Form six na wengine : Uliza chochote kuhusu Muslim University of Morogoro

Mpenda kazi

Senior Member
Dec 13, 2013
170
79
Habari wadau wa JF

Nimefungua uzi huu kwa yoyote mwenye kutaka kujua zaid kuhusu chuo hicho, location, kozi wanazotoa, taratibu za application na mambo mengine ya msingi unayotaka kujifunza kutoka chuo hiki.

ANGALIZO : Kama unataka tujadili kitu hapa basi tafadhali si vizuri kuleta maswala ya UDINI katika uzi huu. Ila cha msingi jenga hoja vizuri na utajibiwa hapa bila ya shaka. Weka wasiwasi wako juu ya chuo hiki hapa na inshallah nitakuelewesha tu na utaelewa bila ya jazba.
 
Ok mkuu Mpenda kazi
1. Eti naskia MUM wanafunzi wanalazimishwa kufunga ktk kipindi cha mfungo wa Ramadhani hata kama ni wa dini tofauti huzuuliwa kutokula kitu maeneo ya chuo?

2.Pia vipi kuhusu hostel zinapatikana karibu na chuo?

3. Vipi kuhusu somo la dini ni lazima kila mwanafunzi alisome na afaulu vizuri na endapo atafeli itamlazimu adisco chuo hata kama masomo mengine kafaulu vizuri.

4.Lastly; Kwanini kwenye vitabu vya TCU hiki chuo hakipo mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Ok mkuu Mpenda kazi
1. Eti naskia MUM wanafunzi wanalazimishwa kufunga ktk kipindi cha mfungo wa Ramadhani hata kama ni wa dini tofauti huzuuliwa kutokula kitu maeneo ya chuo?

mi nadhani jina la chuo linasadifu yaliyomo ndani.. sasa nyie akina CHARLES na JOSEPH mmefuata nini huko?

Chuo cha kiislamu morogoro, that means kinaendeshwa kiislam! na inawezekana kimesajiliwa ili kiendeshwe hivyo mkuu!

Wakristo walioenda huko watakiona cha moto...
 
1 - Wanachuo hawalazimishwi kufunga mkuu. Sio tu wa dini nyingine hata wanafunzi wa kiislamu pia hawalazimishwi kufunga. Kwanza unatakiwa uelewe kwamba kufunga ni lazima kwa waislamu tu na hairuhusiwi kwa mtu asiyekuwa muislamu kufunga. Lakini hata kwa hao waislamu pia kutokana na taratibu za nchi hawalazimishwi kufunga.

2 -Hostel zinapatikana sana tena za kutosha nje ya chuo na wala sio mbali na chuo kilipo.

3 - Ni kweli kabisa kwamba masomo kama; a) Introductiona to islam b) Hadith studies and c) Islamic history
Yote hayo ni lazima kuyasoma.Na nikuondoe wasiwasi kwamba hayo masomo ni marahisi sana kwani hata ufundishwaji wake ni kwa kutumia lugha ya Kiingereza. Lakini hata watu wa dini nyingine wanayasoma na wapo wanaofaulu kuwashinda hata hao waislamu.

4. Chuo kimesajiliwa na TCU hata ukiingia website ya TCU utakikuta ila udahili unafanyika moja kwa moja chuo kwa njia ya form kwahiyo hujakiona kwenye kile kitabu cha TCU kwasababu hakipo kwenye Cenral Admission System (CAS).
 
Last edited by a moderator:
mi nadhani jina la chuo linasadifu yaliyomo ndani.. sasa nyie akina CHARLES na JOSEPH mmefuata nini huko?

Chuo cha kiislamu morogoro, that means kinaendeshwa kiislam! na inawezekana kimesajiliwa ili kiendeshwe hivyo mkuu!

Wakristo walioenda huko watakiona cha moto...

Kuna tofauti kati ya ISLAMIC INSTITUTION na MUSLIM INSTITUION. Chuo hakiitwi CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHA MOROGORO ila chuo kinaitwa CHUO KIKUU CHA WAILSAMU CHA MOROGORO.

Ukisikia chuo cha kiislamu basi jua hapo hata kozi zinazotolewa zinahusika moja kwa moja na uislamu. Na si rahisi kwa mtu asiyekuwa muislamu kumkuta akisoma katika chuo cha kiislamu.

Lakini ukisikia chuo cha waislamu basi jua kabisa kwamba kozi zinazotolewa hapo ni mchanganyiko yani kozi ambazo hata mtu asiyekuwa muislamu anaweza kuzisoma.

