Francis Kiwanga wa LHRC aieleza msimamo juu ya Kifo cha Osama

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Ndugu zangu JF,

Nimefuatilia mjadala wa Kauli yangu juu ya kifo cha Osama bin Laden katika jukwaa hili na hata nje yake na kugundua mambo kadhaa ambayo nastahili kuyaweka wazi yakaeleweka vema kwenu na wadau wengine. Moja kati ya vilivyojitokeza ni uimara wenu katika kudai, kuhamasisha na kuhimiza haki za binadamu pale mlipo na hata baada ya hapo; jingine ni namna mlivyo na matumaini makubwa juu ya kazi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, LHRC.

Nimejifunza toka mjadala huu kuwa mko makini kujua na kufuatilia HAKI za binadamu bila kujali tofauti eyote miongoni mwa binadamu na namna wengine wanavyoweza kuwahukumu. Naheshimu mawazo yenu kwani mmetimiza wajibu wenu wa Kikatiba. Kwa msingi wa mjadala huu pia nimependelea nitoe ufafanuzi wa maneno niliyonukuliwa na BBC juzi jioni (03 Mei 2011) na kusikika jana (04 Mei 2011) asubuhi ambayo ndiyo yaliyozua mjadala mkali hapa JF. Ukweli ni kuwa maneno yaliyonukuliwa hayakuwa yenye maana ya kujitosheleza:

(…kuuwawa kwa Osama kunaweza kuwa sawa kwa kuzingatia mazingira yake.)

Kichwani mwangu nilikuwa nawaza je, kwa kuzingatia mazingira ya suala hilo kulikuwa na nafasi ya kumkamata Osama/ au yeye mwenyewe kujitokeza katika vyombo vya sheria ili utawala wa sheria uchukue nafasi yake?

Maneno hayo yalitanguliwa na maneno:

“… ni vigumu kushangilia kifo cha mtu yeyote na msimamo wetu kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu … pia ni wajibu wa kila kulinda na kutetea haki za binadamu na kuifanya dunia ni mahali bora pa kuishi”

Katika mahajiano yale, niliweka wazi siungi mkono kwa namna eyote kuuwawa kwa binadamu yeyote, achilia mbali Osama bin Laden. Na labda nirudia kusema pia kuwa hatushangilii kifo cha Osama na pia hatuungi mkono ugaidi na matendo ya kigaidi ambayo lengo lake ni kuleta hofu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani,. Huu ndio uelewa wangu.
Nawasilisha.

Francis Kiwanga

Francis K. Kiwanga
Executive Director
Legal and Human Rights Centre-LHRC
P.O.Box 75254
Dar es salaam
email; fkiwanga@humanrights.or.tz
Phone; +255 22 2773038/48
Mobile;+255 787 229933

“My life is my message” M. Ghandi
 
siungi mkono kwa namna eyote kuuwawa kwa binadamu yeyote, achilia mbali Osama bin Laden.

“My life is my message” M. Ghandi

Huyu anajua anachotutaarifu kwa sentensi hiyo hapo au ndo Kiswahili kinamchanganya!
 
Hata kama ni mtuhumumiwa ila cha msingi angefikishwa mahakamani maana hakuna hata mmoja anaweza kuhukumu kwa kumuua na kuona kuwa ni sahihi mbele ya sheria za kimataifa
 
Huyu alikuwa kila kukicha anapanga njama za kuwadhuru Wamarekani. Simwonei huruma shenzi type. Wale Wamarekani elfu tatu aliowaripua kwenye twin towers hawana hata makaburi. He got what he deserved.
 
Some people, ur among of them, still in dreams, fantasy, imagination, etc, umeongea neno SHERIA mara kibaoo as if ww ndio sheria yenyewe, kumbe laa, openly with sharp words nasema you never witness ugaidi, au ww, familia yako, haijapata madhara ya ugaidi, ungeacha ndoto za abunuasi & fantasies u narrate here, stop, stop pretending ww ndio sheria, sheria imekuwa biashara kubwa na haki nyingi haipatikani thru sheria, tumeona, tumefikwa na matatizo mengi still sheria imegeuka biashara kuinunua ili haki ije kwa mwenye fedha, again stop dreaming, Osama declared publicly he is after 9/11 attacks, Nairobi & Dar US embassies, ww ongea bcoz ni haki yako but ujue ni pumba, na usjifanye uko na mawazo different na watu wengiiii ili ujitafutie cheap popularity even kwa upuuzi, mambo ya malipo ya wazee wetu wa EAC yamewashinda kuwatetea unaongelea Osama? Umekunywa leo nini? shame on u.
 
Francis Kiwanga is on point, kama kawaida yake. Kinachonishangaza zaidi ni viongozi wa nchi ya Tanzania na Kenya kuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu suala hili. Kwani wanahitaji kukumbushwa kwamba Osama na kikundi cha Al Qaeda wali-debut hapa hapa kwetu? Mashambulizi ya kwanza ya Osama yaliyotikisa amani yalifanyika kwenye balozi za Marekani mjini Narobi na Dsm, siku moja! kwa gharama ya damu na maisha ya wananchi wa nchi hizo. Kutokana na hilo nilifikiria viongozi wa nchi hizo wangekuwa wa kwanza kutoa msimamo juu ya tukio hili na kukumbushia kwamba hatujawasahu ndugu zetu walipoteza maisha.
 
Back
Top Bottom