tatizo lao kubwa ni kuwa biased, wameamua kwa makusudi kupendelea chama tawala na serikali na kwa hiyo wamesababisha bunge kufanya kazi kama wagonga mhuli tu wa matwaka ya serikali and no one stands for common mwananchi. Ukituhoji wananchi wa kawaida juu ya mwenendo wa bunge tutakwambia kwamba afadhali tusingekuwa na bunge kabisa kuliko kuwa na aina ya bunge tulilonalo kwa sasa.
 
Tunakushukuru sana Yahya, pia tunakushukuru kwa kuona Jf ndo mahali pekee ambapo unatushirikisha katika mijadala yako yote unayoendesha. Big up tunakushukuru kwa kututhamini. Nitaamka mapema kusikiliza kabla ya kwenda kazini. Good night
 
Kwa kweli siku ambayo mwenyekiti anakuwa Mabumba hali ya hewa huwa inachafuka sana bungeni kutokana na kuonyesha upendeleo wa wazi kwa chama cha magamba.
 
wasiwasi wangu ni uwezekano kesho umeme ukakatwa makusudi ili watu tusione kitakachojadiliwa star tv. Si unaona mkakati walioanza nao leo bungeni, yaani kesho TANESCO wameshapata sababu ya kukata umeme kiulaini kabisa!
 
Kiukweli kwa jinsi hawa viongozi wa bunge wanavyoongoza bunge ni bora tusingekuwa na bunge manake hakuna uhura kwa wabunge kuongea mambo yanayowakabili wananchi .
 
KIUKWELI KWA JINSI HAWA VIONGOZI WA BUNGE WANAVYOONGOZA BUNGE NI BORA TUSINGEKUWA NA BUNGE MANAKE HAKUNA UHURu KWA WABUNGE KUONGEA MAMBO YANAYOWAKABILI WANANCHI .
 
Mjadala Utaanza soon karibuni sana kwa mjadala wakuu. Mawazo yaliyokwishachangiwa hapa yatasomwa soon ktk kipindi
 
Ni nani anafadhiri tafiti hizo? Ili kujua objectivity ya matokeo yake, tafadhali tupate jibu hilo
 

ushauri wangu kuhusu viongozi wa bunge

imefika wakati spika wa bunge akachaguliwa na wananchi moja kwa moja kwenye uchaguzi mkuu na si kuchaguliwa na wabunge hii inatokana na wabunge wakimchagua spika basi spika muda wote anakuwa anaogopa wabunge hasa wale kwenye chama chenye wabunge wengi. katiba mpya iweke wazi uchaguzi wa spika kuwa huru na utokane na kundi kubwa la wananchi na si kikundi cha watu wachache. pia kuna dhana imejengeka ya kuwa spika lazima awe mbunge hivyo tukibadilisha uchaguzi wa spika basi tunaweza kupata spika ambaye yuko huru
 
Kwenye katiba mpya ni mapendekezo kuwa speaker akishachaguliwa ajiuzulu ubunge na nafasi katika chama chake, sasa hatuna cha kulaumu mbuzi na chui wanafanya mdahalo na watoto wa chui ndio wanaongoza mdahalo haki haitapatikana. nilishangazwa na speaker Makinda kuzuia suala la Dr. ulimboka lisizungumzwe kwa sababu lipo mahakamani, suala la Ulimboka halipo mahakamani ni muongo, majibu aliyoyatoa Lema yapo wapi?
 
Uongozi uko biased sana mbona wabunge wa upinzani walioambiwa kuthibitisha kauli hatujapewa feedback akiwemo Lema,Zitto,Sakaya etc?
 
Ndiyo Yahaya! Viongozi wa bunge wame oneshwa kupwaya coz hoja zenye tija kwa watanzania zimekuwa zikipingwa kwa makusudi na kupotoshwa kwa makusudi kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Viongozi hawa wamekuwa marefarii wachezaji, bado wanaleta tabia zilezile za chama kimoja za kulifanya bunge kama rubber stamp. Kwa uongozi huu ,matumaini ya wananchi kuifikia Tanzania waitakayo yanazidi kufifia. WITO WANGU, VYAMA VITAPITA, BUT TANZANIA ITABAKI. TUMECHOKA NA LUGHA ZA KUDHALILISHA WAWAKILISHI WA WANANCHI KWA KUWAITA VITUKO,WANAWASHWAWASHWA,WANATAKA CHEAP POPULARITY. 2015 TUTAHESHIMIANA TU.
 
Back
Top Bottom