Sasa chuo kina kozi ambazo hata wasiokuwa waislamu wanaweza kuzisoma.
 
ufafanuzi mzuri...
endelea kusubiri maswali mengine. Kila la kheri
 
1/Kwanini kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan hairuhusiwi chakula kuuzwa chuoni? 2/Kwanini ni lazima kila mwanafunzi asome na kufaulu kwanza masomo ya dini ya kiislam? 3/Kwanini watumishi wote wa hapo chuoni ni lazima wawe waislam? 4/Kwanini dini ndio kipaumbile cha kwanza cha chuo na sio taaluma?
 
Kuna fununu hapo Morogoro kwamba mabinti wanaosoma hapo wanajiuza hapo maeneo ya morogoro hasa Msamvu, oilcom, nane nane nk, hata wageni wakija hapo moro hasa wale wanaokuja kwa semina wanawafaudu sana maana kuna cordinator ambaye hurahisisha kazi ya kuwapata hao mabinti. Je chuo kinayajua hayo, na kama kinayajua kimechukukua hatua gani mpaka sasa ili kuepusha taswira ya chuo kuendelea kuchafuka hasa ikizingatiwa kinamilikiwa na taasisi ya dini kubwa Tanzania na duniani kwa ujumla. Na kama chuo hakijui, je kipo tayari kufuatilia hizo fununu zilizopo viunga vya Morogoro na sasa zinasambaa Tanzania nzima?
 
Je, hiko chuo kipo chini ya Bakwata?
kama sio hio taasisi inaelewana kimsimamo na bakwata?
 
1/Kwanini kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan hairuhusiwi chakula kuuzwa chuoni? 2/Kwanini ni lazima kila mwanafunzi asome na kufaulu kwanza masomo ya dini ya kiislam? 3/Kwanini watumishi wote wa hapo chuoni ni lazima wawe waislam? 4/Kwanini dini ndio kipaumbile cha kwanza cha chuo na sio taaluma?

1.chuo kinaendeshwa kwa taratibu n'a lakini sa kiislam n'a ndio maana mchana chakula hakiuzwi ila HAKATAZWI mtu kula mchana kwa sababu Hata waislamu wenyewe wapo wenye dharura ambao wana ruhusa ya kutokufunga mf wagonjwa,wanaonyonyesha nk

2. Ni lazima kwa wanafunzi wafaulu masomo ya Dini kwa sababu chuo kinalenga kutoa wahitimu ambao wana maadili mazuri ambayo yanapatikana kupitia mafunzo ya Dini ya kiislam,ni km vile TCU walivyoweka mkazo ktk courses km comm skills,ICT nk Iko kupata wahitimu ambao wana uweledi wa mambo hayo

3. Si lazima kwa wafanyakazi wote Kuwa waislamu WaPo ambao si waislam mfano Kuna lecturer mmoja kutoka Cuba ambae ni mwanamke ni mkristo,Kuna mwalim Chitra si muislam lakini pia WaPo part time lecturers ambao si waislam

4. Kipaumbele ni Dini kwa Kuwa Dini ni mfumo kamili wa maisha ambapo Ili mwanadamu aweze kuifanya vizuri Dini yake anahitaji elimu,Kwahiyo ndio maana kipaumbele ni Dini
 
Naomba kuuliza vp wale waliomaliza diploma ualimu mwisho point ngapi kujiunga hapo chuoni, maana nina mdogo wangu kamaliza mwaka jana
 
Kuna fununu hapo Morogoro kwamba mabinti wanaosoma hapo wanajiuza hapo maeneo ya morogoro hasa Msamvu, oilcom, nane nane nk, hata wageni wakija hapo moro hasa wale wanaokuja kwa semina wanawafaudu sana maana kuna cordinator ambaye hurahisisha kazi ya kuwapata hao mabinti. Je chuo kinayajua hayo, na kama kinayajua kimechukukua hatua gani mpaka sasa ili kuepusha taswira ya chuo kuendelea kuchafuka hasa ikizingatiwa kinamilikiwa na taasisi ya dini kubwa Tanzania na duniani kwa ujumla. Na kama chuo hakijui, je kipo tayari kufuatilia hizo fununu zilizopo viunga vya Morogoro na sasa zinasambaa Tanzania nzima?

Kwakweli chuo hakina taarifa ya kujiuza kwa wanafunzi katika maeneo hayo. Kila mwanacchuo ni mlinzi wa maadili ya mwanachuo mwenzie na chuo kina inteligensia kali sana kama ikigundulika kuhusu dai hilo basi mwanachuo/wanachuo wanaohusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.
 
Back
Top Bottom