Freeman Mbowe na Viongozi CHADEMA jiteteeni juu ya hoja hizi za kupotea kwa Ben Saanane

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, amani iwe kwenu.

Nawapa pole ndugu wa Ben Saanane hususan Baba yake mpendwa, Focus Saanane na mdogo wake Erasto Saanane ambao kwa zaidi ya wiki sasa wanahangaika kumtafuta mpendwa wao Benard Rabiu Saanane au Ben Saanane kama tulivyozoea kumuita ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Ninasema ni mazingira ya kutatanisha kwa sababu mpaka leo hakuna anayejua ni lini BEN alipotea na katika mazingira yepi. Pia haijajulikana kama Ben amepotea ama yupo busy na majukumu ya kikazi.

Kutokana na kupotea kwa Ben Saanane, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wanaunyooshea vidole vya lawama uongozi wa CHADEMA hususan Mwenyekiti Freeman Mbowe. Kupitia mijadala mbalimbali wanayoanzisha hasa kwenye kurasa zao za facebook, kwa hakika nimebaini mambo yafuatayo;

1. Julai 2016, Freeman Mbowe alimteua Ben Saanane kuwa Msaidizi wake akimpa cheo cha ‘Executive Assistant’ wa Ofisi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa au kama Malisa Godlisten anavyoita Personal Assistant. Wakati huo huo, Ben Saanane alikuwa na Wadhifa wa Mkuu wa Sera na Utafiti wa CHADEMA kama Gazeti la Tanzania Daima la Desemba 10, 2016 lilivyobainisha.

Kupitia nyadhifa zake hizo, Ben Saanane ameratibu na kusimamia mikakati na Operesheni kadhaa za chama ambazo ni pamoja na Mkakati wa Siri juu ya Zitto Kabwe wa mwaka 2013, Operesheni UKUTA ya Septemba 2016 na Operesheni Kata Funua ambayo utekelezaji wake haujafanyika.

Kwa ujumla, Ben Saanane ni mmoja wa maafisa waandamizi wa CHADEMA ambaye amebahatika kuwa na Siri Kuu za chama. Ni katika siri hizi ndizo zilizoweka rehani maisha ya Ben Saanane.

2. Agosti Mosi 2016, Ben Saanane alipewa jukumu maalum la kumuandama Rais Magufuli kwenye mitandao ya kijamii. Lengo la jukumu hili ni kuuandaa umma uamini kuwa lolote litakalomtokea Ben, watu wataamini kuwa ni kutokana na maandiko yake kwenye mitandao ya kijamii.

3. Wiki ya pili ya Mwezi Novemba 2016, Freeman Mbowe alimuandalia Ben Saanane safari ya kwenda Nchini Afrika ya Kusini ambapo kwa mujibu wa mtu wa karibu na Ben Saanane aitwaye HILDA NEWTON, Safari hiyo ilipaswa kufanyika Novemba 19.

Kabla ya safari hiyo, Ben alipewa na bosi wake (Mbowe) mapumziko ya wiki moja ili akamilishe andiko la Operesheni Kata Funua ambalo lilikuwa katika hatua ya mwisho kukamilika. Pia Mbowe alimpa maelekezo maalum Ben ya kutowasiliana na watu wengine ili apate muda wa kutosha wa kukamilisha andiko hilo.

Aidha, Mbowe alimlipa Ben gharama zote za safari ambapo haikubainishwa ni kiasi gani na haijulikani alipaswa kuwa Afrika ya Kusini kwa siku ngapi na kwa majukumu yepi. Ni katika kipindi hicho ndipo ukimya wa Ben Saanane ulipoanza kuripotiwa.

4. Wakati Ben anaandaliwa kwenda Afrika ya Kusini, Mbowe na baadhi ya viongozi akiwemo John Mrema wakaandaa safari ya kwenda Uingereza. Ni ajabu kwa Mbowe kwenda Uingereza bila ya msaidizi wake wa karibu.

