figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,490
- 54,884
Habari yenu wakuu,
Jana Nlipenda mchango aloutoa Freeman Mbowe, watu wengi hawakuweza kuusikia mchango alioutoa Mbowe alipokua akichangia makadilio na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI kwani habari za Bunge hazikurushwa jioni na haijulikani sababu ni nini. Nimeweza kuwawekea machache kati ya mengi Mazuri aliyo yazungumza jana.
Alianza kwa kusema, "Kama kuna mahali ambapo tunapata aibu kama Nchi ni Dar e ssalaam, kama kunasehemu Serikali inatakiwa kutoa majibu ni kuhusu jiji la Dar es salaam.
Katika historia ya Nchi yetu tangu ipate uhuru, Jiji la Dar es Salaam limefanyiwa masater plani mara mbili. mara ya kwanza ilikua 1968 ambapo Dar es salaam ilikua na wakazi laki mbili na elfu sabini na tatu (273,000) na wote waliishi sehemu iliyopimwa. Master plan ya pili ilifanyika miaka kumi baadae yaani mwaka 1978 na Baba wa taifa kipindi hicho wakazi wa Dar es Salaam walikua (770,000) laki saba na elfu sabini. Tangia hapo Dar es salaam haijafanyiwa master plan tena, si uongozi wa Mwinyi, Mkapa au Kikwete.
Sasa hivi Wakazi wa Dar Es Salaam ni zaidi ya Mil 4.5 ambapo Asilimia 72 ya wakazi wa leo Dar es Salaam wanaishi Sehemu ambazo hazijapimwa. Na ukuaji wa Dar es salaam katika Afrika ni jiji linaokua kwa kasi ikiwemo Mwanza na Mbeya kutokana na watu kuhama vijijini kwa sababu ya hali ngumu ya maisha hivyo wanahamia Mijini.
Jiji la Dar es Salaam lina msongamano wa magari mkubwa mno, sio kwa sababu ya ya Magari mengi, kwa sababu Kenya ina magari mengi mara tatu ya magari ya Dar es salaam.
Dar es salaam ina matatizo makubwa ambayo ni;
1. Haina Master plan
Mnakuja hapa na kusema mtajenga flyovers Ubungo, TAZARA sijui wapi lakini kazijengwi hata zikijengwa sio njia ya utatuzi.
2.Adha ya foleni ya magari
Nimesikia wabunge wanapendekeza wanasema eti viongozi wanunuliwe helcopter kupunguza foleni. nyie mnunue helcopter nani aingie kwenye foleni? Mimi nashauri waondolewe ving'ora kwenye msafara angalau kwa mwezi mmoja ili waonje foleni ya Dar es Salaam.
Mtu unatumia masaa matatu kwenda Ofisini na Kurudi unatumia masaa matatu. Watu wengine hawaendi kazini. Hii inaongeza gharama za Usafirishaji. Na viongozi wanaona ni jambo la kawaida. Magari unakuta Kimara yamesimama, Mbagala yamesimama, Gongo la mboto yamesimama. Magari yote hayo yanazalisha gesi inayo haribu mazingira. Hii ni Serikali gani inakosa Planning? Nakwambia Mh.Waziri mkuu katika kipindi cha miaka miwili ijayo, Dar es Salaam kutakua hakuna movement ya magari vinginevyo jiji la Dar es Salaam linakwenda kusimama.
Mji wa Dar es salaam Unachangia pato la taifa kwa asilimia 70 hadi 80 lakini haina miundo mbinu mnategemea nini? Mnasema mtaleta magari yaendayo kwa kasi ndio, Lakini yatakuwa maangapi? Sasa hivi ukiwa na mgonjwa wako anapekwa Muhimbili asipofia njiani unamshukuru Mungu.
Angalia barabara inayojengwa leo ya Morogoro kuingia Dar es salaam, Hii barabara ndiyo inalisha Dar es salaam kutoka Zambia, kutoka Uganda, kutoka Malawi, Kutoka Burundi Kutoka Congo ina Mistari miwili. Watu wanajenga barabara zenye njia kumi nyie mnajenga barabara zenye njia mbili? Plan ipo wapi? Barabara yenyewe yenye njia mbili nyembamba gari zinapishana zinaacha futi moja halafu mnasema mnafanya planning! Nendeni Muangalie jirani zetu Thika high way, Barabara ina njia kumi nyie bado mna njia mbili kwenye barabara inayolisha nchi nane.
Watu wanapata msongo wa mawazo kwenye foleni, unakuta mtu amekaa kwenye foleni masaa matano, wanavuta hewa chafu ya moshi, nyinyi mnapita na magari yenye yenye vimulimuli hamuoni hii kitu na mnashindwa kufanya planning ni kwanini msiondoke Serikalini tuingie watu wengine tubadilishe mambo haya. Mnapanga mipango ya miaka mitano, hamfikirii miaka 30 ijayo.
Dar es Salaam Haina mifereji ya maji, maji yanasimama kwenye Makazi ya watu. Nashangaa Mbunge leo miaka 50 ya uhuru Mbunge anasimama anashukuru kuchimbiwa visima vya maji leo miaka 30!!?? 21c tunaongelea visima ni aibu.
Dar es salaam mnaiachaje kabla hamjaondoka Octoba? Baada ya Octoba sio kazi yenu tena kwani tutakua tushachukua nchi. tunataka tujue kabla hamjaondoka nchi yetu mnaiachaje. Inabidi mtuambie ufumbuzi wa haraka wa hili tatizo la Dar es Salaam kabla hamjaondoka.
Kwa habari zaidi angalia hizi video;
Video ya kwanza ni hii hapa
Video ya pili hii hapa

Last edited by a moderator: