Former TIC Executive Director, Emanuel Ole Naiko

Wakuu,
I have totally failed to understand how can a public servant of his level end up being a Board Chairman of a private company. Is it that he was favouring them (Barick Gold) that is why they decided to thank him with Board Chairmanship?

Hii ndio Tanzania...Kila kiongozi anao mtaji wake anauandaa awapo madarakani, na mahala pa kupumzikia pale anapotoka madarakani...! Nani hawajui Barrick walivyo corrupt...?? Then Naiko ndio Chairman, its simply kuwa anaendakula walichomwandalia toka alipowapokea na kuwalinda alipokuwa TIC kwa niaba ya 'mkuu wake'..na anaenda kumlindia 'mkuu' share yake na kuhakikisha atakapotoka madarakani 'hesabu' lao lipo sahihi...! Huu ndio uchafu ambao CDM itakuwa na kazi nzito ya kuusafisha bila kupumzika, hadi taifa liwe 'clean'...! Itakuwa hakuna kulala!
 
taifa linapotea.haya mambo yawepo kwny katiba mpya.baada ya kustaafu,mtumishi wa umma awe ktk shughuli gani
 
Tanzania kila kitu kinawezakana. Kuna wakati, spika wa bunge aliwahi kuwa board chairman wa kampuni fulani...itakuwa huyo mstaafu? Watu walivyojaribu kuuliza kulikoni wakaambiwa ati wana "wivu wa kike"!

Under CCM everything is possible only in Tanzania!!!

Tunajua kuna vigogo wengi wa CCM wana shares(hisa) kwenye makampuni ya kigeni a.k.a Wawekezaji. Hizo shares huwa aidha wanapewa bure au wanalipiwa na Makampuni husika. Pius Msekwa ni mmojawapo ya wanufaikaji wa Makampuni ya Mawasiliano-Vodacom ambako naye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi wakti akiwa Supuka wa Bunge. Bwana Ole Naiko alikuwa Mkurugenzi wa TIC wanayoiiita mlango wa Wawekezaji Tanzania. Kwa hiyo Makampuni mengi yaliyoingia Tanzania uwekeza kwenye Mawasiliano na Uchimbaji wa Madini waliwezeshwa na Bwana Emmanuel Ole Naiko.

Kwa hiyo ,kinachoonekana hapa ni FADHILA kwa Bwana Ole Naiko. Mind you hii ni nje ya VILE VIJISENTI VILIVYOKO KULE UGHAIBUNI almaarufu kama OFFSHORE ACCOUNTS!

Watanzania kazi mbona tunayo!!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kwa hiyo unamaanisha Symbion walimhonga hadi Mwanakijiji

Wakina Mwanakijiji waliumbuka kwakuwa wao walaikuwa wanakaomaa kwamba mitambo ile ni ya mitumba serikali isinunue. Sasa wakaja wamarekani na akili timamu wakanunua hiyo hiyo mitambo ambayo sisi tunaita ya mitumba na bado tunauziwa umeme bei juu. Imagine kama tungenunua?
 
Nyerere alijaribu kumgusa mtu anaitwa Tiny Rowlands alikuwa mmiliki wa shirika likiitwa LONRHO. Ulimshinda huo mfupa.

Usicheze na haya mashirika makubwa yanayochangia kwa kiasi kikubwa bajeti za nchi zao, utaumia, ukipenda usipende.

Uliona Symbion ilvyochukuwa mitambo ya Dowans alikuja nani kuitembelea hiyo mitambo? jiulize, ilihusu nini? halafu jiulize tena Mzee Mwanakijiji alikuwa mstari wa mbele kuiponda Dowans, ulimsikia akinyanyua sauti kwa Symbion? na mitambo ndio hiyo hiyo, jiulize kwanini? Hata upinzani hawakuitaja tena.

Cheza na mwenye mali usicheze na mali zake.

kaka upo juu,
hebu tujuze zaidi kwa kututajia ni kina nani hasa,si unajua mambo ya ku-guess sio mazuri
 
Acheni wivu wa kijinga. Huyu jamaa kastaafu serikalini sasa katafuta ajira binafsi ingekua wewe sawa lakini mwenzako inakuuma. Kwanza hujasoma pili hata ukiitwa kwenye usaili atakupita tu. Tujadili mambo ya maendeleo
 
Under CCM everything is possible only in Tanzania!!!

Tunajua kuna vigogo wengi wa CCM wana shares(hisa) kwenye makampuni ya kigeni a.k.a Wawekezaji. Hizo shares huwa aidha wanapewa bure au wanalipiwa na Makampuni husika. Pius Msekwa ni mmojawapo ya wanufaikaji wa Makampuni ya Mawasiliano-Vodacom ambako naye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi wakti akiwa Supuka wa Bunge. Bwana Ole Naiko alikuwa Mkurugenzi wa TIC wanayoiiita mlango wa Wawekezaji Tanzania. Kwa hiyo Makampuni mengi yaliyoingia Tanzania uwekeza kwenye Mawasiliano na Uchimbaji wa Madini waliwezeshwa na Bwana Emmanuel Ole Naiko.

Kwa hiyo ,kinachoonekana hapa ni FADHILA kwa Bwana Ole Naiko. Mind you hii ni nje ya VILE VIJISENTI VILIVYOKO KULE UGHAIBUNI almaarufu kama OFFSHORE ACCOUNTS!

Watanzania kazi mbona tunayo!!!

Iwe wa CCM isiwe wa CCM, "It's Not What You Know, It's Who You Know".

Usifikiri kuwa hakuna watu wa chadema wenye hisa au manufaa fulani kwa hizo kampuni au mashirika yasio ya kiserikali au taasisi za kigeni zenye manufa kwa pande zote.

Njia moja ya kuuwa ukiritimba au "bureaucracy" (kitu ambacho ni hatari kwa biashara yoyote ile) iwe ni Tanzania au kokote kule, ni nani umjuwae na si nini unachokijuwa ndio kinakusaidia kuuwa huo ukiritimba. Leo hata Tanzania kama una unaemjuwa idara fulani au taasisi fulani au wizara fulani au kampuni fulani, una uhakika wa mambo yako kwenda haraka kuliko ukiwa humjui mtu.

System at work.
 
Wakuu,
I have totally failed to understand how can a public servant of his level end up being a Board Chairman of a private company. Is it that he was favouring them (Barick Gold) that is why they decided to thank him with Board Chairmanship?

Akasante kwa kazi nzuri uliyotufanyia kaa hapa sasa nawe ule.....
 
ollee.jpg

Former Prime Minister Edward Lowassa (second right) and African Barrick Gold (ABG) Director of Government Relations, Mr Emmanuel Ole Naiko (third right), cut a ribbon to officially inaugurate a project to buy desks for Minazi Mirefu Primary School in Dar es Salaam on Tuesday. The company donated 10,000 US dollars (about 16m/-) to procure 150 desks. Looking on are Ukonga Constituency Member of Parliament, Dr Makongoro Mahanga (right), ABG’s Corporate Community Relations Manager, Steven
Kisakye (second left) and ABG Public Relations and Communications Manager Nector Foya (left).
Source: Daily News

My concern;
Mkurugenzi Mstaafu wa TIC ni Director of Government relations!!! hii imekaaje? Hawa akina African Barrick si walipewa vibali vya uwekezaji hapa nchini na yeye? Huyu alikuwa mtumishi wa serikali mwenye dhamana ya kuwaruhusu akina Barrick wawekeze Nchini halafu sasa wanakuwa waajili wake yeye akihusika na mambo ya mahusiano na serikali!!

Sina nia ya kumu - offend lakini hii imekaaje before the eyes of justice?
 
Juzi nimetoka kuchukua msamaa wangu wa kodi. Very simple ni kutimiza masharti tuu...tutumie fursa tuache kulalamika. By the way bunge letu tukufu ndio limeweka sheria hiyo. Tic ni watekelezaji.
 
Huenda baada ya kustaafu ameomba kazi huko, na kwa kuwa wakati wanaingia nchini kuwekeza walipiatia ofisini kwake ilikuwa rahisi yeye kuajiriwa. Lakini tatizo ninaloliona hapa ni hili la mtu kustaafu kazi na kuomba kazi tena, kwa nini asipumzike ?
 
Acheni wivu wa kijinga. Huyu jamaa kastaafu serikalini sasa katafuta ajira binafsi ingekua wewe sawa lakini mwenzako inakuuma. Kwanza hujasoma pili hata ukiitwa kwenye usaili atakupita tu. Tujadili mambo ya maendeleo

Poor thinking, you seem to be those who read ijumaa, kiu and the likes. Please think critically and wisely
 
Wakuu,
I have totally failed to understand how can a public servant of his level end up being a Board Chairman of a private company. Is it that he was favouring them (Barick Gold) that is why they decided to thank him with Board Chairmanship?

Naiko ni msani kama wasanii wengine sasa hivi ni consultant kazi zake ni investment facilitator kustaafu kwake kulishamirishwa na bifu lake na Nagu.alijifanya mjanja akawa anasideline na EL kummaliza Nagu Ghafla nagu akapewa wizara ya uwezeshaji na uwekezaji ilipofika Naiko kurenew mkataba wake akachinjiwa baharini.Hicho unachokiona sasa ni Fadhila kwa kazi aliyowafanyia wawekezaji utasikia atakuwa kwenye bodi kibao wait n se.ni Mwenyekiti pia wa BOA Bank.
Huyu jamaa alikuwa siyo chaguo la Jk alikuwa mchemfu sana kuna wakati alichemka Presentation iliyokuwa inatakiwa kusomwa Canada yeye akaisoma Sweden..akakata slide kama 16 kuja kushtuka yupo chaka
 
Nimemuona leo kwenye Luninga,ni mwenyekiti wa bodi ya Africa Barick Gold mines.

Hisa hizo zimeuzwa lini na amenunua kiasi gani mpaka kuwa mwenyekiti?

Msekwa nae aliwahi kuwa wa Vodacom tukauliza na hatukupata majibu sasa aliyekuwa mkuu wa kittuo cha uwekezaji baada tu ya kustaafu tayari yuko kwa wawekezaji, napata mashaka.

Kama ni picha za michuzi hajasema mkiti bali mkuu wa mahusiano kati ya abg na serikali.
Pili mkiti huwa hana hisa ktk kampuni unless ni private ltd co kama ya mengi na kina bakhresa
 
Back
Top Bottom