5. Novemba 26, 2016, Hilda Newton alijitokeza kuwajibu wale wote waliokuwa wanamtumia ujumbe kumuuliza alipo Ben Saanane. Katika ujumbe huo ambao aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook, Hilda Newton alisema kuwa Ben Saanane yupo Afrika ya kusini na kwamba atarejea siku chache zijazo.

Bado haijafahamika nani alimtuma Hilda kutoa taarifa hiyo ijapokuwa habari za chini ya kapeti zinasema kuwa ni maelekezo kutoka ngazi za juu za CHADEMA. Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA walihoji sana andiko hilo. Familia ya Ben Saanane nayo ilishtushwa na andiko hilo kwani haiingii akilini Ben asafiri bila ya kutoa taarifa kwa familia yake.

6. Familia ya Ben imefanya mawasiliano ya mara kwa mara kwa uongozi wa CHADEMA kupitia Katibu Mkuu Vincent Mashinji. Hata hivyo, walijibiwa kuwa Ben yupo salama na anatekeleza majukumu ya kikazi. Hata hivyo, kadri ziku zilivyosonga, wasiwasi uliwajaa na ndipo Jumanne Desemba 6, 2016 walipoamua kwenda kituo cha Polisi Tabata kutoa taarifa za kupotea kwa Ben. Hadi wakati huo, chama kiliendelea kuwa na msimamo kuwa Ben yupo salama na kwamba wasiwe na wasiwasi.

7. Hadi hivi sasa, hakuna kiongozi yeyote wa CHADEMA aliyetoa taarifa rasmi kwa vyombo vya Habari juu ya ukimya wa Ben Saanane. Je ni kweli kwamba amepotea au yupo kikazi Afrika ya Kusini kama baadhi ya viongozi wa chama hicho walivyonukuliwa?

8. Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye Ben ndiye Bosi wake Mkuu mpaka sasa hajatoa tamko lolote. Hii inatia shaka kwani inaeleweka kuwa kwa taratibu za kiofisi, mtu akikosekana kwa muda wa siku saba mfululizo bila ya taarifa zozote lazima aandikiwe barua ya kutaka kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua.

Mbowe hajafanya hivyo na hii inatujengea imani kuwa anajua nini kinaendelea. Aidha, licha ya kupata taarifa kuwa msaidizi wake amepotea, Mbowe anaendelea na ziara zake nchini Uingereza kana kwamba hakuna kilichotokea. Hajashtushwa kabisa na kupotea kwa Ben. Anajua dhahiri nini kinaendelea.

9. Jitihada za kumtafuta Ben Saanane zinafanywa na ndugu zake tu pamoja na marafiki zake wa karibu. Hii inazua mashaka mengine juu ya mfumo wa uendeshaji wa CHADEMA.

10.Gazeti la Tanzania Daima kwa mara ya kwanza limeandika taarifa juu ya kupotea kwa Ben Saanane Desemba 10, 2016. Hili ni gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA. Ukimya wa gazeti hilo kwa hakika unazua mjadala mwingine.

Nimalizie kwa kuwapongeza wafuasi wote wa CHADEMA wanaoendelea kuunyooshea vidole uongozi wa chama hicho juu ya kadhia hii ya kupotea kwa Ben Saanane. Nawaomba muendelea kuwa na nyoyo za ujasiri ili muhoji bila woga. Usalama wenu ni muhimu kuliko kitu chochote. Hamjui nani atafuata baada ya Ben Saanane.

Mungu mjaalie Ben afya njema huko aliko na aungane na familia yake mapema iwezekanavyo.
image.jpg
 
Hii habari inaelea sana..
Kama viongozi wanasema Ben yupo salama nyie wafuasi mnalalamika nini?

Au hamuwaamini viongozi wenu?

Mbona kuna kipindi kile cha matokeo ya uchaguzi baada ya kusambaa taarifa za uongo kuhusu Rais mstaafu Mkapa kuwa amefariki ikulu ilitoa taarifa ya kukanusha pasipo Mkapa kujitokeza mwenyewe na nyie mkatulia?

