Fitina za Shigongo Hizi Hapa

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Huyu Shigongo ni mtu wa ajabu sana!

Kwanza amemuomba msamaha Jose Chamelione na kuahidi kutorudia u pumb avu alioufanya. Upande wa pili, kwenye gazeti lake la Uwazi ameandika habari yenye lugha chafu sana dhidi ya Jose Chameleone.

Mbaya zaidi katika makala bubu hiyo (haina jina la mwandishi) kama kawaida yake anawahusisha Watanzania wote kwa ujumla wao kuwa hawana umoja na wanaponzwa na umasikini.

Nilichogundua ni kuwa anataka kujenga bilateral conflict huku yeye akibakia salama kwa manufaa yake.

Angalia vyanzo hivi;

apolgy.jpg

Uganda Online - Shigongo Issues Apology to Chameleone Over Passport

HUU NDIYO UTAPELI KAMILI WA CHAMELEONE - Global Publishers

Sijui wenzangu mnamchukuliaje mtu huyu.
 
Nashukuru gazeti za huyu mfuasi wa magamba huwa sinunui wala ukinipa bure sisomi,amekazana kukopi na kupesti story kutoka kwenye novel za watu na amekalia kufutilia watu wakiwa faraghani.poleni mnaofuatilia newz za huyu ndugu.
 
Shigongo hawezi kutudanganya adanganye hao hao wasoma udaku kwenye magazeti yake ya udaku
 
Mkuu, sikitika kwanza kabla ya kumlaumu huyu bwana!

Mjasiliamali mzuri daima ni yule anayeweza kubaini gap kati ya kinachotakiwa na wanaokitaka na akitumia hiyo nafasi vizuri ananeemaka.

Shigongo alibaini ujinga wa ndugu zetu wengi kuwa wameathirika na mfumo mbovu wa elimu yetu na badala ya kutumia hiyo nafasi kuwasaidia akaamua kuitumia kwa kuwajaza ujinga zaidi. Na kinachotokea/kitakachotokea huko mbeleni ni ujinga kuongezeka kutokana na 'sumu' aliyotulisha.

Juzi Chameleon alipiga kambi ubalozi wa Tanzania nchini Uganda pale Kagera Road na hilo tukio lili-draw attention ya Waganda na uwezi jua ni wangapi wamejenga mtazamo hasi kuanzia hapo. Yote hayo sababu ya mtu mmoja kufanya mambo ya kipuuzi kwa makusudi mazima.

Ngoja tusubiri lakini historia inaweza kumkumbuka kwa kutumia 'ujinga' wa Watanzania kujitajirisha kama wanasiasa wengine badala ya kutoa mchango wa kuwaelimisha kwa kuwapa ufahamu.
 
mkuu, sikitika kwanza kabla ya kumlaumu huyu bwana!

Mjasiliamali mzuri daima ni yule anayeweza kubaini gap kati ya kinachotakiwa na wanaokitaka na akitumia hiyo nafasi vizuri ananeemaka.

Shigongo alibaini ujinga wa ndugu zetu wengi kuwa wameathirika na mfumo mbovu wa elimu yetu na badala ya kutumia hiyo nafasi kuwasaidia akaamua kuitumia kwa kuwajaza ujinga zaidi. Na kinachotokea/kitakachotokea huko mbeleni ni ujinga kuongezeka kutokana na 'sumu' aliyotulisha.

Juzi Chameleon alipiga kambi ubalozi wa Tanzania nchini Uganda pale Kagera Road na hilo tukio lili-draw attention ya Waganda na uwezi jua ni wangapi wamejenga mtazamo hasi kuanzia hapo. Yote hayo sababu ya mtu mmoja kufanya mambo ya kipuuzi kwa makusudi mazima.

Ngoja tusubiri lakini historia inaweza kumkumbuka kwa kutumia 'ujinga' wa Watanzania kujitajirisha kama wanasiasa wengine badala ya kutoa mchango wa kuwaelimisha kwa kuwapa ufahamu
Ntakugongea like later mkuu! Ukweli mtupu...
 
Nilishaacha long time kusoma udaku wa shigongo
anaweza kukuvunjia ndoa huyu
Wakati signature zake eti
"In god we trust" mmh
 
Hakuna cha ulokole yeye ana tutukana sisi wajinga kumbe yeye na magazeti yake ndio wa kwanza kuandika ujinga na udaku alaf anataka support kutoka kwa anao wavua nguo kila siku kupitia magazeti yake ya kidaku!

Ujinga wake na udaku umemponza kwanza ashukuru tumemsaidia.
 
jamani kumbe wenyewe ndio inawauma ivyo,waache na wenyewe kuwasema wenzao kwenye magazeti yao kama wanavyo lala mika ndio na wenzao inawauma wanavyo wekaga abali za uongo,kuwasema vitu vya uzushi.
 
Back
Top Bottom