Five killed in Barrick Tanzanian mine attack

Mbona polisi huwa hawalindi mashamba ya kilosa yanayovamiwa mara kwa mara na wafugaji?au gold ina maana zaidi kuliko binadamu?
 
Mimi nawashangaa sana wakuu wa JF na maoni yao humu jamvini. Pamoja na kwamba siungi mkono vitendo vyovyote vya ukandamizaji vinavyofanywa na dola au/na vyombo vyake, siwachi kujiuliza, mlikuwa wapi Wazanzibari walipokuwa wakipigwa, kuuliwa, kunajisiwa na kadhalika ndani ya nchi yao?

Kuweni fair.


View attachment 30266


View attachment 30268
hiyoJF unayosema imewapotezea na haiwaungi mkono wa Zanzibar je wakati wa mauwaji ya huko ilikuwepo?
 
Porti wewe aijakuuma kama mimi. YANI NASEMA KWA WANANGU WA TARIME WASIONEA YOYOTE YENYE KUVUA GAMBA HURUMA NI KUFIEKA TUU. AIWEZEKANI NA HUYO KIKWETE AMEKAA KIMYA KWELI ///

JAMANI LET THE CURSE BE ON THEM AND LET THEM BE CURSED FOREVER:sick:
 
dah!too bad....hivi hawa viongozi, na polisi ni kaka na baba zetu kweli? waTz hawahitaji kuchochewa na mtu yeyote kudai haki yao na kulinda rasilimali zao au kudai uwajibikaji wa serikali yao..
wananchi 800 - 1500 hawawezi kuwa wanaenda kuiba dhahabu! haiingii akilini eti kina baba, kina mama, vijana wazee na watoto takribani 1000 waende kuiba dhahabu mgodini kwa mzungu kama Kagasheki na Polisi wanavyosema na wanavyotaka tuamini, kuwa eti ni wahalifu! hawa wananchi wana'madai yao na kero zao ambazo zitakuwa zimepuuzwa, wamechoshwa na ulegelege wa serikali yao ktk kusimamia haki zao.
Mbunge wa upinzani anayezungumzwa ni Lema, ameenda kuangalia waTZ wenzake,yeye ni kiongozi, after all ni waziri kivuli wa mambo ya ndani, so his presence is justifiable! Serikali yetu inaogopa watu wake, wanaogopa kuukabili umma wa watanzania, thats why wanaishia kusema ni uchochezi na kuirushia CDM lawama, HADI LINI? SERIKALI IAMKE....mda c mrefu no place will be safe for them and for all people in green! wataishia kuvaa nguo zao za kijani kwenye party zao za kuvuana magamba, huku mtaani watapigwa mawe
.
 
Thursday, 19 May 2011 22:33

Anthony Mayunga, Tarime

FAMILIA za ndugu waliopigwa risasi na kufa katika mgodi wa African Barrick North Mara, zimeigomea Serikali kuzika miili ya marehemu wakitaka ufanyike kwanza uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.Mbali na kugomea mazishi, familia hizo pia zimekataa kupokea rambirambi za polisi katika msiba huo, zikidai kuwa rambirambi hizo hazina umuhimu kuliko maisha ya ndugu zao.

Hatua hiyo ilimchanganya Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi, Paul Chagonja ambaye aliwakilisha Jeshi hilo kuwasihi wananchi hao bila mafanikio.Mbele ya wananchi hao waliofurika eneo la hospitali, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alisema anaunga mkono msimamo wa kukataliwa kwa rambirambi hizo za Serikali, akieleza kuwa hajawahi kusikia Jeshi la Polisi linaua na kuzika kisha kutoa ubani.
“Hapa tunatafuta haki wala si siasa kama wanavyopotosha, lini polisi wakaua majambazi kisha wakazika na kutoa rambirambi? Kuna kitu kimefichika hapa, hivyo mimi nasema kama ni rambirambi sisi tutatoa, lakini pia ninyi wananchi hamuwezi kuchangia hata Sh1,000?,” Alihoji na kujibiwa "tunawezaaa."

Alisema kuwa baada ya kujadiliana na kupata utaalamu wa kisheria kutoka ngazi za juu, Chadema kimekubaliana na familia na viongozi kuwa maiti hazitachukuliwa mpaka kesho, siku ambayo Waziri Kivuli wa Sheria na Mambo ya Katiba,Tundu Lissu, wakili Mabere Marando na mjumbe wa tume ya haki za binadamu watakapofika.

