Five killed in Barrick Tanzanian mine attack

Habari nilizonazo waliokufa wamefika wanane(8) vijana hawa wangekuwa nguvu kazi kubwa na chachu ya maendeleo kwa taifa hili! Police wa tz wanafundishwa kupiga raia risasi kifuani hata kama hana siraha wala chochote!

Cha ajabu zaidi maamuzi ya kuua yanatolewa na watu wakubwa wilayani! Mungu wangu tuongezee ujasili wanyamongo tuendelee kudai haki zetu japo selikari imelifumbia macho na wala mambo haya hayatangazwi na vyombo vya habari?

Kuna siku nilipata tatizo pale Nyamongo nikaenda police! Nilijibiwa kuwa askari wote wako mgodini (kuuwa watanzania wasio na hatia?) issue yangu itashughulikiwa siku askari wakiwepo! Niliamua tu kuacha kwani niliktwepo kwa kazi ya muda mfupi!

MUNGU IBARIKI TANZANIA ,MUNGU IBARIKI NYAMONGO!
 
Jamani nayaongea haya kwa uchungu sana kama mnyamongo na mtanzania pia mhanga wa 2kio hili maana nimepoteza shemeji na rafiki yangu" HIVI HAKI YETU WANYAMONGO TUTAIPATA LINI?" Mbona kila siku wanainchi wanauwawa nadhani ni wakati wa kutoka wote kama tutakufa tuishe na iwe hivyo! Watanzania wenzetu wanatuua kwa ajili ya mawe ya kwetu? Haki yetu inabidi tuidai kwa kufa na kupona' PEOPLES POWER

Pole sana kwa huo wa shemeji na rafikiyo,huu ni msiba wa taifa..inauma sana kuona hali hii...
 
Upendeleo wa wawekezaji badala ya wananchi waanza kuleta yale tuliyokuwa tunayaogopa. Inasemekana wananchi waliokata tama baada ya Serikali kuwakumbatia wawekezaji badala ya wanachi, hatimaye maafa makubwa yametokea wilayani tarime kwenye mgodi wa Barrick.
Swali: Je, bila kuwa na sera makusudi zinazowanufaisha wanachi, je, Tanzania tutakuwa na amani kama haki haitendeki ? Soma habari ifuatayo- :

" WATU watano wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mapambano kati ya polisi na raia wanaodaiwa kuvamia mgodi wa North Mara Barrick, wilayani Tarime jana alfajiri kwa lengo la kupora mawe ya dhahabu.

Watu wapatao 800 walivamia mgodi huo kwa lengo la kuchukua dhahabu kutoka kinu cha kusagisha mawe hali iliyowalazimu polisi kutumia risasi za moto.

Licha ya waliouawa, watu 10 wakiwamo polisi walijeruhiwa katika mapambano hayo ambayo wananchi walikuwa wakitumia silaha za jadi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tarime/Rorya, Constantine Massawe, alisema jana kuwa, kundi hilo la wavamizi lilikuwa na mapanga, marungu, makombeo na mawe.

Alisema, alituma kikosi cha Polisi waliokuwa na mabomu kuongeza nguvu katika mapambano na wavamizi hao waliojihami kwa mawe na marungu.

Alisema, polisi walilazimika kutumia risasi za moto baada ya kuzidiwa nguvu na kundi hilo.

Katika mtafaruku huo, magari ya Polisi na ya mgodi yaliharibiwa kwa kuvunjwa vioo kwa mawe. Hilo ni tukio la tatu mgodi huo kuvamiwa katika kipindi cha siku nne.
Alhamisi wiki iliyopita, Polisi ilisema watu zaidi ya 500 wa vijiji jirani na mgodi huo, walivamia kwa lengo la kupora mawe ya dhahabu.

Uvamizi mwingine ulifanyika Jumamosi. Miongoni mwa watu waliozungumzia hali hiyo ni pamoja na aliyekuwa Diwani wa eneo hilo lenye mgodi, Augustino Neto, aliyeishauri Serikali itafute utaratibu wa kuwapa wananchi maeneo ya kuchimba dhahabu ili kuepusha chuki iliyojengeka baina ya jamii dhidi ya mgodi huo. "

---------/

Chanzo cha Habari ni Gazeti la Habari leo
Imeandikwa na Samson Chacha, Tarime; Tarehe: 16th May 2011
 
Kama kuna mtu anajuana na organiser wa hawa wananchi wanaooneWa ndani ya ardhi yao anipe contact, nitampa mchongo wa ma AK-47 ili kupambana na hawa mafisadi, si hawataki hata kuongeza kodi kwenye madin i ili hali every day price of gold is hiting worlid record,.we have to take our stones and its our right if they dont give a f$#@^ we do the same
 
Nauliza tu, wamejuaje kama ni 800, wamehesabu vipi? Au hua wanakisia tu? Bif la tarime haliishagi mpaka kieleweke kama MISRI wana mean busness.
 
