Freeman Mbowe - set Tanzanians free!

mbowe kweli ni jembe. huwa anaimia sana kila anapoifikiria tanzania. ni mtu wa pekee kwanza anahuruma sana. mimi ni kijana wake na ninafanya nae kazi kweli huyu kwa nza ni mbunifu na hana wivu.ukitaka kuamini hilo angalia tu chadema na kila kilichopo uliza kwa mtu yoyote muasisi wa hili ni nani? mbowe mungu akupe nguvu akulinde akujaze ujasiri. nipo nyuma yako saa na wakati wowote

ni kweli, pia ametumia rasilimali nyingi sana za familia yake kujenga chama..
 
Mimi ni mtanzania, ninachoangalia na muhimu sana kwangu ni Tanzania kwanza ni si kingine. Nafurahia utendaji kazi wa CDM tangu ilipoanzishwa, kweli wanahitaji pongezi kubwa. Ushauri wangu kwa wana CDM sasa hivi ni kuendelea kudumisha chama kama taasisi. Wasiingie kwenye mtego wa kuona kwamba mtu fulani katika chama ni bora zaidi japokuwa kumsifia mtu sio dhambi.

Nakubali kuwa Mbowe ni mwanasiasa wa kizazi hiki. Ni aina ya wanasiasa wanaohitajika katika zama hizi za kutafuta na kupigania haki za wananchi wanaokandamizwa kwenye nchi yao. Jukumu hili naona CDM wanalitekeleza vizuri sana chini ya uongozi wa Mh Mbowe. Binafsi naona CDM ina watu makini sana. Ukianzia kwa wabunge hadi wanachama wa kawaida. Angalia vichwa kama Prof Mwesiga Baregu na watu wengine makini, wote hawa wanakifanya kuwa chama makini kweli kweli.

Wana CDM safari bado ni ndefu sana, kila mtu ajitahidi kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha kuwa lengo linatimia. Naunga mkono juhudi zozote zinazoelekea kumkomboa mtanzania......
 
days are counted down for the truth to be revealed. what has hapened is a start.
Hi all,

kila wakati nimekuwa nikitafakari dynamics za politics hapa Tanzania na nimegundua kuwa Mungu nio mwema..

nikatafakari modalities za umafia wa siasa zinazotumiwa na CCM kuendelea kushika dola nikaona upendo wa Mungu....

ni Mungu ndiye aliyemtuma mja wake Freeman aje atukomboe.....

Freeman ni mwanadamu, naye ana mapungufu pia ana mazuri.....

Freeman, will set Tanzanians FREE!!!

nina kila sababu ya kusema hivyo na nitaweka mkazo kama ifuatavyo...

Tangu kuanzishwa kwa vyama vingi umafia ufuatao umekuwa ukitumika....

1. kuanzisha vyama utitiri vya kusindikiza CCM ikulu. vyama hivi vimekuwa vikiongozwa ma mamluki au maafisa usalama. vimeshiriki chaguzi lakini kiutaalamu sana kuiachia CCM ipite e.g. NCCR mageuzi ya Mrema na hata sasa ya Mbatia

2. kupandikiza maafisa usalama waliosomea jinsi ya kuua upinzani ndani ya mioyo ya watu. we could see shift from one party to another (eg lyatonga Mrema) na jinsi ilivyowafanya watu wakate tamaa na siasa....toka NCCR hadi TLP kote akichukua nafasi za uenyekiti na kuua morale za watu kupigania haki zao.......

3. kutumia hela kuvuruga vyama na itikadi za siasa za watu.... kama ilivyokuwa pale namba moja, imagine mtu kama DOVUTWA FAHMI DOVUTWA aliwezaje kutimiza masharti ya kuwa mgombea uraisi?? hatuani ni kituko cha mwaka alipojitoa pale mwisho kura zake ziende kwa kikwete? jinsi gani anavyojiunga na mbatia na mrema kuwapiga vita chadema??