“Takwimu zinaonyesha kuwa watu 23 wameuawa na polisi eneo hilo, presha ya kuzika ya nini wakati hawatafufuka? alihoji na kuendelea:"Tunataka liwe fundisho, tumezitaarifu balozi za Canada na Norway na wanaweza kuja huku, huduma hizi tutadili nazo sisi, huwezi kuogopa gharama katika kudai haki,”alibainisha.Chagonja,RPC wapingana Wakati Lema akieleza hayo, Kamishna Chagonja amekanusha taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Mkoa wa Kipolisi wa Tarime, Constantine Massawe kuwa waliouawa walikuwa majambazi.
“Jamani hawakuwa majambazi mimi ndiye mkubwa nimekuja, kauli yangu ifanyiwe kazi si hizo zilizokwishatolewa. Walivamia mgodi tu, ndiyo maana tunataka kutoa rambirambi na kuwataka wazikwe," alisema.

Alisema lengo la kufika kwake ni kueleza msimamo wa Serikali kuwa tume itaundwa kuchunguza mauaji hayo na wahusika watakaobainika watachukuliwa hatua bila kuangalia nyadhifa zao.
“Tunaomba ndugu wakubali kuchukua miili ya marehemu, wakubali kuzika maana kukaa na maiti bila kuzika haisaidii, mimi nimetumwa kwa kazi hiyo, wengine wanawapotosha,”alidai.Hata hivyo, Kamishna Chagonja hakueleza tume hiyo itaundwa lini na itahusisha watu gani, akieleza kuwa hatua hiyo inafanywa na ngazi ya juu zaidi.

Wakati Kamishna Chagonja akisema hayo, Kamanda Massawe alilazimika kuikana kauli yake akisema "jamani sijasema majambazi, bali wavamizi,”

Diwani aingiwa hofu
Diwani wa Kata ya Matongo, Bathlomeo Machage alisema kuna vitisho vinavyoendelea kwa baadhi ya watu kwa madai kuwa wanagomea uchukuaji wa maiti hizo na kuwa watabambikiwa kesi za mauaji.“Mimi naambiwa nilimpiga mbunge kama mimi nazuliwa je wananchi wa kawaida inakuwaje? Alihoji na kuendelea: "Haya mambo yanatakiwa uongozi wa serikali wawepo hapa kama DC na mbunge, ambao hawapo inakuwaje polisi ndio washinikize suala hilo?”
Wakati huohuo baadhi ya askari polisi mjini hapa wameonyesha kufurahia kitendo cha wananchi kuushambulia kwa mawe msafara wa Mbunge wa Tarime Nyambale Nyangwine na mwenyekiti wa halmashauri wakisema: "Afadhali wameonja joto la jiwe"

Polisi hao wamechekelea kuvunjika kwa ziara hiyo baada ya kusikia kuwa tayari mbunge huyo amemwandikia barua Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime na Rorya kutaka polisi itaje majina ya askari wake waliowaua watu hao ili sheria ichukue mkondo wake.

Baadhi ya askari ambao hawakutaka kutajwa majina yao waliliambia gazeti hili kuwa kitendo cha mbunge na msafara wake kupigwa mawe, kinaonyesha wazi kuwa hata askari waliohusika na mauaji walikuwa wakijihami.

Walidai kuwa hali ilivyo kwa sasa eneo hilo kumechafuka na kama hatua za makusudi za Serikali hazitachukuliwa haraka, mauaji yataendelea kwa kuwa askari hawatakubali kufa kibudu wakiwa na silaha.
DC azungumza
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewelle aliliambia gazeti hili kuwa Serikali imeshachukua hatua za makusudi za kuitaka kampuni ya African Barrick North Mara kuwalipa fidia stahiki wahusika waweze kupisha haraka iwezekanavyo.

“Tayari hilo linashughulikiwa tena na wataalamu wa Serikali wanahusishwa kusimamia kuhakikisha sheria ya fidia inatumika, watu walipwe stahili zao wapishe, maana inakuwa ngumu kiusalama kufanya kazi za uchimbaji na wananchi wako ndani ya eneo ,”alisema.

Alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa mchakato huo unakwamishwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na vijiji kwa kuwashawishi wananchi wasikubali kuhama maeneo hayo.

Mwenyekiti wa Kijiji
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kewanja, Kata ya Kemambo, Tanzania O’mtima aliliambia Mwananchi kuwa mauaji yanayofanywa si suluhisho bali yanazidisha chuki kubwa.“Nakupa takwimu za kutoka mwaka 2009 nilipoingia madarakani, vijana watano kutoka kijijini kwangu wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi, acha waliojeruhiwa na kuwa walemavu, ni wengi sana,”alidai.

Madai ya wizi wa maiti
Kaka wa mmoja wa watu waliouawa kwa kupigwa risasi na askari polisi, Marwa Mwita Mwasi, ameibuka na kudai kuwa maiti ya mdogo wake imeibwa na kutoroshwa usiku wa manane.Alisema mdogo wake Chacha Mwasi aliuawa Mei 16 mwaka huu baada ya kupigwa risasi na askari polisi. Mwili wake ulihifadhiwa chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Marwa alidai kuwa Mei 17 mwaka huu baada ya kukosa mwafaka kati ya Serikali na wao, alitoka na kwenda kwa jamaa yake kwa ajili ya kusubiri utaratibu Mei 18 kama watazika ama la."Nikiwa kwa ndugu yangu, mke wangu saa 5 za usiku Thereza Bhoke, alinipigia simu akitaka kujua niko wapi, nikamwambia niko Tarime, akadai mbona maiti imeletwa na wewe haupo inakuaje?” Alisema.

Alisema aliambiwa kuwa maiti imefikishwa katika Kijiji cha Bisarwa Bhukenye na magari ya Serikali, lakini yeye aliwaambia kuwa hakushirikishwa kuchukuliwa kwa mwili huo na kuwa waliuiba kwa nia ya kutaka kudhoofisha msimamo wao.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Pracidia Rweyemamu alikiri maiti hiyo kuchukuliwa na kuwa walijitokeza ndugu wakiwamo katibu tarafa.“Ni kweli niliombwa na ndugu wa familia nami natokea huko nikaomba halmashauri wakatoa gari. DC akatoa laki moja za jeneza na wakati wa kuchukua, kamati ya ulinzi na usalama ilikuwapo, mimi nilisaidia tu na nimekuwa nikitoa msaada mara kwa mara,”alieleza katibu tarafa aliyejulikana kwa jina moja la Machango.
Nao Fidelis Butahe na Patricia Kimelemeta wanaripoti kutoka Dar es Salaam kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amewataka wananchi wanaoishi karibu na migodi kufuata sheria na taratibu ili kuondoa tofauti zinazojitokeza baina yao na wawekezaji.

Waziri Ngeleja alisema hayo jana kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya Wakala wa Ukaguzi wa Migodi (TMAA),uliofanyika jijini Dar es Salaam.“Kuna migogoro inayotokea kwenye baadhi ya migodi. Hii inatokana na baadhi ya wanasiasa kuchochea vurugu ambazo zinaweza kuhatarisha amani kwenye maeneo yao. Wajibu wa watu hao ni kushirikiana pamoja ili kuondoa tofauti yao,”alisema Ngeleja.

Aliongeza kuwa Serikali kupitia kampuni ya mgodi wa Barrick wameandaa mradi wa kuwasaidia wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kimitaji ili waweze kupata vifaa vya kisasa vya kuchimbia madini.
 
Ni aibu kwa serikari kufikia hatua ya kuiba maiti kulazimisha yaishe wakati wananchi wana machungu ya ndugu zao ku uwawa na polisi wanaopaswa kuwalinda raia ndani ya nchi yao huru, yaani wageni na wawekezaji wanathaminiwa kuliko mtanzania

Hivi tumefikia hatua hii ya thamani ya mtanzania kuuwawa kama mbwa ndani ya ardhi yao kisa wawekezaji wasiokuwa na tija kwa uchumi wetu.

Hii laana na usaliti wa serikari ya chama cha mapinduzi kwa watanzania itawatafuna mpaka vizazi vyao na tutawalaani mpaka kwenye makaburi yao. haiwezekani watanzania wafe kama kuku ndani ya nchi yao wakitetea maslahi yao na tena wanaitwa majambazi, baada ya moto kuwashwa na chadema chagonja anabadilisha kauli eti sio majambazi, inakuwaje polisi waue majambazi halafu watoe ubani na gharama za mazishi kwa majambazi?
 
