Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Niulize swali! Kipi kilitangulia kwanza ni CCM yenye alama ya jembe na nyundo (nina uhakika unafahamu maudhui ya hizo alama)
au hili kundi la mafisadi majizi na maporaji (kama ulivyoyaita). The way I understand akina Mwakyembe, Six, Ole, Mama Kilango they are standing for the value of the party! The founding fathers of the party and party's policy stood and as of today stands for saving nation's interest. Although they dress like CCM, walk nad talk likewise, this prooves the old saying "Kwenye msafara wa mamba kenge huwa hawakosi" They are the ones who should leave, because the original CCM wasn't for msafara of Kenges it was for Mambas.
They might not be willing to leave, but with this dwindling public approval and this growing public anger and frustration well, CCM has no choice, they have to ask them out!! It won’t be long before CCM will be history like KANU of baba Moi

REV 13:9 "Aliye na masikio, na asikie

Kwanza nikupe pole kwa kuendelea kuamini kuwa CCM ndo ile ile (japo sikumbuki ilikuwa wapi nzuri) ya akina Nyerere na Karume (the worst one than this),ndugu yangu vampires wote asili yao ni watu,when it comes to sipping blood they turns to animals and monsters,ndivyo ilivyo CCM, zipo wapi hizo values,ethics n.k unazoongea wakati chama chenyewe kimeingia madarakani kwa fedha chafu? once human now vampires, mm tokea nizaliwe nchi hii masikini, wananchi wanaishi maisha mabovu ya ulimwengu wa tatu,huku viongozi na watawala wakiishi maisha ya ulimwengu wa kwanza,tokea CCM ilipoasisiwa mpaka leo...dhana ya kuondoa ujinga, maradhi na umasikini...tokea enzi hizo imekuwa kama hadithi ya "kuhamishwa makao makuu ya serikali kutoka Dar kwenda Dodoma",tokea siku hizo za wanaoitwa waasisi mpaka leo hatukuwa kuwa na wakati wa ahueni ya kimaisha (sijuwi ww mwenzangu) mpaka leo...utanambiaje habari za ethics,values,misingi ya waasisi...nk?
CCM is the same party since the day it was established to date.
Alama ya nyundo ndo ile ile ya kuwagonga vichwa watanzania masikini, na jembe ndo lile lile la kuwafukia wakikata roho.
wake up!
 
Sasa kasamehe kile kiinua tumbo chake cha 40/ Million, spika atamchukulia?
 
Mtu B usianze kuchekesha watu wewe unafikiri kura zilikuwa za nani za Juma Shamte wa CUF

Ni kura za CCM. Unless wewe unafikiri kuwa Mpendazoe ndio CCM yenyewe! Mimi nadhani Mpendazoe alikuwa mwanachama wa CCM, ameondoka CCM imebaki na wanachama wengine. Au wasemaje?
 
Kwanza nikupe pole kwa kuendelea kuamini kuwa CCM ndo ile ile (japo sikumbuki ilikuwa wapi nzuri) ya akina Nyerere na Karume (the worst one than this),ndugu yangu vampires wote asili yao ni watu,when it comes to sipping blood they turns to animals and monsters,ndivyo ilivyo CCM, zipo wapi hizo values,ethics n.k unazoongea wakati chama chenyewe kimeingia madarakani kwa fedha chafu? once human now vampires, mm tokea nizaliwe nchi hii masikini, wananchi wanaishi maisha mabovu ya ulimwengu wa tatu,huku viongozi na watawala wakiishi maisha ya ulimwengu wa kwanza,tokea CCM ilipoasisiwa mpaka leo...dhana ya kuondoa ujinga, maradhi na umasikini...tokea enzi hizo imekuwa kama hadithi ya "kuhamishwa makao makuu ya serikali kutoka Dar kwenda Dodoma",tokea siku hizo za wanaoitwa waasisi mpaka leo hatukuwa kuwa na wakati wa ahueni ya kimaisha (sijuwi ww mwenzangu) mpaka leo...utanambiaje habari za ethics,values,misingi ya waasisi...nk?
CCM is the same party since the day it was established to date.
Alama ya nyundo ndo ile ile ya kuwagonga vichwa watanzania masikini, na jembe ndo lile lile la kuwafukia wakikata roho.
wake up!