Habari hii inatofauti gani na ile ya zanzibar watanganyika kuchomewa biashara zao,na sababu kuu ilikuwa wamefungua biashara hizo kinyume na sheria,na wanakijiji walishapeleka habari kwa vyombo vya dola lakini walishindwa kuchukua hatua za kisheria na kulitupilia mbali na wananchi kuchua hatua mikoni mwao,lakini kwa utashi wa maneno yamekuja mambo ya kubaguzi baina ya mzanzibari na mbara.

Jee hili tukio katika mgodi ingelikuwa wachimbaji ni wazanzibar na walivamia ni wababra jee mungelichukuliaje ? Kisiasa ? Kiukabila ? Au kijamii ? VIPI ?
 
Kama kuna mtu anajuana na organiser wa hawa wananchi wanaooneWa ndani ya ardhi yao anipe contact, nitampa mchongo wa ma AK-47 ili kupambana na hawa mafisadi, si hawataki hata kuongeza kodi kwenye madin i ili hali every day price of gold is hiting worlid record,.we have to take our stones and its our right if they dont give a f$#@^ we do the same

Nguvu ya wananchi inaanza kuchukua sura mpya kwani haiwezekani mafisadi waendelee kujitajirisha na rasilimali za wantanzania ili hali wenye nazo hawana hata fetha za kununulia hata panadol. Kwa kweli inauma sana !
 
Habari hii inatofauti gani na ile ya zanzibar watanganyika kuchomewa biashara zao,na sababu kuu ilikuwa wamefungua biashara hizo kinyume na sheria,na wanakijiji walishapeleka habari kwa vyombo vya dola lakini walishindwa kuchukua hatua za kisheria na kulitupilia mbali na wananchi kuchua hatua mikoni mwao,lakini kwa utashi wa maneno yamekuja mambo ya kubaguzi baina ya mzanzibari na mbara.

Jee hili tukio katika mgodi ingelikuwa wachimbaji ni wazanzibar na walivamia ni wababra jee mungelichukuliaje ? Kisiasa ? Kiukabila ? Au kijamii ? VIPI ?

Hivi Zanzibar ipo Tz au ipo wapi vile? Hivi Tanganyika kuna wazanzibari wangapi wanaishi na kufanya biashara zao? Hivi wale watanganyika waliokuwa na maduka Zanzibari walikuwa ni wawekazaji wa kigeni huko!! Kama wazanzibari si watanzania, wangevamiwa tu, ila kama wazanzibari ni watanzania wasingevamiwa, tungechimba pamoja bila upendeleo.
 
Hivi hii vita kati ya maintruder na police wa mgodi itaendelea mpaka lini? Maana jana wameuwawa 4 na 7 kujeuliwa kwa risasi za moto,na hii ci mara ya kwanza wameishauwa watu kibao hata siku za nyuma,serikari inakuja wanafanya vikao vyao, lakini hmn jipya tunaloona.
Kwanini serikari isiushauri uongozi wa mgodi ukawalipe watu wakaamie mbali,m'na kijiji kiko krb na mgodi na wao wanataka riziki kwa kuokota mawe ya zahabu ijapokuwa baathi ya wengine wanafanya fujo kwa kurusha makombeo kwa police na walinzi.
Nimewasilisha.
 
Habari hii inatofauti gani na ile ya zanzibar watanganyika kuchomewa biashara zao,na sababu kuu ilikuwa wamefungua biashara hizo kinyume na sheria,na wanakijiji walishapeleka habari kwa vyombo vya dola lakini walishindwa kuchukua hatua za kisheria na kulitupilia mbali na wananchi kuchua hatua mikoni mwao,lakini kwa utashi wa maneno yamekuja mambo ya kubaguzi baina ya mzanzibari na mbara.

Jee hili tukio katika mgodi ingelikuwa wachimbaji ni wazanzibar na walivamia ni wababra jee mungelichukuliaje ? Kisiasa ? Kiukabila ? Au kijamii ? VIPI ?

Amiii!
Naona unalinganisha mbingu na pepn! Hivi ni vita vya rasilimali kati ya wenyeji dhidi ya wageni mafisadi wanaolindwa na serikali. Watanganyika sio wageni ndani ya zanzibar. Wala hawagombanii rasilimali za TZ dhidi ya waz'bar. Wana haki ya kuishi popote ndani ya nchi hii kama vile tunavyoishi na wapemba jengo moja hapa Arusha!
 
Jamani nayaongea haya kwa uchungu sana kama mnyamongo na mtanzania pia mhanga wa 2kio hili maana nimepoteza shemeji na rafiki yangu" HIVI HAKI YETU WANYAMONGO TUTAIPATA LINI?" Mbona kila siku wanainchi wanauwawa nadhani ni wakati wa kutoka wote kama tutakufa tuishe na iwe hivyo! Watanzania wenzetu wanatuua kwa ajili ya mawe ya kwetu? Haki yetu inabidi tuidai kwa kufa na kupona' PEOPLES POWER

Mbona mapambano yanakuja kwa msimu...yaani mnaanza then mnatulia...?kwanini msipambane mpaka kieleweke? Najua unajua ni kwanini nimeuliza hili...
 