Waaminini viongozi wenu.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nawapa pole ndugu wa Ben Saanane hususan Baba yake mpendwa, Focus Saanane na mdogo wake Erasto Saanane ambao kwa zaidi ya wiki sasa wanahangaika kumtafuta mpendwa wao Benard Rabiu Saanane au Ben Saanane kama tulivyozoea kumuita ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Ninasema ni mazingira ya kutatanisha kwa sababu mpaka leo hakuna anayejua ni lini BEN alipotea na katika mazingira yepi. Pia haijajulikana kama Ben amepotea ama yupo busy na majukumu ya kikazi.

Kutokana na kupotea kwa Ben Saanane, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wanaunyooshea vidole vya lawama uongozi wa CHADEMA hususan Mwenyekiti Freeman Mbowe. Kupitia mijadala mbalimbali wanayoanzisha hasa kwenye kurasa zao za facebook, kwa hakika nimebaini mambo yafuatayo;

1. Julai 2016, Freeman Mbowe alimteua Ben Saanane kuwa Msaidizi wake akimpa cheo cha ‘Executive Assistant’ wa Ofisi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa au kama Malisa Godlisten anavyoita Personal Assistant. Wakati huo huo, Ben Saanane alikuwa na Wadhifa wa Mkuu wa Sera na Utafiti wa CHADEMA kama Gazeti la Tanzania Daima la Desemba 10, 2016 lilivyobainisha. Kupitia nyadhifa zake hizo, Ben Saanane ameratibu na kusimamia mikakati na Operesheni kadhaa za chama ambazo ni pamoja na Mkakati wa Siri juu ya Zitto Kabwe wa mwaka 2013, Operesheni UKUTA ya Septemba 2016 na Operesheni Kata Funua ambayo utekelezaji wake haujafanyika. Kwa ujumla, Ben Saanane ni mmoja wa maafisa waandamizi wa CHADEMA ambaye amebahatika kuwa na Siri Kuu za chama. Ni katika siri hizi ndizo zilizoweka rehani maisha ya Ben Saanane.

2. Agosti Mosi 2016, Ben Saanane alipewa jukumu maalum la kumuandama Rais Magufuli kwenye mitandao ya kijamii. Lengo la jukumu hili ni kuuandaa umma uamini kuwa lolote litakalomtokea Ben, watu wataamini kuwa ni kutokana na maandiko yake kwenye mitandao ya kijamii.

3. Wiki ya pili ya Mwezi Novemba 2016, Freeman Mbowe alimuandalia Ben Saanane safari ya kwenda Nchini Afrika ya Kusini ambapo kwa mujibu wa mtu wa karibu na Ben Saanane aitwaye HILDA NEWTON, Safari hiyo ilipaswa kufanyika Novemba 19. Kabla ya safari hiyo, Ben alipewa na bosi wake (Mbowe) mapumziko ya wiki moja ili akamilishe andiko la Operesheni Kata Funua ambalo lilikuwa katika hatua ya mwisho kukamilika. Pia Mbowe alimpa maelekezo maalum Ben ya kutowasiliana na watu wengine ili apate muda wa kutosha wa kukamilisha andiko hilo. Aidha, Mbowe alimlipa Ben gharama zote za safari ambapo haikubainishwa ni kiasi gani na haijulikani alipaswa kuwa Afrika ya Kusini kwa siku ngapi na kwa majukumu yepi. Ni katika kipindi hicho ndipo ukimya wa Ben Saanane ulipoanza kuripotiwa.

4. Wakati Ben anaandaliwa kwenda Afrika ya Kusini, Mbowe na baadhi ya viongozi akiwemo John Mrema wakaandaa safari ya kwenda Uingereza. Ni ajabu kwa Mbowe kwenda Uingereza bila ya msaidizi wake wa karibu.

