Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mungu aliyenileta duniani na atakayenitoa hapa duniani,Ndungu zandu na wadau zangu wapendwa nitakuwa si mpiganaji wa kweli kama nitabaki na siri hii ya kukamatwa kwangu na jeshi la polisi na pia sitakuwa muungwana kama nisipowashukuru wote kwa dua zenu hadi nimeachiwa huru.
Ninaomba kwa sehemu niweze kuelezea yaliyonikuta hadi nikakamatwa na polisi ilikuwa ni jumanne ya Mei 31 majira ya saa 7.45 eneo la shule ya sekondari Tosamaganga wakati nikitoka kufuatilia sakata la mgomo wa wanafunzi ndipo nilipokamatwa na askari wa upelelezi watatu . Dalili za kuwepo kukamatwa zilianza kujionyesha toka jumatatu ya mei 30 eneo la Mseke wakati nikiwa na mwenzangu wa Radio Ebony Fm ambapo mkuu wa polisi wilaya ya Iringa alitupiga stop kuendelea kufuatilia sakata la FFU kuwapiga mabomu wa wanafunzi wa sekondari ya Tosamaganga bila kuwa na kibali cha polisi . kutokana na kiongozi huyo wa polisi wilaya kututaka kuomba kuifanya kazi hiyo tulilazimika kuondoka na kwenda kuripoti tukio la wanafunzi hao kugoma katika vyombo vya habari ukiwemo mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima.
" Kabla ya kuondoka eneo la tukio kijiji cha Mseke mpakani mwa Iringa vijijini na mjini ambako wanafunzi hao zaidi ya 1000 walitawanywa na FFU kwa mabomu tulipata kumuuliza mkuu huyo wa Polisi aina ya vibali ambavyo vinatolewa na jeshi la polisi kwa waandishi wa habari wanapotakiwa kufuatilia tukio " Hata hivyo siku ya pili ambayo ni jumanne Mai 31 majira ya saa 7.45 nikiwa katika shule ya sekondari Tosamaganga kufuatilia hali ya mgomo huo ghafla alizingirwa na polisi wa upelelezi ambao waliziba barabara na kunishusha katika gari kwa nguvu huku wenzangu wawili akiwemo wa Radio Ebony na ITV wakiachwa .
"Pamoja na madai hayo nilishangazwa hatua ya askari mmoja ambaye anaitwa Mrisho kwa kuanza kunitukana matusi ya nguoni na kudai kuwa mimi nimejifanya mjuaji na kupitia gazeti la Tanzania Daima na blogu ya Francis Godwin nimeonyesha tukio la wao kuwapiga mabomu wanafunzi hao na tukio jingine alilonihusisha ni lile la madai ya polisi kudaiwa kumpiga kwa risasi mwanamke mmoja mkazi wa Don Bosco " Pamoja na askari huyo Mrisho kutishia kuwa angempiga sana ila hakuweza kufanya hivyo baada ya kuwasiliana na wakuu wake ambao wamemtaka asinipige wala kunitesa kwa namna yeyote ile.
Baada ya kukamatwa nikiwa eneo la shule hiyo alipelekwa kituo kidogo cha polisi Tosamaganga na baadae kupakizwa katika gari iliyokuwa na askari wa FFU zaidi ya 10 huku wakipiga king'ora mfano njia nzima na kumfikisha kituo cha polisi mfano wa jambazi sugu amekamatwa na baada ya kufika mkuu wao aliagiza niwekwa mahabusu bila maelezo kwa zaidi ya masaa mawili.
Majira ya saa 12.49 ndipo mwandishi wa habari za Chanel Ten mkoa wa Iringa Daud Mwangosi na mwandishi wa gazeti la Majira mkoa wa Iringa Eliasa Ally walifika kituoni hapo kwa ajili ya kuniwekea dhamana na ndipo nilipotoa maelezo yangu kuelezea mazingira ya kukamatwa japo katika maelezo hayo sehemu ya kosa haikujazwa chochote zaidi ya askari aliyokuwa akichukua maelezo kudai kuwa kosa ni kuwaonyesha wanafunzi hao zaidi ya 1000 askari wawili wa upelelezi na dhamana ya shilingi milioni 1 ipo wazi.
"Nikiwa ndani ya gari ya FFU baadhi ya askari walikuwa wakinihoji ili kujua kama ni mfuasi wa Chadema na kuwa wao walielezwa kuwa nimetumwa na Chadema katika shule hiyo huku wengine wakitoa vitisho kuwa yaliyompata Jerry Muro na Said Kubenea ndio wanayotaka kunifanyia mimi"
Maelezo ya polisi na yale ya kamanda wa polisi mkoa kwa vyombo vya habari yalionyesha kutofautiana baada ya polisi kudaiwa kuwaonyesha wanafunzi askari wa upelelezi na kuhatarisha maisha yao huku kamanda wa polisi akidai kuwa sababu ya kushikiliwa na polisi ni kuchochea mgomo wa wanafunzi.
"Hata nawashukuru wanahabari ndani ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kwa kulishughulikia suala hilo kwa uzito wake pamoja ....pia namshukuru mkuu wa polisi wilaya (OCD) Semunyu kwa kuniachia huru na kunitaka kuendelea na kazi yangu kwa amani"