Fisi ni fisi tu

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Demu mmoja wa kusoma alimwona kijana mmoja mzuri sana katika kituo cha daladala. Yule binti bila kuvunga akaamua kumfuata yule kaka ili amweleze hisia zake, “…wewe kaka ni mzuri, nimekupenda ghafla…”

Jamaa akiwa katika taharuki iliyoambatana na mshangao mkubwa sana alijikuta akimstaajabia binti huyu aliyeonekana kuyachokoza mapenzi wakati usio wake! Huku akimshika mabegani alimsihi yule binti kwa maneno ya busara, “mdogo wangu, mapenzi na tamaa ya mwili vyote ni ubatili tu. Wewe bado mdogo sana kuyafanya haya uliyonifanyia. Nenda nyumbani tafadhari, usome kwa bidii kwa ajili ya mafanikio yako ya baadaye.”

Kisha jamaa akachana kijikaratasi na kumpa yule binti huku akimwambia, “humu nimekuandikia mafungu kadhaa ya Biblia, kabla ya kulala leo hii yasome na utashinda yote!

Yule bintiakaondoka kwa mfadhaiko mkubwa sana maana alihisi kadharirika sana. Alipofika bwenini, wakati anataka kulala akakumbuka lile fungu alilopewa na yule kijana. Ndipo alipokitafuta kile kijikaratasi na kukisoma. Baada ya kukifungua alikutana na maneno haya, “wewe huoni nini? Wakati unaongea yote yale hukumwona mke wangu alikuwa nyuma yangu? Anyway, hii hapa namba yangu! Nitext nitakupigia any time.”
 
Jamaa super striker aisei..! Bila shaka alitumia akili yangu..
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom