Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Nadhani kuna watu hawataki kuamini tu kile ambacho kinapendekezwa na Chadema. Wanaposema kuwa "free education" haina maana "costless education". Elimu bure siyo sawana elimu isiyo na gharama. Hata wakati wa Nyerere elimu ilikuwa na gharama lakini gharama hiyo haikulipwa moja kwa moja na familia na wanafunzi wenyewe. Tulijifunza kupitisha gharama hiyo kwenye taasisi au sekta nyingine.
Unapoweka lengo la kusema tunataka kutoa elimu ya kuanzia shule ya msingi hadi sekondari kuwa ni ya bure haina maana kutakuwa haina gharama. Na hii haina maana kuwa watu hawatopeleka watoto wao kwenye shule za gharama za binafsi.. la hasha kwa ufupi ni kuwa wale watakaopitia elimu katika shule za umma watapata elimu hiyo bure. So, kama mtu anataka kumpeleka mtoto wake kwa elimu ya sekondari kule St. Mary's au shule ya Msingi ya "international" basi atafanya hivyo kwa gharama yake.
Lakini, mzazi atakayetaka mtoto wake apate elimu nzuri kwenye shule za serikali basi mtoto huyo atapata elimu hiyo bure kabisa na gharama nyingine zitaingiwa kama ilivyoanishwa na Ilani ya Chadema. Ilani yao inasema hivi:
Lakini Ilani yao inaenda mbele zaidi kwa kufanya vitu viwili ambacho CCM haijavifanya kwa sababu "haiwezi":
·
NNa yapo mengine ambayo ukiyasoma utaona kuwa si tu kwamba yanawezekana lakini yanapaswa kufanyika.
La

· Elimu ya ngazi ya msingi na sekondari itagharamiwa na serikali kuu pamoja na serikali za mitaa. Lengo ni kuhakikisha kuwa elimu hii ya msingi kabisa inakuwa ni haki kwa kila mtoto wa Kitanzania na kiwango cha ubora kinalingana kwa nchi nzima.
Lakini Ilani yao inaenda mbele zaidi kwa kufanya vitu viwili ambacho CCM haijavifanya kwa sababu "haiwezi":
·
Kuinua ujira wa walimu kwa kuangalia upya viwango vyao vya mishahara na kuimarisha mazingira ya kazi na kimakazi. Katika kuboresha mishahara ya walimu, na wafanyakazi wengine wote katika sekta ya umma, tutaweka fomula ya kupandisha mishahara kwa kadri mfumuko wa bei na gharama za maisha zinavyopanda kwa kutumia mpango wa Scala Mobile, ambayo ndio inayotumika katika nchi nyingi duniani. Hii ndio kusema kila mara ambapo mfumuko wa bei utapanda na hivyo gharama za maisha kupanda, mshahara nao utapanda. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanamudu gharama za maisha ya kawaida ili waweze kuwekeza muda na utaalamu wao katika kulitumikia taifa. Utaratibu huu pia utaondoa umuhimu wa migongano baina ya Serikali na vyama vya wafanyakazi.
· Sambamba na kuboresha mishahara ya wafanyakazi kwa ujumla, Serikali ya CHADEMA itarudisha posho ya mazingira magumu kwa walimu wanaofundisha maeneo magumu ya vijijini hasa katika mikoa inayotambulika kuwa ni ya pembezoni.
NNa yapo mengine ambayo ukiyasoma utaona kuwa si tu kwamba yanawezekana lakini yanapaswa kufanyika.
La