Freeman Mbowe: Nguzo na mhimili muhimu kwa ustawi wa CHADEMA

Kwayu

JF-Expert Member
Nov 8, 2007
499
92
Ninaandika hapa jamvini nikiwa na mawazo lukuki juu ya mustakabali wa cdm endapo kamanda Mbowe ataamua kutogombea tena Nafasi ya uenyekiti wa chama taifa.Hakuna mwana jamvi asiyeelewa ni kwa jinsi gani kamanda na mpiganaji Mbowe amekikbeba chama hiki na kufikia hapa kilipo na kutishia kabisa mustakabali wa ccm.Juhudi, maarifa, kujituma, uthubutu na uzalenda wa kamanda huyu umeweza kuijenga cdm ambayo kwa sasa ni tumaini jipya kwa watanzania.Wengi wetu tunatambua kwamba mwaka 2013 kwa mujibu wa katiba ya chama ni mwaka ambao chama kitaenda kuchagua mwenyekiti mpya wa chama taifa. Mpaka sasa cjaona ni nani ambaye anaweza kurithi nyayo za kamanda huyu siye tetereka na mwenye uthubutu wa hali ya juu.Ni wengi sana wanaoutamani uenyekiti wa chama taifa na wengi wao wakiwa ni wale walio kwenye pay roll ya chama cha mapinduzi, nia na madhumuni yao yakiwa ni kukidhohofisha chama na kuacha upenyo kwa ccm kuendelea kushika atamu.Ninaomba ikiwezekana wale walio na nia njema na cdm pamoja na taifa kwa ujumla tumuombe kamanda Mbowe ifikapo 2013 agombee tena uenyekiti ili cdm iendelee kung'ara kuiondoa ccm madarakani.Nimejaribu kupitia katiba ya chama na cjaona limitation ya muda wa kuwa mwenyekiti.Hofu na mashaka ni kwa nafasi ya uenyekiti kutwaliwa na virus kama Zitto ambao tunajua wapo kwenye pay roll ya ccm.
 
Hiyo ni demokrasia kweli? Mbowe si pekee ndani ya CDM anayeweza kuingoza, tuwe wawazi na wakweli tujenge demokrasia ya kweli ndani ya chama tawala na vyama vya upinzani,.............
 
Hata mm nafikiri kama Mbowe hatakubali basi mikoba akabidhiwe Slaa then Mbowe awe katibu mkuu.au mwaonaje?
 
Inaonekana ulikuwa umelala ukakurupuka toka usingizini ndo ukaandika hii thread.nna mashaka na uwezo wa kifikra....hebu jaribu mda mwingine kabla hujapost thread isome mara mbili ht tatu af jikosoe..niko tayari unikosoe km ntakuudhi ktk koment yng hii.
 
kupisha ni muhimu sana , hapa hatupo kwa majaribio ,wapo wengi wenye uwezo kama yeye, ila tunamshukru kwa moyo wake wote
 
Cdm ni ya wana cdm wote au ni ya mbowe na slaa pekee.mimi kwa mtizamo wng naona kuwe na uwanja huru kwa kila mwanachama anayependa kugombea agombee ktk hao wataojitokeza atapatikana mbora ya wote ndo atakuwa mkiti.hi ya kuteua km tunavoteua hapa ni ufalme type,nachelea kuita udikteta.tufuate sheria tartibu na kanuni tulojiekea kwny katiba.thts true demokrasi values.
 
Dj Mbowe na NGO yake..Lola. Naona defensive mechanism na sarakasi zake zimeanza mapema.
 
Ukiwauliza CCM nani anakupeni shida sana mbali na Slaa kwemnue issues ndani upinzanij watasema mwenyekiti wa Chadema maana hataki kuhongwa na anaenda nao kijeshi jeshi CCM .Wanamuogopa kama nini maana hata njaa pia .
 
Kwanza nakubaliana na hoja yako kuwa Mbowe amekuwa ni M/kiti wa pekee sana katika historia ya CDM,lakini pia amekuwa mstari wa mbele sana katika kuimarisha chama..lakini pia ni kweli kuwa kupata mrithi wakufanana kabisa na Mbowe ni ngumu,isipokuwa nina imani kuwa watu wapo na watapatikana wala usijali.......
 
Demokrasia ya CDM iwapi kama watu wana amini kuna mtu mmoja tu anayeweza kuongoza vizuri?

acheni unafiki
 
Ni ukweli isiopingika kwamba mbowe ameplay part kubwa sana kuifanya iwe kama ilivyo,nakumbuka wakati anapewa uenyekiti mkakati wake ulikuwa ni kutafuta vijana kutoka vyuo mbalimbali ambao aliona wangeweza kumsaidia ktk harakati za kukijenga na kukitangaza chama,hapa ndo tunaona aliwapata watu kama akina john mrema,zitto,mdee, mnyika na wengine.mbowe ni tofauti sana na wenyeviti wa vyama vingine.kila kukicha ccm wanawaza namna ya kumdhibiti huyu kamanda kwa vile amekuwa na misimamo isiyotetereka.
 
Huwa sipendi thread za namna hii lakini ukweli ni kwamba Mbowe bado anatufaa sana CHADEMA............
 
Back
Top Bottom