Freeman Mbowe amgomea OCD - Wananchi wakachachamaa, OCD akatoweka

Heshimuni mamlaka nyie watu!

mnashangiria kiongozi kutokuheshimu sheria nza nchi ?

quote_icon.png
By Candid Scope
Kwa mujibu wa Mbowe,
muda
wa kuhutubia mkutano huo
ulikuwa bado
unampa fursa ya kuzungumza na wananchi wa Nanyumba

Anaetakiwa kuheshimu sheria hapa ni nani..? Angalia kwenye red kisha utapata jibu hata kama sio lile unalolipenda liwe...
 
Tume ya katiba
Heshimuni mamlaka nyie watu!

mnashangiria kiongozi kutokuheshimu sheria nza nchi ?

quote_icon.png
By Candid Scope
Kwa mujibu wa Mbowe,
muda
wa kuhutubia mkutano huo
ulikuwa bado
unampa fursa ya kuzungumza na wananchi wa Nanyumba

Anaetakiwa kuheshimu sheria hapa ni nani..? Angalia kwenye red kisha utapata jibu hata kama sio lile unalolipenda liwe...
 
Anaetakiwa kuheshimu sheria hapa ni nani..? Angalia kwenye red kisha utapata jibu hata kama sio lile unalolipenda liwe...

Kama muda ulikuwa bado, kwa nini ODC alitoa ujumbe huo, Labda Great Thinkers kuna haja ya kufuatilia huyu OCD isije ikawa ni miongoni mwa wenye vyeti vya kugushi.(Kihiyo), Maana jeshi letu wamejaa vihiyo wengi labda ndo sababu ya baadhi ya maamuzi wanayoyafanya hata mtu ambaye hajui mlango wa darasa ana ya hoji.
 
images

Katika hatua nyingine, Mbowe alijikuta akipinga hoja ya ofisa wa polisi aliyesemekana kuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nanyumbu, alipomtaka ashuke jukwaani kwa madai kuwa muda wa kuhutubia ulikuwa umepiga.​

Ofisa huyo alimtuma mmoja wa viongozi wa Chadema amfikishie ujumbe Mbowe, kwamba alitakiwa kukatisha hotuba yake na kushuka jukwaani, ndipo Mbowe aliposema na kuhoji:

“Mimi ni Mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, OCD sikiliza usitutishe, tumetembea maelfu ya kilomita kwa ajili ya kuwaokoa Watanzania wakiwemo watoto wako…unakuja kuniambia funga mkutano?”
Kwa mujibu wa Mbowe, muda wa kuhutubia mkutano huo ulikuwa bado unampa fursa ya kuzungumza na wananchi wa Nanyumba, jimbo lililowahi kuwakilishwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Hivyo, aliendelea kuhutubia na mwishowe kuuza kadi na kuorodhesha majina ya wanachama wapya, wakiwemo waliojitokeza kuyaongoza matawi ya Chadema kwa muda, kabla ya kufanyika uchaguzi baadaye mwaka huu.

Chadema ilimaliza mikutano yake ya Operesheni Okoa Kusini iliyofanyika mkoani Mtwara jana na leo wanaanza mikutano kama hiyo kwenye vijiji, kata na wilaya za mkoa wa Lindi.

pole sana ocd kwa kumuonea huruma laichi wako nkapa
 
ni ujinga kwa anajiita kiongozi kutotii sheria. Ha tumhitaji kiongozi mshari, ha aki kutii hata shERIA AKIWA RAHIS ATAKuwa anakaa juu ya meza. Maana amezoea k uvunja sheria.
 
kazi ipo hapo tatizo palisi wa tanzania shule hamna ndo maana kila jambo wanafanya kwa kushurutishwa,promotion yao inategemea na maagizo toka kwa baba riz
 
ni ujinga kwa anajiita kiongozi kutotii sheria. Ha tumhitaji kiongozi mshari, ha aki kutii hata shERIA AKIWA RAHIS ATAKuwa anakaa juu ya meza. Maana amezoea k uvunja sheria.

Bora yeye hatii sheria kwa kuwapa watu mema je sheria aliyovunja Jairo, Chenge, Lowasa kwa kuhujumu mali za walalahoi ndo sio ujinga? Punguza povu basi kwa wavuja jasho fisadi dagaa wewe

Sent from my BlackBerry 9910 using JamiiForums
 
[h=2][/h]JUMATANO, JUNI 06, 2012 06:02 NA BENJAMIN MASESE, NANYUMBU

*Alitaka kumshusha jukwaani, Mbowe akagoma
*Wananchi wakachachamaa, OCD akatoweka


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemgomea Mkuu wa Polisi (OCD), Wilaya ya Nanyumbu, Mohamed Said, aliyekuwa akitaka kumshusha jukwaani alipokuwa akihutubia wananchi eneo la Mangaka, wilayani hapa.


Tukio hilo lilitokea juzi jioni wakati OCD, Said alipokuwa akitaka Mbowe ashuke jukwaani kwa madai kuwa, muda wa kuhutubia ulikuwa umemalizika.


Wakati wa tukio hilo, OCD huyo alikuwa chini ya lori la matangazo ya CHADEMA, ambapo alimwagiza mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni diwani, apande jukwaani ili kumwambia Mbowe aahirishe mkutano wake, kwa kuwa muda ulikuwa umemalizika.


Baada ya mtu huyo kumpa taarifa Mbowe, Mbowe aliwaambia wananchi kuwa OCD anataka ahitimishe mkutano, jambo ambalo liliwafanya wananchi kuchachamaa na kutaka kumshambulia ofisa huyo wa polisi.


“Jamani OCD anataka niache kuhutubia, sasa nasema wewe OCD mimi ni Mbunge na ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, hebu sikiliza, usitutishe sisi, tumetembea maelfu ya kilomita kwa ajili ya kuwaokoa Watanzania na watoto wako halafu unakuja kuniambia nifunge mkutano!.


“OCD sikiliza, kwanza usinitishe, mimi simuogopi mtu yeyote, awe Rais Kikwete wala Waziri Mkuu Pinda, hao nawaheshimu nao wananiheshimu.


“Tafadhali ujue kazi yako na inavyoonekana unataka kujifunzia kazi kwangu, nasema umekosea,” alifoka Mbowe.


“Lakini kwanza niwaulize wananchi, hivi mnasemaje?, nifunge mkutano au nisifunge,” alihoji Mbowe huku wananchi wakiitikia, usifunge.


OCD Said baada ya kusikia wananchi wameonyesha kutoridhishwa na agizo lake kwa Mbowe, alihama katika eneo alikokuwa na kusogea pembeni akionekana kuzungumza na simu kuashiria kuwa kuna mtu anampa taarifa za mkutano huo.


Baada ya dakika chache, OCD huyo alikuwa katika mazungumzo na baadhi ya askari kanzu kisha wakaondoka eneo la tukio.


Awali, Mbowe alimshambulia Rais mstaafu, Benjamini Mkapa akisema kuwa, alishindwa kutatua kero zinazowakabili wakazi wa Mkoa wa Mtwara na Jimbo la Nanyumbu, aliloliongoza kwa muda mrefu kama mbunge kabla ya kuwa rais mwaka 1995.


wakati wa mkutano huo ambao mamia ya wanachama wa CCM walirudisha kadi na kujiunga na Chadema, Mbowe alisema inashangaza kuona eneo alikozaliwa Mkapa wananchi wake wana maisha magumu sawa na maeneo mengine yasiyokuwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini.


Kwa mujibu wa Mbowe Rais mstaafu Mkapa, alishindwa kuondoa kero za wananchi ikiwamo tatizo la maji na upatikanaji wa soko la kudumu la zao la korosho.


“Mkapa amekuwa rais kwa kipindi cha miaka kumi, amekuwa waziri kwa miaka karibia ishirini, amekuwa balozi kwa miaka nane na ndiye rais aliyehusika na ufisadi wa kutisha nchini kwani aliuza mashirika yote ya umma, viwanda na nyumba za Serikali, lakini ameshindwa kuleta maendeleo katika mikoa ya kusini pamoja na Jimbo hili la Nanyumbu.


“Mkapa ni shemeji yangu lakini kwa sasa hawezi kurudi huku nyumbani kwake, kwa sababu ameshindwa kujenga na ndiyo maana amekimbilia Tanga na Kilimanjaro kwa wakwe zake,” alisema Mbowe.


Katika hatua nyingine, Mbowe alisema atawakaba koo mawaziri wawili, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe na Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia.


Alisema kuwa, katika ziara yake katika mikoa ya kusini,wananchi walitoa malalamiko mengi ambayo Membe na Ghasia watatakiwa kuyajibu kwa kuwa ndiyo wawakilishi wao.


Alisema kuwa, Membe atalazimika kutoa majibu juu ya sera mbovu za mahusino ya kimatifa zinazowafanya Watanzania kunyanyaswa pindi wanapovuka mipaka ya nchi lakini wageni wanaotoka nje wanathaminiwa.


Mbowe alitoa kauli hiyo kufuatia mwananchi mmoja, Mkapura Omary, kumweleza kuwa Watanzania waokwenda nchini Msumbiji, wananyanyasika licha ya kufuata taratibu zote za uhamiaji.


Kuhusu Hawa Ghasia alisema atalazimika kutoa majibu kuhusu viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwamo madiwani na wenyeviti wa vijiji, kutofanya mikutano ya kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya fedha zao.


Wakati huo huo, alisema kama mradi mkubwa wa mafuta utafanikiwa na kuanza kuchimbwa katika mikoa ya kusini chini ya utawala wa CCM, hali ya wananchi katika maeneo hayo itakuwa mbaya kuliko ilivyo sasa.

 
Nape na Mchemba wakifanya Mikutano huwa wanaingiliwa na OCD? Au Haki huwa hakuna kwa Vyama Vingine OCD hajui kuwa 2015 anaweza asiwe na kazi sababu ya kutofuata haki na sheria?

Maeneo yote CCM wakienda OCD anatoa Ruhusa?
 
Nape na Mchemba wakifanya Mikutano huwa wanaingiliwa na OCD? Au Haki huwa hakuna kwa Vyama Vingine OCD hajui kuwa 2015 anaweza asiwe na kazi sababu ya kutofuata haki na sheria?

Maeneo yote CCM wakienda OCD anatoa Ruhusa?
Kwa kuwa Nape na Nchemba wanavunja sheria!Na mbowe naye avunje! Hapo hatuwezi kwenda mbele. Viongozi wa vyama vya upinzani yafaa wawe mifano ya kufundisha mema katika jamii, na si kufata maovu ya ccm
 
Kwa kuwa Nape na Nchemba wanavunja sheria!Na mbowe naye avunje! Hapo hatuwezi kwenda mbele. Viongozi wa vyama vya upinzani yafaa wawe mifano ya kufundisha mema katika jamii, na si kufata maovu ya ccm

Sasa Wafanye nini? Angalia kama kweli wangekuwa wanavunja Sheria kwanini OCD atokomee vichakani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom