Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Tupeni source basi tafadhali...Il hizo habari zitakuwa sio za kweli kwani strategically atakuwa wrong..Akeinda sasa maana yake na Ubunge anauvua..I dont think so kama anaweza kufanya hivyo kwa sasa..

Take it. Hivi tunavyoandika hapa ndio naambiwa amemaliza press conference akimaliza kueleza hayo maamuzi yake.
 
Ndugu, sio kila mtu anahusudu vijisenti. Kwa wengine, hata kama ni wachache, uhuru, utu na utashi ni muhimu zaidi kuliko hayo mamilioni ya pensheni!!
Kitila, kaka upo? Ni kweli kuwa fedha si kila kitu. Lakini unahitaji fedha kufanya kampeni ili ushinde uchaguzi!
 
Ila kwa mtizamo wangu, CCJ nina mashaka kama ni chama imara cha upinzani halisi. Upinzani wa kweli ni lazima utokane na mpasuko ndani ya Chama cha Mapinduzi tu. Yaani ni sawa na kuchora mstari, kundi moja la SSM kule na la pili kule!!

Una uhakika kwamba ndani ya CCM hamna mpasuko? yaani mpaka sasa hujui ndani ya CCM kuna nini mkuu?
 
Mwache aende zake - ameshakuwa "liability" na angebakia CCM "tungempiga chini" katika kura za MAONI!

Napenda mtu anayeweza kusoma ALAMA ZA NYAKATI...

OFF Topic: TuskerBariiiidi? Siku hizi sikuoni mitaa yetu ya Meeda na B-Bar! Au kwa sababu Tusker imekuwa adimu?

Duuh Baba_Enock nipo kwenye vi-grocery vilivyobaki na stock ... Nikipita Meeda na nasuuza na Kilimanjaro chuuungu... kisha naseppa... Baba_E.... Ha ha ha haaaa...
 
Tuesday, March 30, 2010
mpendanzoe ahamia CCJ



Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe (katikati) akitangaza kwa waandishi wa habari jana jijini Dar leo ju ya nia yake ya kuondoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) . Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise na kushoto ni Katibu Muenezi wa CCJ Dickson Nghilily.


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) leo. Picha na Tinganya Vicent - MAELEZO​
 
Hivi kutangaza nia ya kuhama ccm na kujiunga na ccj ndio kujiunga kwenyewe au kujiunga ni kurudisha kabisa hadi kadi na kupokelewa rasmi? Wana JF nisaidieni hapa
 
so CCJ is becoming a reality? Has it something to do with the 8/April/2010 meeting?
 
Hivi kutangaza nia ya kuhama ccm na kujiunga na ccj ndio kujiunga kwenyewe au kujiunga ni kurudisha kabisa hadi kadi na kupokelewa rasmi? Wana JF nisaidieni hapa
Unatenganisha vipi nia na kuwa mwanachama? Mwache Fred aonyeshe njia. Nadhani ile dharura ya vikao vya CC na NEC ya CCM ilitokana na hili pia.
 
so CCJ is becoming a reality? Has it something to do with the 8/April/2010 meeting?
Huyu jamaa alikuwa mmoja wa wabunge wa kutimuliwa kwenye hicho kikao. Naona kaona bora aruke sasa ili isionekane kafukuzwa. Naambiwa kuna wabunge wengine kati ya wawili mpaka watano.
 
CCJ wanajua uchaguzi utasogezwa mbele (either kwa sababu ya suala la mgombea binafsi au sababu ya serikali ya Mseto wa Zanzibar), kwa hiyo kwao itakuwa ni advantage ya kukamilisha mambo ambayo yalitiliwa shaka na msajili wa vyama! So, uchaguzi ujao CCJ ndani!
 
Hivi kutangaza nia ya kuhama ccm na kujiunga na ccj ndio kujiunga kwenyewe au kujiunga ni kurudisha kabisa hadi kadi na kupokelewa rasmi? Wana JF nisaidieni hapa

Anapoamua kuita press conference anakuwa ameshaamua tayari - hapa hakuna mjadala kilichobaki ni kurudisha kadi yao rasmi kama kuna umuhimu huo. Cha msingi naanza kuamini kwamba CCJ wamejipanga vilivyo si kama tunavyodhani. si tu eti Fred kahamia hapana, ila hili chama wenzangu kiangalieni kwa makini sana, yaliyosemwa na MM na wengine huhusu CCJ humu JF yatafakarini sana.

MM - Naomba ninukuu maoni yako kuhusu CCJ

"Unaona watu wanalia kwenye kabuli unafikiri wanamlilia Nyerere! Hawa nimeanza kuwapenda kwani they are doing all the good things I would have done kama ningeanzisha chama.. Wanajua wanachokitaka, wanafalsafa inayowaongoza na kinyume na wengi wanavyofikiria hawahitaji kigogo kuwa nyuma yao! Ni ajenda inayoelewekak na ambayo wanajua itawavutia Watanzania.

Uongozi ni uwezo mara zote siyo ahadi, siyo kutoa misaada, siyo cheap popularity ni kuweza kuchukua msimamo na watu wakajua msimamo huo. CCJ (SisiJUU).. ni chama ambacho kinafuata hatua zote muhimu za kuongoza mapambano ya kifikra kwenye sanduku la kura.." Mwisho wa kunukuu.
 
Nani anamfahamu vizuri Mpendazoe atujuze? Asije akawa Mrema, Marando type!
 
mpendanzoe ahamia CCJ
Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe (katikati) akitangaza kwa waandishi wa habari jana jijini Dar leo ju ya nia yake ya kuondoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) . Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise na kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCJ Dickson Nghilily. Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ) leo. Picha na Tinganya Vicent - MAELEZO


 
Eeh...yameshakuwa hayo eeh.....this is a very good day kwa demokrasia ya vyama vingi...nadhani its healthy kupata changamoto kama hizi!
 
Kati ya sababu alizotoa ni kuwa CCM inanuka rushwa na hakuna mtu wa kuweza kuikemea wote ni walevi wa rushwa. Amesema kuwa sheria ya uchaguzi iliyotungwa na serikali na kupitishwa na bunge kwa lazima ni Ghiliba za Kikwete tu si ukweli hata kidogo kwamba kuna mkakati wa kupambana na rushwa popote Tanzania. "Kikwete anaishangilia rushwa" he concluded.

Kwa njia yoyote anayetoka CCM kwetu ni shujaa.
 
hiki kiini macho tu akuna lolote upinzani wa kweli bado cku ccm wakipinzana aitakuwa siri na kishindo chake kitakuwa kikuu kitasikiwa ndani na nje ya nchi
 
Back
Top Bottom