4. Uwepo wa vyama kama kina dovutwa na SAU ni shindikizo la kuunga mkono maazimio yasiyo na mashiko. tumeona mara nyingi hawa huitwa kuunga mkono maazimio yale hayaungwi mkono na vyama upright... hupewa hela nzuri tu kama ujira wao.....

5. kupandikiza viongozi wenye siasa za mrengo wa kati ili kuiwezesha CCM kubaki madarakani

6. Kutumia POSHO kukamata wasomi. na watu wenye ufahamu kujiunga nao na kuuhujumu upinzani.

kwa nini Mungu ni mzuri kwa kutupa Mbowe?

1. hahongeki

2. Ana nia ya dhati ya kumkomboa mtanzania. imefanya chama kiaminike na kugain popularity miongoni mwa watanzania hata wale wasomi.

3. ni shupavu, ana msimamo na ana uwezo wa kuchukua hatua behind the curtain (umafia anauweza)

4. ana adabu kubwa kwa wazee, mnyenyekevu, anaheshimu mchango wa wasomi wa tanzania, na kwa busara kubwa ameweza kuzuia mapandikizi yenye siasa za mrengo wa kati kuja kuidismental chadema. I SINCERELY TO DO NOT SEE THE BEST ALTERNATIVE SO FAR.

5. Ni shujaa wetu - japo tunauthamini mchango wa viongozi wetu wote wa chama, bado tuna imani kubwa kwa mwenyekiti wetu Mh Mbowe tukiamini kuwa atatuvusha salama katika kipindi hiki chenye ukuwadi mkali wa kukiua toka CCM

6. ni mtu wa kazi, pamoja na nafasi yake kubwa, huweza kufanya kazi masaa mengi, bila kula wala kupumzika.. kwa kweli wakati wa kazi za chama mara nyingi huwa mtu wa mwisho kuchoka.....na kukumbuka chakula....(kaka wa ajabu)

7. ameongoza na anaendelea kuongoza wabunge wake kuchapa kazi bila kulala... huongoza na kusisitiza kuwa kupata ubunge sio mwanzo wa holiday........aliapa kuwa kuupata ubunge ni mwanzo wa safari na sasa tunaona....

Mungu Mbariki Mbowe,

Mungu ibariki CHADEMA,

Mungu ibariki Tanzania.
 
siku hizi mambo hayaendi kwa hisia kama wanavyo taka watu wakijani. we think, analyse den act.
 
kweli tupu jameni pamoja na kwamba sio lazima awe rais lakini anawezashika nafasi nyingine ya kiutendaji na akafanya mambo tunayohitaji nchi hii. yeyote atakayekuwa rais 2015 tuhakikishe ni mtu mwajibikaji mambo ya kuchagua kwa kuangalia sura au dini yametuangusha sana Watz.
 
Huyu Mbowe sitaki hata kumsikia! Kaharibu sana vijana wengi tanzania na ule ukumbi wake pale katikati ya jiji!
Hafai kuwa kiongozi mkubwa! Biashara na siasa wapi na wapi?
Pole! Naona sasa mnaweweseka kama kuku mwenye mdondo. Kawaharibu kivipi fafanua. Alianzisha jela au wanakwenda jiliwaza wenyewe? Wanaokwenda huko wako chini ya miaka iliyoruhusiwa kisheria kwenda kwenye majumba ya starehe? Wewe ulitaka vijana wabaki wakiomboleza uhaini wa CCM majumbani muda wote? Kwa nini Mbowe hafai kuwa kiongozi mkubwa wakati mchekeshaji wa kimataifa a.k.a. Mzee wa kuchakachua na ngome ya walio kama wewe yaani mafisadi anafaa? Tafakari kwanza kabla hujaandika hoja maana itasomwa na waliokuzidi kwa mbali uwezo wako kiduchu wa kufikiri kimagamba magamba. Endeleeni kuhunya hunya mwisho wa siku mtaelewa kwa nini watanzania wana imani na Chadema, Mbowe na viongozi wana mapinduzi hao. To Hell with CCM, God bless CHADEMA.
 
Back
Top Bottom