Freemasons: Sir Andy Chande Live On Clouds TV!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Wanabodi,

Kwa mnaotaka kuifahamu Freemasons, angalia Clouds TV now, Mkuu wa Freemasons Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Sir Andy Chande anahojiwa na Gerald Hando na kuweka what is purported to be "kila kitu hadharani!".

Kipindi kimekwisha!.

My Take: Andy Chande ame mention about Freemasons lakini hakusema lolote kuhusu inside freemasons!.

Mtangazaji Gerald Hando, very unfortunately didn't do his homework well!.

1. Alipoambiwa ili mtu kuwa freemasons lazima ufanyiwe "initiation" alipaswa kuuliza hii "initiation",inafanika vipi?, na ni kwa nini kila
member lazima afanyiwe?!.

2. Alipoelezwa huwa fremasons wanafanya "ceremonies" hakukuliza hizo ni ceremonies za kusherehekea nini na zinafanyikaje?!.

3. Alipoelezwa Freemasons sio dini, ila ili kuwa member wa freemasons lazima kwanza uwe na dini, kwa nini wasio na dini hawaruhusiwi?!, kama sio dini, what does dini ya mtu got to do freemasons.

4. Ameeleza hawana siri zozote (no secret) ila tuu ishara za jinsi ya kujuana, alipaswa aseme kama sio secret society hizo ishara za siri ni za nini, what for and why secret?!.

5. Alipoelezwa kuwa hicho ni chama cha kutoa misaada alipaswa aulize misaada gani wametoa au wameshasaidia nini?.

6. Alipoambiwa kuwa MV Bukoba ilipozama, freemasons wa Uingereza walitoa Pauni 10,000, alipaswa kuuliza why only that wakati taifa limepata majanga kibao?.

7. Alipoambiwa freemasons wala level fulani fulani na grand lodge za kila level, kama hujafikia level fulani huwezi kuingia lodge fulani, alipaswa aulize hizo levels ni za nini?, kuna vigezo gani kufikia level fulani? na kwa nini watu wa level fulani hawaruhusiwi kuingia lodge za level fulani?, nini kinafichwa humo? na ikitokea asiyehusika kuingia lodge isiyomhusu, nini huwa kinamkuta?!.

8. Alipaswa kuuliza what time of a day do they meet and why?. Kwanini hukutana usiku wa manane?, mikutano yao huwaje? wakikutana wanafanya nini?!.

9. Angeuliza kwenye hizo karamu zao za usiku wa manane, wanakula vyakula gani na wanakunywa vinywaji gani?.

10. Alipaswa kumuuliza kwa nini wanawake hawaruhusiwi? na zaidi ya yeye, ma freemasons wengine prominent Tanzania ni akina nani?.

Kusema ukweli, Andy Chande has taken Gerald Hando for a ride kwa leading questions za maswali mboga mboga ili kuipromote freemasons, nimejikumbuka enzi zangu nilipokuwa nikifanya interview programs, ilikuwa ni grilling time and leave no stone unturned!.

All and all tuishukuru Clouds FM, something is better than nothing!.

Thanks

Pasco.
 
Alipoulizwa Freemasons ni nini, amejibu Freemasons sio dini, sio imani, haina "dogma" wala haina kafara yoyote!.
 
Kuna kamati inayokuhoji kabla ya kujiunga na process ni very slow na inaweza kuchukua zaidi ya miezi 8.........na ili kuingia kwenye stage ya degree ya kwanza inachukua kama miaka 2........na utahojiwa sana.......Head of free mason is in UK.......NA WALIWAHI KUCHANGIA WAHANGA WA MV BUKOBA
 
Freemasons ni taasisi ya kijamii kusaidia shughuli mbali za misaada mfano MV Kagera ilipozama, yeye alimpigia simu mkuu wa Freemasons wa Uingereza, Malkia Elizabeti wa Uingereza hivyo walileta msaada wa Pauni 10,000 za Uingereza (just imagine kile kivuno)!.
 
Kwa tz Kuna lodges Arusha, Tanga, mwanza, Dar na vikao vinaanza mara moja kwa mwezi saa 12 na kwenye vikao hakuna discussion za siasa au dini.............
 
Back
Top Bottom