Hizi ni dalili za mwanzo tu za watu kuchoka kuibiwa rasilimali zao mengine makubwa kuliko haya yanakuja....magamba kaeni tayari na waume zenu mnaowaita wawekezaji
 
Habari nilizonazo waliokufa wamefika wanane(8) vijana hawa wangekuwa nguvu kazi kubwa na chachu ya maendeleo kwa taifa hili! Police wa tz wanafundishwa kupiga raia risasi kifuani hata kama hana siraha wala chochote!

Cha ajabu zaidi maamuzi ya kuua yanatolewa na watu wakubwa wilayani! Mungu wangu tuongezee ujasili wanyamongo tuendelee kudai haki zetu japo selikari imelifumbia macho na wala mambo haya hayatangazwi na vyombo vya habari?

Kuna siku nilipata tatizo pale Nyamongo nikaenda police! Nilijibiwa kuwa askari wote wako mgodini (kuuwa watanzania wasio na hatia?) issue yangu itashughulikiwa siku askari wakiwepo! Niliamua tu kuacha kwani niliktwepo kwa kazi ya muda mfupi!

MUNGU IBARIKI TANZANIA ,MUNGU IBARIKI NYAMONGO!

Ni kweli mkurya anaingia rama pit bila silaha..mbona sio taratibu na mila kutembea bila siraha hasa sehemu unayo jua kuna kupigwa risasi...
mbona husemi ni polisi wangapi wamepigwa mawe..na wake kuumizwa?
 
Kuna taarifa kutoka mkoani Mara kuwa polisi wamewauwa raia takribani tisa (9) na kuwarejeruhi wengine wengi waliokuwa wamevamia mgodi wa North Mara.

Inaniwia vigumu kuamini kuwa kikundi cha majambazi kinaweza kuwa na wanachama wanaozidi 20. Ujambazi ni mojawapo ya shughuli ambazo zinahitaji usiri wa hali ya juu ili kuwezesha mipango yao isiweze kugundulika na vyombo vya usalama kabla hawajatekeleza uharifu, unapokuwa na kundi la majambazi wapatao 800 unatakiwa kukaa chini na kutafakari kwa kina badala ya kuwaita majambazi.

Siungi mkono wananchi kujichukulia hatua mkononi katika kudai haki zao lakini katika matukio haya ya Tarime naona kama watu waliokata tamaa na serikali yao kuwatetea na badala yake wameamua kujichukulia hatua kudai haki yao kwa nguvu, huu siyo ujambazi na polisi inataka kuficha ukweli kuwa wameua watu waliokuwa wanaandamana kudai haki kwa kuwaita wavamizi.

Natoa wito kwa wabunge wanaotoka eneo hili kupeleka ombi la kuundwa kwa tume ya kuchunguza matukio haya na kuyapatia ufumbuzi wa haraka kabla hayajasambaa sehemu zingine ambapo wageni wananeemeshwa kwa rasilimali zetu huku wenye nazo wakitota kwa umasikini uliokithiri....

HUU SIYO UVAMIZI UNAOSTAHILI KUSHUGHULIKIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI, inahitajika busara na kutatua kero za watu hawa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa!
 
Hivi hii dhahabu na madini mengine ambayo tumepewa na mungu hatuwezi kuchimba wenyewe? Inauma sana
 
Hapa tatizo ni mikataba waliyoingia watawala Dar Es Salaam, ambapo hawakuwashirikisha wananchi wa maeneo husika, lazima hapa lawama ni kwa serikali kwani mara nyingi tunaona hata mikataba mingine inasainiwa nje kwa ajili ya kuwabana wananchi wa maeneo ya madini.

Kwa mtazamo wa kawaida unaweza ukawlaumu hawa jamaa lakini ukiangalia kwa makini utaona jamaa wanamantiki ya kuvamia maeneo hayo ili wajinufaishe moja kwa moja badala ya kusubiri mpaka wapate mgao kwa njia ya barabara au zahanati ambazo hazina uhakika wa kuwafikia.
 
Kweli tatizo ni serikali.

Serikali inawatisha wawekezaji kuwa bila CCM wawekezaji hawatakuwepo nchi hivyo wawekezaji wanasikiliza serikali inasema nini basi.

Pia Barrick nao wanakiburi kwakuwa wako karibu na serikali kuu kwani CSR yao inaanzia serikali kuu tu halafu wajuu wanawaamrisha watendaji wa chini....Hawa ripoti kwenye wilaya bali wanampigia waziri husika waziri anapiga simu kwenye wilaya kuwataarifu kuwa barrick wapo wilayani kwako...

Je, DC na wengine watajifikiriaje? Let them suffer for their bad behavior
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom