Florian Kaijage apigwa chini TFF

katika itv leo usiku waziri Mkuchika ametoa agizo TFF imchukulie mtu yeyote atakae dhirihika kuhusika na uzembe uliosababisha nyimbo za taifa zisichezwe hapo uwanja wa taifa. Wakati huo akijua wazi kuwa TFF ilishachukukua hatua ya kumsimamisha msemaji wake bw Kaijage.je hamuoni hatua hiyo ya serikari itapelekea FIFA kutuchukulia hatu kali kama walivofanya kwa Nigeria?
 
Lazima kitu kama kile kiwe na majeruhi. Bahati mbaya majeruhi sio wacina waliojenga uwanja...ni ofisa habari wa TFF
 
At least tumeona hatua za mwanzo zimefanyika, Jk kazidi kuwa mpole, ila mi napata shida na kuunda tume wanamtafuta mchawi wa nini? si wamempata wamemsimamisha ni adhabu tosha sasa kumaliza pesa tu za bure watarudi na majibu yasiyoridhisha kama tume zlizopita kwenye nyanja mbalimbali.
 
Binafis naona kama si kukurupuka wamemtoa kafara tu kaijage . Japo Kaijage ni mdau kwenye hiyo kasfa Muhiska mkuu aliyetakiwa kuwajibishwa ni Fundi mitambo mkuu wa huo uwanja.

Lakini kibong bong sitashanga kusikia uwanja kama huo hauna mtu maalum aliyeajiriwa kwa job specification za kueleweka za fundi mitambo.

Sioni kama hili ni tatizo la TFF bali ni Tatizo la Management ya uwanja.
Hivi muziki ukishindwa kucheza kwenye harusi utamlaumu MC?

Labda kama kaijage alishindwa kuiwakilisha hiyo CD za nyimbo kitu mabacho probability yake kwangu naona ni below 0.2


Nahakika kuna wanasheria wameshajitolea kununua hiyo kesi ya kijage na nadhani atawakamua TFF kwa fidia.
 
Naamini Tume or whatever .....ili mradi Vichwa vinavyotakiwa kupasha ....Vichungulie pamoja na mambo mengine michakachuo katika nyanja zifuatazo :-
1) Timu ya Taifa iweke au iongeze nafasi ya kushaulika,hususani by wadau wakuu.... IkumbukWe Timu yoyote ni mjumuiko wa Kocha,Wafadhili,Wachezaji,mashabiki,wapinzani,na NAWEKA nafasi moja ya Wachezaji wa zamani .....wadau wote hawa wana nafasi sawa za kusikilizwa Ushauri wao.
2)_Mikakati ya muda mfupi na muda mrefu iwekwe ili timu iwe ya ushindi.... Kushinda ikumbukwe ndilo lengo letu.
Katika mikakati ya muda mfupi sehemu kubwa ya wadau wotE inajua nani anayemudu namba fulani as at today kuliko wote.
Tunaweza kuanzia hapo kumodel Killer Squad !
Mikakati ya muda mrefu,inaweza kutumika kumodel Timu ya baadaye.
TUNATAKIWA KUFANYA MASHAMBULIZI HAYA KWA PAMOJA.
3) Nadhani Uzalendo kwa wadau wote uwe dira yetu Kuu...Tuweke nyuma mambo yote yanayohusisha Ubinafsi,ubabaishaji,kutowajibika,upotoshaji,ulegevu .... Si mnajua hayo yote ni adui wa timu yoyote duniani !
Maana Wahenga husema mshika mbili moja humponyoka.
Let us be a team Please .....Tunataka bao..
 
Back
Top Bottom