Freeman Mbowe - Afanya maajabu Houston TX

quote_icon.png
By t2015ccm
weka picha uumbuke.hakuna kitu kama hicho,watu walikuwa 20 tu.punguza maneno.unamdanganya nani???

quote_icon.png
By t2015ccm
picha yenye watu wengi kuliko zote ina watu 23,ndio unasema haijawahi kutokea??? kawadanganye wasiojiuliza ie akina YES BOSS

picha yenye watu wengi kuliko zote ina watu 23,ndio unasema haijawahi kutokea???

kawadanganye wasiojiuliza ie akina YES BOSS

Comments za Ribosome hizi..
 
Sasa ngoja nikupe fact wana diaspora sio lazima tupige kura ila tunachofanya ni kukisaidia chama tunatoa magari, pikipiki Na hata helcopter yote hii kwa ajili ya kujenga chama kuanzia ngazi ya chini, ccm 2015 hamtoki, lazima chadema ichukue nchi mtake msitake habari ndiyo, wana wa diaspora houston tawi la chadema tutatoa pikipiki 126

Mheshimiwa naona umeguswa na swali la awali. Pamoja na maelezo yako mazuri ukweli unabaki kuwa kura ndio zinazokiiingiza chama madarakani. Haya magari, pikipiki, helocopter hata vyama vingine vitakuwa nayo. Tena CCM watakuwa nayo mengi zaidi ya chama kingine chochote nchini kwani hata haya ya serikali yatatumika. Hivyo kitakachotofautisha kati ya mshindi na mshindwa ni jinsi gani atapigiwa kura na watu wengi zaidi na KUZILINDA zisichakachuliwe. Hii hoja yako ya mwisho imekaa kishabiki zaidi - suala la ama CCM itatoka au la litaamuliwa muda muafaka utakapofika.
 
picha yenye watu wengi kuliko zote ina watu 23,ndio unasema haijawahi kutokea???

kawadanganye wasiojiuliza ie akina YES BOSS


Mkuu mbona umewapendelea sana hapo kwenye red. Mimi ninamwona Mh. Mbowe na Mh. Sugu tu. Hivyo wapo wawili tu na sio 23. Hivi hii picha ya Kinana na Maubwabwa wapo wangapi vile???
 
nimeipenda hiyo kwani itawachanganya ccm na nape akiona pikipiki hizo 126 atazusha kuwa zimetolewa na wafadhili wa kizungu!

mkidangaywa kidogo tu mnalipuka,mwambie aweke jajo picha 1 hata ikiwa ni ya kampeni za 2010
 
Mkuu mbona umewapendelea sana hapo kwenye red. Mimi ninamwona Mh. Mbowe na Mh. Sugu tu. Hivyo wapo wawili tu na sio 23. Hivi hii picha ya Kinana na Maubwabwa wapo wangapi vile???


Huyo mbwiga ujue kwenje picha ya hilo gaidi ka kisomali amehesabu na idadi ya punje za ubwabwa.
 
Ha ha ha ha daaaaah kweli wajinga ni chakula cha wasomi...................eti kuwekeza nchini Haha haha ha haaha haaaaa........

Nyie ambao wengi wenu huko life ni kuunga unga ndo mje muwekeze huku.......give the poor Tanzanians a break please....mliamua kukaa huko na myamalize huko huko wenyewe kwa wenyewe......uwekezaji unahitajika kweli ila you are not of the capacity banaa
bila kupunguza dharau na kuhoji kuwa uwekezaji utafanywa je utabaki kwenye hicho kibox ulimojifungia! umeshakuwa na kasumba kuwa wawekezaji lazima wawe wazungu au wahindi! wapo watu majuu wana biashara na mitaji ya kutisha lakini kutokana na miundo mbinu mibovu, ukosefu wa umeme na rushwa kwenye taasisi nyuingi za fedha wanashindwa kuwekeza Tanzania! wewe baki na kutengeneza supu ya makongoro ukidhani kila mtu anafanya hiyo!!
 
Tanzania bado kuna watu wengi hawana ufahamu wowote katika kujua haki zao za kidemokrasia wanaitaji kupewa elimu ya uraia, wafuateni hao kwanza sio kukimbilia Ulaya na Marekani kufungua matawi tatizo la Watanzania sio matawi.

Huyu Ritz bwana anatoa hoja hata bila kuitafakari. Ina maana habari za Moro wewe huna kabisa, mabo ya Igunga jana huna kabisa. Diaspora ni watatnzania pia. Mabadiliko ya kweli hayabagui watu na maeneo yao aunwingi wao. Umeishia ff4 nini. Nape ana kazi kweli kweli na vijana wake alioleta jf.
 
Wengi wajiunga Chadema, Mkusanyiko ulikuwa ni mkubwa sana kwa historia ya mwana siasa yeyote aliyewahi kutokea Houston TX . Mbowe awabadili Wana CCM na kuwa Chadema. Mbowe afanya Houston kuwa base ya CHADEMA na wanachadema watoa Pikipiki 126

hivi hii diaspora kiduchu ya watanzania nje na yenye wababaishaji wengi kuliko watu makini inasaidia nini kwenye siasa zetu hapa Tanzania? haswa ukichukulia vile vile wengi hawaji kupiga kura wala hamna mfumo wa wao kupiga kura huko walipo...kila ninaposikia CDM wako London, DC, Houston, au Nape yuko Ny kwa ajili ya kufungua tawi la watu 20 au kwa ajili ya kuimarisha chama nakua sipati majibu.
 
Ukosoaji wote humu JF umeanza mara tu baada ya CHADEMA kuanza kufungua matawi ughaibuni, kabla ya hapo CCM wamekuwa na matawi huko lakini haikuwahi kubezwa,

Lakini CHADEMA walipoanza tu imekuwa nongwa, na usishangae serikali ikaanza mchakato wa kutunga sheria kuzuia, huu ni wivu mbaya sana.
 
wanauhimu sana wanadiaspora watatusaidia hata kutupa habari jinsi mafisadi yanavyochakachua pesa za wananchi yanapokwenda ng'ambo."SOMETHING IS BETTER THAN NOTHING"
 
Kufungua vyama vya siasa ughaibuni kama vile ilivyokuwa ANC ambayo haikupewa nafasi SA ikawa na mashambullizi tokeaTanzania siungi mkono kabisa.

Tubanane hapa hapa nchini; atakayeweza kuwashawishi wananchi kwa ukweli na kuwajali atakubalika!
 
Kweli kwa hizi picha za mikutano ya karibuni ya diaspora (CHADEMA wakiwa Houston Texas na CCM wakiwa DMV area), ni wazi kuwa imethibitika beyond any hint of a doubt kuwa CHADEMA wana kila nia njema na Tz lakini CCM wao na matumbo yao tu.

I have another classic example of what individualism means and accomplishes. I further being exposed to another classic example of patriotism and leadership means. Mbowe and CDM typifies the latter, of coz. No reward to name who fits the forme slotr!
 
Hivi siku hizi mambo yote ni kwa diaspora? Hivi ni kweli wanaenda kufungua matawi au wanasukumwa na posho na kutembea ughaibuni? Mipango ya diaspora kupiga kura ikoje ifikapo 2015 manake isiwe kufungua tu matawi lakini mwisho wa siku hao wanachama wanakuwa hawana maamuzi siku ya kupiga kura!

Mkuu, maswali yako yana mantiki sana.
Lakini je, hao diaspora wanapochangia ambulance, pikipiki na zana zingine muhimu kwa muendelezo wa yanayofanyika TZ, hawana umuhimu hata kama hawatapiga kura?

Mimi nadhani, kama lengo lao ni maendeleo ya TZ, basi waendelee vivyo hivyo.
 
Mungu aendelee kuwalinda hadi wa maono yenu wana wa ukombozi wa nchi hii.
mbona hajsema lolote kuhusu unemployment rate ya TZ? na yeye bado ataiacha nchi yetu ikae katika umoja wa non alignment au atajitoa. Unajua liumoja hili limejaa nchi za kiarabu, hivyo ni anti west and anti zionist. mwambieni ajitoe huko, maana sasa hakuna vita baridi kwa nini TZ bado ipo huko?
 
Back
Top Bottom