• Mbunge Lema apambana na kamishna wa polisi

na Mwandishi wetu


MAUAJI ya watu watano waliouawa na polisi, Tarime mkoani Mara kwa madai walikuwa ni wahalifu waliotaka kuvamia mgodi wa North Mara Barrick sasa ni dhahiri yameikoroga serikali na taifa kwa ujumla.
Jana Jeshi la Polisi pamoja na kutuma timu ya maofisa waandamizi kutoka makao Makuu ya Jeshi hilo, lilishindwa kuwashawishi ndugu wa marehemu hao ambao walikataa kusitisha mgomo kususia miili hiyo hadi serikali itoe tamko la kukomeshwa mauaji hayo na wahusika kuchukuliwa hatua.
Timu ya maofisa waandamizi kutoka makao makuu ya jeshi hilo ikiongozwa na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja walilazimika kuondoka pasipo kufikia muafaka katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya baada ya mamia ya waombolezaji waliopiga kambi tangu Jumatatu kukataa mapendekezo yao.
Awali Kamishna Chagonja aliwahutubia wananchi hao akiwataka waridhie miili hiyo ifanyiwe uchunguzi na kuchukuliwa kwa ajili ya mazishi yatakayogharamiwa na serikali lakini juhudi zake ziligonga mwamba baada ya ndugu wa marehemu kukataa mapendekezo hayo, kwanza wakitaka taarifa ya serikali kulaani mauaji hayo.
"Sisi tumekuja hapa kushirikiana nanyi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi sasa tunawaomba mridhie kufanyika uchunguzi halafu taratibu nyingine za mazishi zifuatwe ambapo pia tumejitolea kama jeshi la polisi kushiriki kwa kutoa msaada wa hali na mali ili tufanikishe zoezi hili, tunaomba mkubali kufanyika uchunguzi na tume huru itaundwa kuchunguza tukio hilo," alisema Changonja.
Kauli yake hiyo ilipingwa vikali na waombolezaji hao ambao walishikilia kuwa kwa vyovyote vile ilivyotokea hakukuwa na sababu ya kuhalalisha vifo hivyo kwa sababu polisi ndio wahusika na walitumia nguvu nyingi kupita kiasi kukabiliana na raia wasiokuwa na silaha za moto.
Wakiongozwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema (CHADEMA) aliyepiga kambi katika eneo hilo, wana ndugu hao walidai ingawa hawakupinga kuendelea na zoezi la mazishi lakini wasiwasi wao ulitokana na uharaka wa jeshi hilo kutaka kupoteza ushahidi kwa kulazimisha kufanyika mazishi.
Lema apambana na kamishna wa polisi
Katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti, mbunge wa Arusha mjini, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Lema alilazimika kumhoji Kamishna Changoja kwa maswali mazito akitaka kujua uharaka wa Jeshi la Polisi kufanya maziko tena ya watu waliowaita kuwa ni wahalifu.
"Kwa nini mnaharakisha maziko bila kuwepo kwa mtu anayewafanyia postmotem? Wewe unasema umetumwa na serikali umetoka makao makuu kuja kuiwakilisha serikali ni serikali ipi unayoiwakilisha?
"Asubuhi Waziri Kagasheki amesema waliouawa ni wahalifu… umekuja hapa huna mkuu wa mkoa, wilaya wala mbunge unamwakilisha nani kwenye serikali iliyokutuma? Ninatilia mashaka uharaka wa serikali kuwazika watu hawa. Ina maana serikali inazika majambazi? Umeanza lini utaratibu huu?" alihoji Lema.
Alisema polisi na serikali yao kuamua kutoa sh milioni tatu kwa kila marehemu kwa ajili ya maziko haijawahi kutokea.
Akizungumza na gazeti hili Lema alisema; "Wakati namuuliza chagonja anasema nisilete siasa kwenye jambo hilo hivi nani sio mwanasiasa? Huyo waziri aliyesema waliokufa ni wavamizi naye mwanasiasa.
"Kwa niaba ya chama changu tumefanikiwa kushwawishi ndugu wote wa marehemu na wameshawishika tukaondoka kwa pamoja pale chumba cha kuhifadhi maiti tukamuacha Chagonja na polisi wenzake, tumemwambia tunaahirisha maziko haya hadi postmotem itakayosema marehemu waliuawa kwa kupigwa risasi wapi kama ni mguuni au kichwani tujue," alisema Lema.
Kauli nyingine ya Kagasheki
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamis Kagasheki, amemtuhumu mbunge mmojawapo wa chama fulani cha siasa (hakukitaja) kuhusika katika tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwile (CCM), aliyedai kufika katika eneo la Nyamongo kwa ajili ya kuwafariji ndugu wa marehemu waliouawa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa sera ya ukimwi eneo la kazi kwa jeshi la polisi nchini, Waziri Kagasheki alisema mbunge wa chama hicho cha siasa alitoka jimboni kwake na kufika kwenye jimbo lingine kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kufanya fujo.
"Suala la Nyamongo sitaki kulizungumzia kwa kina, ila niseme kwamba kuna mbunge mmoja wa chama fulani cha siasa, alisafiri kutoka jimboni kwake na kwenda jimbo hilo kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kufanya fujo….
"Kitendo kama hicho na vingine vinavyowiana kamwe haviwezi kuvumiliwa ndani ya nchi…," alisema Waziri Kagasheki.
Alipoulizwa ni hatua gani serikali itazichukuliwa dhidi ya mbunge huyo, Waziri alishindwa kuweka wazi.
"Nimeshasema sitaki kulizungumzia kwa kina suala hilo, na kuliweka wazi mbele ya umma…." alimaliza na kuondoka.
Ngeleja naye azungumza
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ameeleza kusikitishwa na vurugu zilizotokea katika mgodi wa dhahabu wa North Mara. Ngeleja alieleza hayo jana alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua tamko la wizara yake kuhusu vurugu hizo mgodini.
"Tumesikitishwa na taarifa hizo pamoja na vifo vilivyotokea tunatoa salamu za pole kwa wafiwa, kwa sasa vyombo vya usalama vinashughulikia hali hiyo," alisema Waziri Ngeleja baada ya kuzindua bodi ya wakala wa ukaguzi wa madini.
Alisema pamoja na mambo mengine, serikali kupitia wizara yake imekuwa ikifanya juhudi kuhakikisha katika eneo hilo kunakuwa na mahusiano mazuri kati ya wawekezaji na wananchi wa eneo hilo.
Alieleza pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo katika eneo hilo tayari serikali na wawekezaji wamebuni mradi wa uchimbaji mdogo wa madini ambao utaanza baadaye mwaka huu ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.
Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 23 wameuawa kwa vipindi tofauti kwenye mgodi huo. Hata Barrick wenyewe wanasema nia yao si kuua raia hivyo hawakubaliani na kitendo kilichofanywa na polisi.
 
""Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamis Kagasheki, amemtuhumu mbunge mmojawapo wa chama fulani cha siasa (hakukitaja) kuhusika katika tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwile (CCM), aliyedai kufika katika eneo la Nyamongo kwa ajili ya kuwafariji ndugu wa marehemu waliouawa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa sera ya ukimwi eneo la kazi kwa jeshi la polisi nchini, Waziri Kagasheki alisema mbunge wa chama hicho cha siasa alitoka jimboni kwake na kufika kwenye jimbo lingine kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kufanya fujo.
"Suala la Nyamongo sitaki kulizungumzia kwa kina, ila niseme kwamba kuna mbunge mmoja wa chama fulani cha siasa, alisafiri kutoka jimboni kwake na kwenda jimbo hilo kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kufanya fujo….
"Kitendo kama hicho na vingine vinavyowiana kamwe haviwezi kuvumiliwa ndani ya nchi…," alisema Waziri Kagasheki.
Alipoulizwa ni hatua gani serikali itazichukuliwa dhidi ya mbunge huyo, Waziri alishindwa kuweka wazi.
"Nimeshasema sitaki kulizungumzia kwa kina suala hilo, na kuliweka wazi mbele ya umma…." alimaliza na kuondoka""


Hivi waziri tena wa mambo ya ndani anapozungumza kimbea hivi, sie wananchi tumweleweje? Arrrggggggyyyy!!
 
Ee Mola tusaidie watanzania.Wale tuliowapa dhamana ya kutulinda wamekuwa kinyume chetu.wana nguvu sana kutuzidi na hawana masikio ya kusikia kilio chetu,tulifarijika tulipogundua wana macho tukasema hebu tuwafuate labda wataona haya!maskin kumbe ndo tumejipeleka wenyewe ahera.poleni Tarime Mungu ndiye mwamuz wa haki tusikate tamaa,tuzid kuomba.
 
Hao siyo inruders hao ni wenye mali wachoka na ujinga wa wezi wajimba madini kuiba kwa kushirikiana na viongozi wetu hivyo hawana mtetezi zaidi ya kujimibilise na kutumia mawe, nawapongeza kwa kwenda kushare kuchukua mali zao kwa majizi haya na hao waliokufa wamekufa kishujaa na wengige wauinge mkono vuguvugu hilo hasa kwenye migodi ya Buzwagi na Kahama mine

Kicheruka, shame upon you na kizazi chako chote. Wewe unakula kuku kwa mrija harafu unashangilia watu wa kijijini kupoteza wapendwa wao ati"wamekufa kishujaa". Suppose huyo polisi aliyeumizwa ni wewe, je bado utashadadia ujinga huu wa watanzania kuacha kufanya legal activities na kwenda kudokoa mali za watu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom