Foleni ya magari barabara ya Mandela mradi wa matrafiki

saluu

Member
Apr 29, 2010
33
2
leo majira ya saa mbili kasoro mpaka saa mbili na nusu nimethibitisha kili nilichokua nakifikiria kila wakati ninapokuta
foleni kubwa barabara ya mandela. maeneo ya songas kuna u turn. Ilikua gari
NO T470 BNT TOYOTA CORONA PREMIO yenye tinted walikua trafic waili wakivizia daladala
zinazogeuza wanazikamata then wanachuka funguo za gari abiria wakiondoka dereva wa daladala
anamkatia trafik mpunga(rushwa) anamrudishia funguo daladala linaenda kupakia abiria pale kitua cha darajani
linaendelea na kazi. mpaka naondoka dala dala saba zilikua zimekamatwa na kuachiwa.

Hii sio mara ya kwanza kwani hata jioni huwa unakuta folen imeanzia mtaa ya garage kabla hujafika extenal sasa wale madereva wenye haraka wakitanua wanakuta polisi wa kituo cha extenal wanawakamata ukienda kituon kuchukua fungua unakata mpunga unaruhusiwa kuendelea na safari

ukifika mtaa ya river side mambo ni hayo hayo kutoka polisi wa kituo cha kibangu.
hakuna kuandikiwa notification wala nn unatoa mpunga wanakuachia.

wanapo kua wamekamata gari hawa matrafik wanawasiliana kwa simu za mkononi na dhani yule
ane ongoza magari ili folen iwe kubwa.

hii hua inatokea hata hata ukifika mtaa ya buguruni ukikuta wapo mtaa karibu na kituo cha mafuta
buguruni folen inaanzia tabata anae tanua anakamatwa anaka mpunga anaondoka

JEE HUU SIO MRADI WA MATRAFIAK
 
PHP:
wanawasiliana kwa simu za mkononi na dhani yule 
ane ongoza magari ili folen iwe kubwa.
Du!
Mpango wa mabasi yaendayo kwa kasi nina uhakika utapigwa vita sana na watendaji wengi tu serikalini!
Nadhani ndiyo maana hauanzi kamwe!
 
Huwa sitetei mtu anaevunja sheria! kwa nini ugeuzie paiporuhusiwa? au kwa nini utanue? haraka isiwe sababu ya kuvunja sheria!
 
huwa sitetei mtu anaevunja sheria! Kwa nini ugeuzie paiporuhusiwa? Au kwa nini utanue? Haraka isiwe sababu ya kuvunja sheria!


na kama kavunja sheria kwanini aachiwe baada ya kukata kitu kidogo?acha kutetea uozo, trafic hawa ni wajinga na washenzi wakubwa, kuna limtu linaitwa waziri sijui kazi yake nini kwenye matatizo makubwa haya ya barabarani!
 
Kwakweli mleta mada umeona mbali, naamini katika jiji hili hakuna barabara yenye jam kama hii. hilo linajulikana kwamba wanataka wapate rushwa kwa wale watakaotaka kuwahi.
pili wanawasiliana na vibaka wa kundi la Matembo ili wapate magari ya kukwapu vioo vya magari pindi tunaposimama mda mrefu.

katika maisha yangu ya sasa jijin DSM hii ndio kero yangu kubwa katika masuala ya usalama barabarani ...... ni mbinu chafu za kujipatia rushwa thats 100% true mkuuu anaebisha ni gamba!

kutoka mabibo Hostel kwenda mwenge masaa matatu!!!!!!!!!!!!!!!! huu ni upuuzi usiovumilika!!!
 
Tatizo la barabara ya Mandela ni nyembamba kulinganisha na traffic ya magari makubwa yanayoingia na kutoka bandarini. Moja ya kielelezo cha kushindwa kwa viongozi wetu! Barabara hii inatakiwa kuwa angalau na njia 4 zinazoingia na 4 kutoka na pale Ubungo mataa wajenge daraja la juu. Barabara ya Morogoro inatakiwa mpaka Kibaha iwe na njia 6 zinzoingia na 6 kutoka kwa kiwango kikubwa foleni itapungua na matraffic hawatakua na sababu za kupiga bao hapo Ubungo!
 
kwa nini utanue? Hapo mnawatajirisha matrafiki bila sababu, trafiki wenyewe mnajua wanategesha.....
 
Back
Top Bottom