Mkirua
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 5,647
- 2,498
Note the spelling,
Le grand Maître
Le Tout puissant
Nami nawakubali mno.
Meaning??....
:focus: hakuna kama Francoo wala sioni dalili za kupata mwingine....
Note the spelling,
Le grand Maître
Le Tout puissant
Nami nawakubali mno.
Kwa hio ilikua ni uongo kwamba walikua na biffu kwa ajili ya Mwanamke? Hicho kipindi cha "La Aunthenticite" is one of the things ambacho naona Mobutu alifanya la msingi thou alienda a bit extreme with the names, walikua lao moja na Leopold Senghor wa Senegal katika falsafa ya preserving African ethnically authentic....
Mkuu wewe umeniona nini nna headset hapa nasikilita Tangawusi. Huyu jamaa mungu alimtunuku hasa, nikisikiliza nyimbo zake nakumbuka miaka ya mwanzo ya themanini nikiwa mdogo kaka zangu walikuwa wakizisikiliza sana hizi nyimbo na mzee wangu! na hata quality ya nyimbo zake ni za hali ya juu sana zilirekodiwa kwenye mitambo ya kisasa sana tena mnoo! hebu sikiliza Tokabola sentiment aliyoimba Josky kiambukuta!
Nakumbuka mwaka 1984 nikiwa songea tulikuwa na kanda yake, moja ya wimbo uliokuwepo ni mbanda ako ti kikumbi, saa yale matamshi ukisikiliza ni km anaimba matakoni kivumbi, basi si nikajirekodi kweli hiyo chorus eti matakoni kivumbi eeeeh mwanamama hahaha sister angu alikuwa anacheka hana mbavu.
Wimbo wa Mario part 1 unanikumbusha sana bustani ya nyanya aliyolima kaka yangu mwaka 1984-85. nilikuwa nikirudi toka shule wakati huo nipo std 4 basi nakuta bro kauweka, nikiingia ndani tu mdingi anaamka ananiambia badirisha yuniform nenda kamwagie nyanya, wakati huo mie sina mpango kabsaa wa kwenda bustanini, natorokea kiwanjani kupiga chandimu, nikirudi tuu saa moja moja ni bakora kwa kwenda mbele!
Hebu sikiliza Matata ya mwasi basi kwa leo halafu uniambie Franco amekukuna vipi
Sio SADA..ni SIDA..wimbo unaitwa ATTENTION NA SIDA..amboya ina nyimbo kama KINSHASA MBOKA YA MAKAMBO,LIKAMBO YA NGANGA,MARIO,Q'U EST LE SERIEUX.
thenksi kwa kuniweka sawa mkuu.
huo wa Kinshasa Mboka ya Makambo?
I know the song very well...
Nilishawahi kuona mahali Live Performance ya L'e TP Ochestra, hadi jukwaa lilikuwa limepigwa logo yao, na performer alikuwa Vercky Longomba, ambaye anaimba na kucheza.
CARLITO LASSA
Carlito - Kitiwala - YouTube
hizi nyimbo za franco huwa nazipenda sana..nikiwa nasafiri safari ndefu...tangu mwanzo wa safari hadi mwisho ni kusikiliza nyimbo hizi na nnjia nakuwa makini kwlei halafu sichoki..nashangaa nimefika .....mama yangu ndo chachu ya kuzipenda nyimbo hizi ..anajua kuziimba mwanzo mwisho na anaimudu vizuri lugha ...
AshaD,Franco alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mobutu japo walizinguana kipind kile cha 'LA Aunthenticite',,ambapo alitaka kila mwenye majina yenye asili ya kifara abidilshe haraka,ilipelekea wanamzikwengi wa congo kutimkia ufaransa ambo yeye franco alikubali kw shingo na akapewa jina la L'OKANGA LA NDJU PENE LUAMBO LUANZO MAKIADI.
Mamuu..ameimba na yule dada anitwa okamana.
Mkuu Bakulutu,
Nikufanyie masahihisho kidogo. Wimbo wa Mamuu umeimbwa na wanaume wote. Anayeongoza kwa kuimba ni Madilu System na mwisho anaingia Franco kuwa anapiga simu kwa mpenzi wake huko Majuu. Simu inapokelewa na Mwanamke ila ni yule jamaa Mpiga Bass ambaye anajifanya ana sauti ya KIKE.
AshaD, ni kweli Luambo walikosana wakati fulani na Mobutu ila walikuja wakapatana na Franco hadi akawa Waziri wa Muziki na utamaduni sijui? Pana wakati Mobutu akafanya uchaguzi eti wa Rais na Franco akamtungia wimbo kabisa wa kumpigia kampeni. Siku moja akiimba huko Ubelgiji kama sikosei, wakamtandika risasi ya mguu na Mobutu akapeleka dege kubwa la abiria kumbeba mtu mmoja tu, Franco.
Sijui kama kweli hiyo story ya risasi maana na mie nilikuwa mdogo sana kipindi hicho.
Bakalutu, ukianzia dakika ya 6:50, utamuona huyo jamaa anayejiita Mamou.
Wimbo wa Luambo akimsifu Moboutou ni huu hapa AshaDii. Huu wimbo ukiacha maneno, ni mzuri sana.
Jasusi. weke tytle basi ya wimbo tuutafute. Nina CD kadhaa za Franco ila sijui upi ni upi. Kuna wanamuziki kibao unakuja tu kusikia baadaye kuwa kumbe walikuwa kwenye kundi la TP OK Jazz.