Fiterawa ya Dr Rahabu

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,242
Jamani kwa wale mnaojua au mliowahi kutumia dawa ya huyu binti Dr Rahabu ambayo inasemekana kutibu vidonda vya tumbo. Ni kweli hii dawa inatibu?
 
Watanzania tunamatatizo mengi sana sector ya afya na ndio maana wananchi wanapoteza imani na hospital zetu. Na anapojitokeza mtu yeyote wa uongo kama akina Rehab,Ndodi na babu wa Loliondo watu wanakimbilia huko wakifikiri ni mwisho wa matatizo yao kumbe ndo wanaongeza matatizo na kwenda hospital amekwisha na sisi hatusiti kucertify na kutoa burial permit. Tanzania ni nchi ya kwanza Duniani kwa ushirikina refer mauji ya albino, vikongwe, uchunaji wa ngozi vikombe hii inadhihirisha huduma za jamii zilivyombaya kiasi kwamba watu wake hawatrust. Fikiri serikali inaajiri MA AMO na CO wakati MD wapo wanazurura mtaani haya ndo matokeo yake.
 
nasikia TFDA na mkemia mkuu wamekana kuithibitisha au kuitambua dawa hii!

Sasa kwa nini anaendelea kuhadaa katika vyombo vya habari. kapata hela kaenda hadi ulaya ndo anatumia picha hizo kuendelea kuhadaa watu!! Au ndo huyo mkemia anawaambia watu wamhame wenyewe watakapo prove dawa haina kitu.
Nina ushuhuda wa jamaa yangu wa karibu ambaye alikunywa na ilmrudi dawa hiyo karibu apoteze maisha - hakurudia tena kubebeshana na madumu ya hiyo "dawa"
 
Msinikumbushe Kovu..hawa matabibu feki niliwapita wote kipindi cha kumuuguza mama yangu mpendwa lakini aliishia kufariki.! SITAKI HATA KUWASIKIA! MATAPELI!
 
Mimi mwenyewe ni victim wa hiyo dawa kwani nimepoteza mda,pesa na nguvu zangu nyingi kinyume chake hakuna kitu na hata leo nina file la matibabu pale kwake...kiufupi Fiterawa ya R.Lubago haitibu urcers.
 
Msinikumbushe Kovu..hawa matabibu feki niliwapita wote kipindi cha kumuuguza mama yangu mpendwa lakini aliishia kufariki.! SITAKI HATA KUWASIKIA! MATAPELI!
pole sana mkuu!lakini inasikitisha zaidi kwa sisi wasomi tukiiamini hizi tiba feki!
 
Watanzania tunamatatizo mengi sana sector ya afya na ndio maana wananchi wanapoteza imani na hospital zetu. Na anapojitokeza mtu yeyote wa uongo kama akina Rehab,Ndodi na babu wa Loliondo watu wanakimbilia huko wakifikiri ni mwisho wa matatizo yao kumbe ndo wanaongeza matatizo na kwenda hospital amekwisha na sisi hatusiti kucertify na kutoa burial permit. Tanzania ni nchi ya kwanza Duniani kwa ushirikina refer mauji ya albino, vikongwe, uchunaji wa ngozi vikombe hii inadhihirisha huduma za jamii zilivyombaya kiasi kwamba watu wake hawatrust. Fikiri serikali inaajiri MA AMO na CO wakati MD wapo wanazurura mtaani haya ndo matokeo yake.
Kwa kuongezea hapa mkuu ni kwamba hata hao ma MD ni kanyaboya tupu siku hizi tuna maksi za kutokana na nyeti, vifaru, makombora na kizinga, manake mtaalamu nyeti kama huyu anakaririshwa theory badala ya vitendo zaidi. Ukienda kwenye clinical procedure siku hizi ni kuomba rushwa kwa wagonjwa tu wakati huo huo vifaa/ vitendea kazi unakuta ni OS hivyo hata kama unataka kufanya follow up management ya mgonjwa uliyekuwa assigned inakuwa vigumu.

Bila kusahau Lecturers wamekuwa wajasiriamali kutwa kucha wako kwenye miadhala ya kimataifa au semina na workshop za ndani ya nchi, ushauri wangu ni kuwa kila mtanzania ajitahidi kuwa na basic knowledge ya afya ya mwili wake kuliko kutegemea hospitali na maoni ya daktari pekee, wagonjwa wengi wanapoteza maisha kwa wrong treatment siku hizi na kwakuwa tunasema kuna kupona au kufa kwa mgonjwa tunashindwa kuhoji juu ya kifo kilivyotokea zaidi ya kusema ni kazi ya Mungu!
 
Kuna jamaa yangu alipona ivyo vidonda tena mtoa dawa anakupa na kukuambia ukipona ndo uje kulipa kama shukrani kwanza kwa mola then kwake!
Ukiona dawa yoyote inatangazwa sana ujue ina walakini
 
wa kuu kuna Mama mmoja yuko mara ana dawa ya vidonda vya tumbo na mtu anapona kabisa kuna watu wangu kama watatu wametumia na wamepona so kwa anae hitaji nitawapatieni namba zake
 
.........Kuna jamaa yangu alitumia hiyo dawa ya Rahabu kwa mwaka mzima aliishia kuharisha tu, hakupona wala nini. Labda inategemea na stage ya vidonda vya tumbo vya mtu. Lakini sasa yupo poa baada ya kunywa vidonge alivyopewa hospital.
 
mimi nilidhani ni madawa ya kusafisha tumbo kutoka kwa wamasai ndio hufanya hivyo,kumbe hata ukinywa fiterawa inabidi usikae mbali na uani!!!!
 
wa kuu kuna Mama mmoja yuko mara ana dawa ya vidonda vya tumbo na mtu anapona kabisa kuna watu wangu kama watatu wametumia na wamepona so kwa anae hitaji nitawapatieni namba zake
Tupatie namba mkuu. Hiyo dawa ya dada Rahabu inayoitwa fiterawa ni wizi mtupu. Watu wanainywa na kuharisha sana lakini hawaoni mabadiliko ya maana. Badala yake yeye mwenye hiyo dawa anaendelea kunawili siku hadi siku kwa fedha za wagongwa. Siku hizi hata 'ttako' limeongezeka.
 
Huyu Dada first time nilipomuona alionekana mdada mchovu chovu ila kwa sasa anang'aa dah kama ni utaperi basi hii ndio Bongo kuishi kwa ubongo
 
Back
Top Bottom