Footballer ataka kuvunja ndoa ya Jay Dee na Gardner?

cuiusvis hominis est errare,nullius nisi insipientis in errore perseverare=Anyone can err,but only the fool persists in his fault:Marcus Tullius Cicero,Philippica XII,ii,5.
 
Habari hizi wapelekee wale wambea wa clouds radio Gea Habib na wenzake kwenye kipindi chao cha heka heka!!!
 
Baada ya kuwapa michapo ya ukumbi wa disco raining money courtesy of Hasheem Thabeet, sasa nawapa vimbwanga vya masupa staa wengine wa Bongo.

Hawa ni muimbaji Lady JayDee au "Jide" na mume wake, mtangazaji wa zamani wa Redio Clouds, Gardner G. Habash. Lady Jaydee ni muimbaji wa bendi ya Machozi na anaendesha ukumbi wa starehe wa Nyumbani Lounge ulio nyuma ya Best Bite pale jijini Dar.

Ilikuwa ni usiku wa Jumapili, Mei 29, 2011. Credo Mwaipopo anayecheza mpira nchini Sweden alienda Nyumbani Lounge na rafiki yake aitwaye Pacha. Jide alivyomuona Mwaipopo alimrukia na kuanza kumkumbatia. Wakakaa kwa karibu huku Mwaipopo akiwa anamshika kiuno Jide, kwa mujibu wa mashuhuda. Inadaiwa kuwa Jide na Mwaipopo wana urafiki wa karibu kwa muda mrefu. Hata Jide huwa anatoa habari za kumhusu Mwaipopo mara kwa mara kupitia blogu yake, kama habari hii ambayo amewahi kuitoa Jide kuhusu rafiki yake huyo:

Lady Jay Dee: CREDO MWAIPOPO AMEUMIA MGUU

Wapasha stori wanasema ghafla Gardner alitokea na kuanza kuhamisha hasira zake kwa Pacha. Inadaiwa kuwa Pacha aliagiza redbull na maji, Gardner akamwambia leta elfu 10 kama kumkomoa. Pacha akakataa na kumuita mhudumu akamwambia vinywaji hivyo ni shilingi 4,500 tu.
Hapo basi Gardner akaanza kumrushia maneno Pacha na kumtemea mate. Pacha akamjibu kwa kumtemea mate pia. Ukaanza ugomvi, ambapo Mwaipopo na Pacha wakaamua kuondoka kwenda Maisha Club huko Masaki.

Hivyo basi Gardner akawasha gari aina ya Nissan Murano ya mke wake Jide na kuamua kuwafata kina Mwaipopo mpaka Maisha Club. Wakiwa nje ya Maisha Club, Gardner alimfuata Pacha na kuanza kupigana naye hapo nje ya parking ya club hiyo.

Pacha akamwambia Gardner najua tatizo lako ni kuwa Mwaipopo anakula mzigo kwa Jide (yaani wana uhusiano wa mapenzi). Hapo Jide naye akashuka kwenye gari na kumwambia Mwaipopo aache unafiki.

"******** zenu, mnataka kuniulia mume wangu? Mnajua umuhimu wake kwangu?" Alisikika Jide akisema baada ya Pacha kutoa sime na kumtishia Gardner.

Mtu mmoja aliyeingilia kati ugomvi akakatwa na sime shingoni lakini inasemekana hakuumia sana japo damu zilitoka.

Jide, ambaye anasifika kuwa ni mvutaji mzuri wa majani (weed), naye anasemekana mara nyingi hugombana na wasichana wanaoenda hapo Nyumbani Lounge kuwashutumu wanatembea na mume wake.

Nawatakia maisha mema yenye furaha..huyo Jide sijui na Credo Mwaipopo.........Gadner utakula vumbi tu.......nipo ofisini jamani..
 
:violin:Hapo pagumu, mke wako na wenzio pia ni mke wao, gari lake ni lako na wenzio pia ni gari lao. ugomvi wa nini Gadner. hujua Jide anachotafuta kwa hao wenzio, tulia pengine utaona matokeo:peep:
 
mie nilikuwepo. Hiyo story yote kaipika huyu ndugu. Jiulizeni:

Credo ndie mlengwa kwanini agombane na Pacha?
Gadner kachukua gari la mkewe Jide naye alifikaje Maisha club?
Credo anamchukua jide, iweje amkumbatie live?
Gadner kaamua tu kumtemea Pacha mate!!!. LOL

Akili kichwani wana JF
 
Back
Top Bottom