Aisee sio kuwa hawajui au wamesahau, mfumo wao wa kufikiri umeathriwa na vumbi chakavu la ujinga.Hakuna kiongozi mzuri keshawahi kutawala nchi hii kama tutakubaliana kutumia standard of living kuwa kigezo cha kupima uzuri wa viongozi kwani kama shida za maji,umeme,barabara n.k Zipo tangu 1961 mpaka hii 2010 sasa tunawapimaje viongozi wetu, Nyerere kaitoa nchi kutoka ya 26 kwenye line ya umaskini 1961 mpaka kwenye red line 3 bora za umaskini ,Mwinyi akatuopeleka kwenye top ten ya Rushwa, Mkapa top 3 ya kuibiwa kupitia truck ya Utandawazi, Kikwete ndo kabsaa, kahakikisha kwenye hizo top ten na 3 hatutoki ng'o Yeye kaja na single ya SERIKALI YA KISHKAJI, sasa huo uzuri wa CCM uliopotea uko wapi, CCM ikizikwa kama kipo cha kumiss kwanza kabisa ni hayo mawazo legevu na yasiyo na mashiko
 
...nani alikuambia kuwatumikia watu lazima uwe mbunge tu??? zipo kazi nyingine nzuri atafanya kwa dhamira safi bila unafiki!!

Hapa nakuelewa. Kama amechagua kuwatumikia wananchi kwa kurudi miongoni mwao kuendelea kunung'unika, sawa tu. Lakini hii naona utakuwa utumishi wa ngazi ya chini zaidi au wenye tija ndogo zaidi. Ni sawa na kumsomesha mwanao hadi university na anapata kazi nzuri inayoweza kuwasaidia wadogo zake nyumbani, halafu ghafla anaamua kurudi nyumbani kuchunga mbuzi na nduguze kwa madai kwamba hata hiyo pia ni kazi muhimu!

Hiyo hatua ya kuwatumikia watu kwa malalamiko ya mtaani alishaipita, alishapewa jukumu kubwa zaidi na wananchi wake, sasa amelitelekeza. Lakini bado ni mtu wao, labda watamzawadia japo uenyekiti wa CCJ wa wilaya akaendelee kulalamika tu kama anavyotaka mwenyewe. Chaguo lake of course.
 
Ni sawa na kumsomesha mwanao hadi university na anapata kazi nzuri inayoweza kuwasaidia wadogo zake nyumbani,

Yaani kazi ni kazi hata ukiamua kushirikiana na wezi au majambazi ! Eti mradi unamsaidia mzazi wako na wadogo zako - hii mbona kali. Hii yanikumbusha baba aliyeshtuka na kuzirai alipopewa taarifa kuwa mwanaye ameuawa akifanya ujambazi ! Kumbe mali zote alizokuwa akizipokea zilitokana na wizi !

halafu ghafla anaamua kurudi nyumbani kuchunga mbuzi na nduguze kwa madai kwamba hata hiyo pia ni kazi muhimu!
Siku akitubu na kutangaza anaacha ujambazi na unyang'anyi na kurudi nyumbani je ? Kumbe ufisadi nao ni kazi muhimu - duh ! Huyo mzazi au ndugu ambaye hatafurahi akipata taarifa ya mwanaye kuachana na ujambazi labda anapatikana CCM tu kwa sababu it is their way of life !

Hiyo hatua ya kuwatumikia watu kwa malalamiko ya mtaani alishaipita,

Na hiyo hatua ya kushiriki katika kuwaibia wananchi waliokuchagua kwa mapozi je ? Si heri ushirikiane nao mitaani kupambana na vibaka wa taifa na ikiwezekana kuwachoma moto na kuwatokomeza. Ndio, yeyote anayeendela kubaki CCM hana tofauti na vibaka wa mitaaani !

alishapewa jukumu kubwa zaidi na wananchi wake, sasa amelitelekeza. Lakini bado ni mtu wao,

Twaambiwa wanachama wa CCM taifa ni kama milioni 4 sawa na asilimia 10% ya watanzania wote. Alichaguliwa na wananchi lakini akawa analinda maslahi ya CCM. Hii ina maana alikwisha watelekeza asilimia 90% ya wananchi kitambo tu ! Sasa kama mwana mpotevu ameamua kurudi nyumbani, ubaya uko wapi ?
labda watamzawadia japo uenyekiti wa CCJ wa wilaya akaendelee kulalamika tu kama anavyotaka mwenyewe. Chaguo lake of course.
Chaguo lake ni kuungana na raia wema wa nchi hii kutetea na kulinda rasilimali za taifa. Kama hili la Mpendazoe limekutia hofu kiasi hiki basi subiri, machungu zaidi yanakuja na sina hakika kama utaweza kuyameza. Wanga wote huingiwa na hofu mwanga unapoanza kupenyeza, anza kutafuta pa kujisetiri ndugu yangu usijeumbuka !
 
wish him (Mpendazoe) all the best.

ila ajipange vyema maana janja yake ni kupata wapiga kura wa kutosha kumrudisha mjengoni
 
JAMANI NAPENDA KUJUA KWANZA BACKGROUND YA HUYU MPENDAZOE FRED, i MEAN ELIMU YAKE, WAPI ALIFANYA KAZI KATIKA TAASISI ZIPI KAFANYA KAZI AND THEN PRIVATE LIFE YAKE KWA WALE WANAOJUA TUPENI. TUSIBAKI KUSHABIKIA AU KUMLAUMU TU TUNA KILA SABABU YA KUFANYA RESEACH YA HUYU MTU NA BAADAYE TUJUE KUWA ANATUPELEKA WAPI. ISIJE IKAWA YA AKINA MREMA.!!!!
 
