For your EYES ONLY: From Salva to Rostam

Haya ndio mambo niliyokuwa yanayapendea JF

siku hizi tumeishia kutukanana kwenye Mengi vs all na hatufiki kokote kule

Kila kukicha tunachambua articles za magazeti zilizopostiwa na Bubu Ataka kusema

In short tumekuwa hatuna jipya

Kwa hili namshukuru sana KA-NZI na ingependeza haka kanzi kangekuwa kanatua yua kila baada ya siku mbili tatu hivi ili tupate mpya

Invisible naona WATERMARK uliyoweka ni ndogo sana hebu liondoe hili file weka watermark kisha hao magazeti ya kuja kukocopy na kupaste from JF tuone kama wataweza...huwa wananiudho sana wao kuja humu ku copy copy mambo bila ku acknowledge JF

Hivi wewe unafikiri hizo nyaraka wanaenda sehemu wanajaza form ya Freedom of Information Act wanapewa kama haki yao kama nchi za watu?

Wewe mbona hujaleta hizo nyaraka, uko hapo unalaumu badala ya kushukuru? Tena wenzako wanachukua risk kibao kwa uzalendo wao kutafuta hizo nyaraka na ni watu wanajulikana kwa majina yao. Wewe "Game Theory" nani anajua ni binadamu kutoka dunia gani? Watu wengine bana.
 
Duu? Nilipo kuwa mdogo nachumbia kigoli wangu, alinitolea nje akawa anawambia rafiki zake hanipendi kabisa. Nilipo kuwa katika hali ya kukata tamaa rafiki yangu akanitia moyo kwamba ukiona anaweweseka kwenda kusema kwa rafikize kwamba hakupendi, ujue huyo anakupenda sana ( na hakika ndiye honey wangu).

Akanambia wanadamu tuna silka ya kusema kinyume cha jambo tunalo lipenda ama kutamani liwe..

Kwa barua hii ya Salva, na maneno ya JK kwamba hana ubia kwenye uraisi wake, yana nikumbusha kisa hiki, Kumbe JK alikuwa anajua ana ubia kwenye uraisi wake ndo maana alikuja kwetu kuji shaua kwamba hana ubia na mtu!
 
Sasa nyinyi mmewahi kuleta nyeti gani tuchambue kama hamtaki mabandiko ya Bubu Ataka Kusema?

Leteni basi manyaraka ya siri na nyinyi tuyachambue ili tuachane na magazeti ya Bubu Ataka Kusema.

M-bongo anaweza akalaumu tu kitu wakati na yeye anafanya kile kile. Duuu
 
Je Mheshimiwa Raisi ataona hili ni kubwa la kutosha kutengua uteuzi wa Salva?
Je Salva ataona umuhimu wa kuandika barua ya kuomba apumzike ili kulinda heshima ya ofisi ya Raisi?

Labda jibu HAPANA linakuja haraka kwa wengi wetu. Lakini hii barua ukiingalia kwa makini utakubaliana na mimi majibu sahihi hapo juu ni NDIO. Je watanzania tumekufa kimaadili kiasi cha kutoweza kufuatilia hili litendeke? Natumaini waheshimiwa wabunge humu watafanyia kazi. Kama sijakosea ushahidi huu unaweza kuilazimisha ofisi ya DPP kufanyia uchunguzi ajira zote ofisi ya Raisi, ikiwa itafuatiliwa kisheria.
 
Hivi ni kwa nini Nyerere alikataa JK kuukwaa Urais wa hii nchi 1995?

Inakuwaje mpaka sasa hamjatambua kuwa Rostam ndiye Rais wa Chama kilichoshika hatamu Za Serikali akisaidiwa na Mwenyekiti wa Chama?

Imekaaje mkashindwa kuelewa kuwa lolote analotaka Rostam ndilo linalofanyika ndani ya Chama na sirikalini?
 
Kwenye hilo 'bolded' umelenga haswa. Asante

Nonsense. There is nothing wrong with posting news articles. If you already have access to these articles or if you are too stupid or lazy to read them then don't nobody is forcing you.

Some of us don't always have access to these articles.

Thank you Bubu, please ignore the ignorance of some of these people and continue to keep people informed and stimulate debate.
 
Kila kukicha tunachambua articles za magazeti zilizopostiwa na Bubu Ataka kusema

Nobody is forcing you to read them.

I and i am sure many other people on this board appreciate Bubu Ataka kusema's contributions. Which is more than i can say for you.
 
Nonsense. There is nothing wrong with posting news articles. If you already have access to these articles or if you are too stupid or lazy to read them then don't nobody is forcing you.

Some of us don't always have access to these articles.

Thank you Bubu, please ignore the ignorance of some of these people and continue to keep people informed and stimulate debate.

Je lugha ya kashfa na matusi ndio inaonyesha kwamba umwelewa na/au mwerevu zaidi?
 
HII NDIYO HESHIMA KWA JF.

HONGERENI SANA KWA KAZI NZURI MNAYOIFANYA HUKO NYUMBANI.

KWA KUWA SI WATANZANIA WENGI WANATUMIA KOMPYUTA NASHAURI HIYO DOKUMENTS WAPENYEZEWE NA WAANDISHI KAMA VILE TANZANIA DAIMA (MHARIRI MKUU, NI MPIGANAJI) NA GAZETI LA MWANAHALISI.

Hii itasaidia wengi kujua yaliyojificha.
 
Kazi nzuri sana Inzi. Kwa ufupi, hizi paragraph tatu zinaelezea vema yote juu ya nia ya Salva kumuandikia hii barua Rostam.

Salva Rweyemamu said:
Even if you found the idea of helping us become independent unattractive and costly, you could at least have looked for a way to accommodate us in some positions within the new Government whose struggle to get into power we so painfully supported and for so long.

Salva Rweyemamu said:
That almost everybody who supported this process, excluding yourself and a few friends, who led from the very front, is now comfortable in some secure job, and that even people who were directly and openly opposed and even hostile to us, have been accommodated in one form or another in the new administration, and some of us are still in the wilderness, after almost two years of the new administration taking office, is really a matter of a serious story, which needs and should be told publicly, at some stage.

Salva Rweyemamu said:
That everybody of you is comfortable and some few of us are struggling to make ends meet, speaks volumes about our friendships and how we help each other as friends. How could you have allowed such a thing to happen to us? Is it an oversight? Is it that we are incapable to work for the administration or do not deserve some part of the cake?

Fundisho kwetu;
  1. Serikali ya JK iliingia madarakani kwa msaada mkubwa sana wa Rostam na wapambe wake. Hivyo JK hawezi kumchukulia RA hatua yoyote licha ya kelele za wa TZ wengi ikiwemo Mengi aliyeamua kujitoa mhanga.
  2. Kama wengi wa walio madarakani wameingia kwa kujuana na sio sifa za utendaji wao, au hata kama zifa wanazo, watawajibika vipi ili kuendeleza nchi badala ya kutunisha kilichowavutia kwenye utumishi wa nchi yaani vibaba vyao?
  3. Hivi ni kwa nini JK aendelee kuwa raisi kama yeye na mafisadi ni timu moja?
  4. Je bunge letu linasemaje au watasubiri mpaka nchi ifilisike au tuchinjane ndio wamchukulie hatua JK?
Kwa wale wanaotaka JK apewe miaka mingine 5 wajitokeze na kutueleza apewe kwa uzalendo upi alionao?
 
Kazi nzuri sana Inzi. Kwa ufupi, hizi paragraph tatu zinaelezea vema yote juu ya nia ya Salva kumuandikia hii barua Rostam.

Fundisho kwetu;
  1. Serikali ya JK iliingia madarakani kwa msaada mkubwa sana wa Rostam na wapambe wake. Hivyo JK hawezi kumchukulia RA hatua yoyote licha ya kelele za wa TZ wengi ikiwemo Mengi aliyeamua kujitoa mhanga.
  2. Kama wengi wa walio madarakani wameingia kwa kujuana na sio sifa za utendaji wao, au hata kama zifa wanazo, watawajibika vipi ili kuendeleza nchi badala ya kutunisha kilichowavutia kwenye utumishi wa nchi yaani vibaba vyao?
  3. Hivi ni kwa nini JK aendelee kuwa raisi kama yeye na mafisadi ni timu moja?
  4. Je bunge letu linasemaje au watasubiri mpaka nchi ifilisike au tuchinjane ndio wamchukulie hatua JK?
Kwa wale wanaotaka JK apewe miaka mingine 5 wajitokeze na kutueleza apewe kwa uzalendo upi alionao?

Kaka mimi sioni kwa nini JK apewe miaka mingine 5 kwani keshatuonesha kuwa yeye na Rostam ni kitu kimoja. Infact barua hii ilikuwa pia inaenda kwa JK na si RA pekee.

Tunaomba Salva ajiuzulu!!
 
Kwani mlikuwa hamjua kuwa nchi imejaa wanaharamu hata kabla ya vita vya Kagera? Na sio kiutani ni kikwelikweli. Na watu kama hawa hawana aibu wala 'backbone' ni kwa kiswahili fasaha 'makuwadi na matoashi' wasio na chembe ya soni wala haya.

Hivi kweli hata kama ulilishwa fadhila bado unaweza kumwamini mtu ambaye anaweza akawauza wenzake mchana kweupe? Hivi unaweza kumwamini mtu anayeamini vipande vya dhahabu ni Mungu wake? Hivi unaweza kumwamini mtu ambaye 'hajiwezi taabani' na kazi yake ni kuwaondoa wale wote wanaoonekana wanajua kazi kuliko yeye ili azungukwe na watu mabomu kila upande?

Kuna waandishi wa habari wazuri tu nchi nzima lakini unakwenda jalalani kuchukua mtu wa kukaa Ikulu. Anayeigeuza Ikulu danguro lile Baba wa Taifa alilolikataa?

Kikwete ana nafasi ya kutumia mkakati wa Obama mwaka 2010 na hana haja na mafisadi na makuwadi tena!!!!!
 
Hello the Jamii comunity. This is my first time in the community and issues are really tough to our Nation currently. God show us the way give Musa who can lead us out of this mess.
 
Hello the Jamii comunity. This is my first time in the community and issues are really tough to our Nation currently. God show us the way give Musa who can lead us out of this mess.
haya mambo ya MUSA ndo yametufikisha hapa.
Tunahitaji Mtanzania mzalendo maana hata hao wanaoongoza nafsi zetu wameshaonesha failure kwa sana tu. Rejea sakata la DECI (true color)
 
Back
Top Bottom