Forbes wadai Mkuu wa Kaya ame-boost uchumi

Kiukweli uchumi wa Tanzania kwa kuzingatia kipimo cha GDP umekuwa ukikua kwa asilimia 7 kwa takribani miaka 10 sasa. Hivyo, hili siyo jambo jipya.

Tatizo linakuja ni pale tunapoangalia chanzo cha uchumi huo kukua. Chanzo kikuu ni service sector (utalii na huduma za ICT). Hapa ndipo penye tatizo. Kwani watanzania wengi wanategemea sekta ya kilimo. Sekta hii ndiyo inaajiri watanzania wengi directly na indirectly. Kwa kuwa haichangii kwa kiwango cha kuridhisha kwenye pato la taifa, ndiyo maana tuna uchumi unaokua kwa kiwango kikubwa duniani, lakini umaskini uliotopea bado unatusumbua.

Well, kuwa na uchumi unaokuzwa na service sector siyo mbaya. Kwa Tanzania, na haswa chini ya tawala za CCM, tatizo la ufisadi na matumizi yasiyo ya lazima ya kifedha kumepelekea hata fedha zinazopatikana kutoka kwenye service sector zishindwe ku-trickle down kwenye sekta zingine. Nchi ya Botswana imefika hapo ilipo kutokana na sekta ya madini tu! Norway sekta ya uvuvi tu iliwatoa; baadaye oil & gas ikawapelekea mbele zaidi.

Tatizo jingine la tawala za CCM, na hata hii ya sasa inayo 'uzwa' kama yenye mafanikio makubwa, sijaona mpango ambao serikali inao katika kuinua sekta ya kilimo. Serikali bado imeendelea kushindwa kutenga 10% ya bajeti yake kwa kilimo, kama makubaliano ya Maputo yanavyoelekeza. Serikali inapenda kusikia uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kiwango kikubwa duniani, lakini haipendi kujiuliza ni kwanini kwa miaka hiyo 10, bado umaskini ni mkubwa. Naamini wachumi washauri wa serikali wanafahamu hili; kwani hata mimi layman ninalifahamu. Sasa pengine wameamua kuendelea kukaa kimya na kumwacha Magufuli afanye anavyojisikia.

Kazi tunayo...
 
Salary slip angalia hii website
(Contributors: Sid Wahi - CNBC Africa)

Kuna hawa watu CMA Investment Holdings kumbe ndio wenye CBN Africa yote, Forbes Afrika (ambayo ni franchise ya Forbes), hiyo ABN group etc... na inavyoelekea wote hao wako kwenye jengo/adress moja (88 stella street, sandton, ZA). Kwa maana hiyo hizi awards/tuzo ni zao.

Kuna huyu kijana Sid, yeye ndie managing director wa CMA Holdings (ni biashara ya familia). Ananikumbusha watu wetu flani hivi wa huku, very business driven...
Well, mwaka jana mshindi wao wa hizi tuzo alikuwa Mtanzania ambaye ni M Dewji, CEO wa MTL group... alafu (kama ni kweli), mwaka huu tena mshindi atokee Tanzania, aisee, wanatupenda sana.
Kwa jinsi CMA Holdings wanavyotupenda labda tutawaona soon wakija ku-investment na hapa kwetu, au labda pengine wapo tayari...

Anyway, Ingekuwa vizuri kama wakina Sid wangetueleza wametumia criteria gani, vipi waliongea na watu huku mitaani kwetu au labda walifanya research kwa references za bot na world bank...
Alafu najiuliza hawa people of Rwanda kwani wako wangapi... Yani people wote hao of Rwanda wameshindwa kujipigia kura ili meter yao nayo ipande kwa kasi?
 
Mkuu,nimedharau sana hizi tuzo pamoja na waandaji wao.Ni ovyo kabisa!Hawa ni wakurupukaji tu.
 
Mbona wewe kila siku unaandika ameshusha Uchumi na sisi hatukujadili.. Kila mtu anaandika kwa mtazamo wake
 
1. Mbona wengine wanasema hii kitu imetengenezwa Lumumba tu?

2. Suppose kuwa hii kitu iwe ya kweli, inawezekanaje mtu maarufu ktk mwaka 2016 apimwe kwa kuchanganywa na nchi?

3. Ni kina nani wanaopiga kura za kumtambua huyo mtu maarufu? Na maarufu ktk nini...yaani kwa kuzingatia vigezo gani hasa? wizi? ukali? vituko? Uvaazi? woga?kuminya demokrasia?.........au .... au nini hasa??
 
Back
Top Bottom