Binafsi, ninafikiri Mpendazoe amefanya jambo la maana ambalo ni vigumu kuufikia uamuzi wa namna hiyo kulingana na kwamba unapoteza mafao yako, na cheo chako kwa kukataa kushirikiana na watafunaji nchi.

Sidhani kama anakwenda kuwa nyuma kimaisha eti kwasababu kaacha ubunge, ni mtu ambaye ameshika nyadhifa mbali mbali na atakuwa amejipanga kimaisha, anyway hiyo si hoja hapa ya maisha yake ya mbeleni, hoja ni nguvu yake ataitumiaje katika chama hicho alichohamia. Tunataka afanye kazi kwa nguvu kama ilivyokuwa wakati wa Mrema alivyoihama CCM, alitikisa nchi na viongozi, sasa ndugu yetu sisi tunaamini kwamba huko alikohamia anaenda kuweka chachu na msukumo zaidi kwenye hicho chama na hasa kufichua zaidi upumbavu wa kifisadi unaonendelea. Na CCJ itabidi wampe ushirikiano wa karibu. Sitakuwa na shaka kuona wabunge wengine wanaendelea kuiama CCM.

Kuna fununu kwamba hata CCM wenyewe walikuwa kwenye harakati za kumtema, so ni bora amefanya hivyo na nina imani kama atagombea tena ubunge mwakani, kwenye jimbo lake kupitia CCJ, atashinda tu.
Naomba badala ya kumkandia, tumpeni nguvu ili tuendelee kuwakurupusha hawa mafisadi, ambao waketafuna pesa ya nchi bila kuogopa kwamba kuna kifo mbeleni.
 
Hapa nakuelewa. Kama amechagua kuwatumikia wananchi kwa kurudi miongoni mwao kuendelea kunung'unika, sawa tu. Lakini hii naona utakuwa utumishi wa ngazi ya chini zaidi au wenye tija ndogo zaidi. Ni sawa na kumsomesha mwanao hadi university na anapata kazi nzuri inayoweza kuwasaidia wadogo zake nyumbani, halafu ghafla anaamua kurudi nyumbani kuchunga mbuzi na nduguze kwa madai kwamba hata hiyo pia ni kazi muhimu!

Hiyo hatua ya kuwatumikia watu kwa malalamiko ya mtaani alishaipita, alishapewa jukumu kubwa zaidi na wananchi wake, sasa amelitelekeza. Lakini bado ni mtu wao, labda watamzawadia japo uenyekiti wa CCJ wa wilaya akaendelee kulalamika tu kama anavyotaka mwenyewe. Chaguo lake of course.

watetezi wa mafisadi ndani ya ccm naona kiroho kinawauma kweli .... mtakoma mwaka huu na shehe whu-sein wenu
 
JAMANI NAPENDA KUJUA KWANZA BACKGROUND YA HUYU MPENDAZOE FRED, i MEAN ELIMU YAKE, WAPI ALIFANYA KAZI KATIKA TAASISI ZIPI KAFANYA KAZI AND THEN PRIVATE LIFE YAKE KWA WALE WANAOJUA TUPENI. TUSIBAKI KUSHABIKIA AU KUMLAUMU TU TUNA KILA SABABU YA KUFANYA RESEACH YA HUYU MTU NA BAADAYE TUJUE KUWA ANATUPELEKA WAPI. ISIJE IKAWA YA AKINA MREMA.!!!!

Fred Mpendazoe alizaliwa mwaka 1957 na alipata elimu yake kati ya 1966 hadi 1972 katika Shule ya Msingi Bugoro.
Mwaka 1973 hadi 1976 alisoma kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule ya Sekondari ya Sengerema mkoani Mwanza.
Mwaka 1977 alisoma kidato cha tano na sita. Aidha, 1979 hadi 1983 alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutukiwa Shahada ya Uhandisi katika Kemia.
Baada ya masomo hayo, aliajiriwa na kiwanda cha Sukari mkoani Morogoro ambapo alifanya kazi kwa miaka minane, baadaye alikwenda kufanya kazi Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) na hapo alifanya kazi kwa muda wa miaka tisa.
Mpendazoe, pia alifanya kazi Wizara ya Maji kama Ofisa Mkuu wa Maji kwa miaka minane.
Baada ya hapo alikwenda Zambia kufanya kazi kama mkufunzi katika Chuo cha Evalin Hone na mwaka 1991 1992 alipata Shahada ya Uzamili nchini Uingereza.
Alishika nafasi ya Naibu Kamanda wa Vijana wa CCM wilaya ya Kishapu mwaka 2004 na mwaka 2005 aligombea ubunge na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya CCM hadi jana alipoachia nafasi hiyo na kujiunga na CCJ.
 
Back
Top Bottom