5. Novemba 26, 2016, Hilda Newton alijitokeza kuwajibu wale wote waliokuwa wanamtumia ujumbe kumuuliza alipo Ben Saanane. Katika ujumbe huo ambao aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook, Hilda Newton alisema kuwa Ben Saanane yupo Afrika ya kusini na kwamba atarejea siku chache zijazo. Bado haijafahamika nani alimtuma Hilda kutoa taarifa hiyo ijapokuwa habari za chini ya kapeti zinasema kuwa ni maelekezo kutoka ngazi za juu za CHADEMA. Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA walihoji sana andiko hilo. Familia ya Ben Saanane nayo ilishtushwa na andiko hilo kwani haiingii akilini Ben asafiri bila ya kutoa taarifa kwa familia yake.

6. Familia ya Ben imefanya mawasiliano ya mara kwa mara kwa uongozi wa CHADEMA kupitia Katibu Mkuu Vincent Mashinji. Hata hivyo, walijibiwa kuwa Ben yupo salama na anatekeleza majukumu ya kikazi. Hata hivyo, kadri ziku zilivyosonga, wasiwasi uliwajaa na ndipo Jumanne Desemba 6, 2016 walipoamua kwenda kituo cha Polisi Tabata kutoa taarifa za kupotea kwa Ben. Hadi wakati huo, chama kiliendelea kuwa na msimamo kuwa Ben yupo salama na kwamba wasiwe na wasiwasi.

7. Hadi hivi sasa, hakuna kiongozi yeyote wa CHADEMA aliyetoa taarifa rasmi kwa vyombo vya Habari juu ya ukimya wa Ben Saanane. Je ni kweli kwamba amepotea au yupo kikazi Afrika ya Kusini kama baadhi ya viongozi wa chama hicho walivyonukuliwa?

8. Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye Ben ndiye Bosi wake Mkuu mpaka sasa hajatoa tamko lolote. Hii inatia shaka kwani inaeleweka kuwa kwa taratibu za kiofisi, mtu akikosekana kwa muda wa siku saba mfululizo bila ya taarifa zozote lazima aandikiwe barua ya kutaka kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua. Mbowe hajafanya hivyo na hii inatujengea imani kuwa anajua nini kinaendelea. Aidha, licha ya kupata taarifa kuwa msaidizi wake amepotea, Mbowe anaendelea na ziara zake nchini Uingereza kana kwamba hakuna kilichotokea. Hajashtushwa kabisa na kupotea kwa Ben. Anajua dhahiri nini kinaendelea.

9. Jitihada za kumtafuta Ben Saanane zinafanywa na ndugu zake tu pamoja na marafiki zake wa karibu. Hii inazua mashaka mengine juu ya mfumo wa uendeshaji wa CHADEMA.

10.Gazeti la Tanzania Daima kwa mara ya kwanza limeandika taarifa juu ya kupotea kwa Ben Saanane Desemba 10, 2016. Hili ni gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA. Ukimya wa gazeti hilo kwa hakika unazua mjadala mwingine.

Nimalizie kwa kuwapongeza wafuasi wote wa CHADEMA wanaoendelea kuunyooshea vidole uongozi wa chama hicho juu ya kadhia hii ya kupotea kwa Ben Saanane. Nawaomba muendelea kuwa na nyoyo za ujasiri ili muhoji bila woga. Usalama wenu ni muhimu kuliko kitu chochote. Hamjui nani atafuata baada ya Ben Saanane.

Mungu mjaalie Ben afya njema huko aliko na aungane na familia yake mapema iwezekanavyo.

Suspect mkubwa ni wewe, you see !
 
Unanikumbusha sakata la mtu mmoja akiitwa Msabaha kule Kisiwani. Mkuu Lizaboni yaani pamoja na ujanja wa rafiki yetu Ben unathubutu kusema kwamba kapotea. Mtu mzima yule hawezi kupotea.
Nakubaliana na wewe Mkuu. Hoja ya kupotea kwa Ben Saanane imekolezwa hasa baada ya familia yake kuripoti polisi
 
Back
Top Bottom