Fisadi wa Rada, Tanil Somaiya afanya kufuru IKULU

1. hakuna aliyehukumiwa kwenye kesi hii hivyo wote bado ni innocent

2. Issue ya kuingiza gari geti la mbele au nyuma ni kazi za walinzi au watu wa protocal hivyo ni non issue

3. Tangu lini ikulu ikawa ya Nyerere? Ikulu ni ya waTanzania wote au ushasahau kama nyerer naye alikuwa na secretary wake ambaye alikuwa CIA kwenye hiyo hiyo ikulu yetu?

4. Wikileaks doc...hosea mwenyewe anasema tatizo sio watu kupewa kamisheni ya 30% bali je ni halali?

5. Dont hate the player, hate the game...considering huyo Hosea naye ana kashfa za kifisadi pia
 
Dont hate the player, hate the game...considering huyo Hosea naye ana kashfa za kifisadi pia

Comment kama hizi huwa zinaninyima raha kabisa......(and I always ask myself ni wangapi tuliobaki wenye uchungu na hii nchi) kwahiyo kama Hosea ana kashfa so its okay kwa wengine kuwa na kashfa????? au kuwa na kashfa kwa hosea inajustify huu upuuzi........ brother "Two wrongs dont make a right"

And what kind of a game is being played???? am sure wananchi are nor part of this game... they are just on the loosing end
 
Kishongo prove innocence ya mkwere usikurupuke eti habari ya kutungwa tueleze ilikuwaje siku hiyo nani alikuwa wa kwanza kuingia na nani alikuwa wa mwisho kuingia maana inaelekea unajua tusilolijua. Huu ubumbavu utaisha lini??????Mkwere miaka mitano sio mingi ni kama mvua za vuli utashangaa fumba na kufumbua tupo wote kijiweni hahahah... huku Weakleaks akiendelea kufanya mambo yake.Kweli utakuja kushangaa mbuzi kuvaa kanga imeandikwa chama cha majangili ziiiiiiiiiiiiiiii!!!
 
Wakati vodacom imesaidia kampeini vodacom na shivacom ni kama makalio ya sufuria na moto,RA+Somaia=ccm+state house!!mnachoshangaa nini??nisawa mfuko wakoti wa nje na wandani kwa koti moja!.
 
Ilikuwa ni siku ya Desemba 9, 2010. Tanzania ilikuwa inasherekea miaka 49 ya Uhuru wa taifa. Baada ya kukagua gwaride Uwanja wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete alifanya dhifa ya kitaifa Ikulu na kualika viongozi wa serikali, mabalozi, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakuu.

Waalikwa wote, walikuwa wanaingia Ikulu kupitia mlango wa nyuma ulio karibu na bahari upande wa ferry. Lango kuu la kuingia Ikulu lilikuwa halitumiki kwa wageni siku hiyo na lilitumiwa na Rais na viongozi wengine wakuu. Magari yote, ikiwemo ya mawaziri na mabalozi yalipaki nje ya Ikulu kwenye uwanja mkubwa ulio karibu na ferry na wageni waalikwa waliingia kwa mguu kwenye viwanja vya Ikulu.

Mmoja wa wageni waalikwa mashuhuri wa Kikwete alikuwa ni Tanil Somaiya, mmiliki wa Shivacom Group of Companies.

Wakati mawaziri na mabalozi waliambiwa na maafisa usalama Ikulu watumie mlango wa nyuma wa kuingia Ikulu na kutembea mpaka kwenye gardens ambako sherehe ilifanyika, Tanil alipewa heshima ya kipekee na kuruhusiwa kutumia main entrance gate.

Tanil aliingia Ikulu na gari la kifahari jekundu (a red FERRARI) na kuipaki gari hiyo kwenye mlango mkuu wa kuingia IKULU ampako huwa gari la Rais ndipo linapaki.

Aliiacha FERRARI hiyo hapo kwenye lango la kuingia Ikulu kwa zaidi ya masaa mawili huku akijimwaga kwenye dhifa.

Mawaziri, mabalozi na vigogo wengine walibaki wamepigwa na butwaa iwaje wageni wote waambiwe waingie Ikulu kupitia mlango wa nyuma kwa mguu na kuacha magari yao nje halafu mfanyabiashara huyu apite main gate na kuweka gari lake kwenye main entrance ya lango kuu la kuingia Ikulu.

Tanil ni rafiki wa karibu na business partner wa Shailesh Vithlani, mfanyabiashara ambaye amekimbia nchi kutokana na kashfa ya rada.

Tanil, ambaye ametajwa kwenye WikiLeaks kuhusu rada, amehusishwa pamoja na Vithlani kwenye kashfa ya rada, military trucks, military choppers, Gulfstream presidential jet na scandal nyingine.

Inaeleweka kuwa Tanil alimchangia pesa nyingi sana Kikwete kwenye uchaguzi wa Rais uliopita na pia alitoa helikopta zake zitumike kwenye kampeni ya CCM, lakini hii ndivyo Ikulu ya Mwalimu Julius Nyerere inavyodharauliwa siku hizi?

Kwa kutumia main entrance na kupaki gari lake mbele ya lango kuu la Ikulu, Tanil alikuwa anataka kuwaonesha wageni wote kuwa yeye yuko karibu sana na Rais wa nchi na Ikulu ni kama nyumbani kwake.

Mbaya zaidi, kufuru hii ilifanywa siku ambayo Tanzania inaadhimisha uhuru wake. Kuna uhuru kamili kweli kama watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wanafanya kufuru namna hii mpaka IKULU?

Unatarajia kweli Edward Hoseah wa PCCB anaweza kuondokana na uoga wa kumkamata Tanil kwa ufisadi wa rada wakati Rais wa nchi ni besti wake na Ikulu ni kama playground yake?
Mkuu,

Tumeifahamu mada ila umeitowa ladha kidogo kwa kusahau kuingiza hizi sentensi.

Tusilisahau jina la nchi yetu, jamani.

Tanzania ilikuwa inasherehekea uhuru wa lililokuwa taifa la Tanganyika.

Tanzania ilikuwa inaadhimisha uhuru wa Tanganyika

Kama huyu mdosi kuna siku anavaa nguo za kijani na manjano basi anahaki ya ku-park popote. Mkuu, yeye si katika sisi,yeye ni katika wao.
 
1. hakuna aliyehukumiwa kwenye kesi hii hivyo wote bado ni innocent

2. Issue ya kuingiza gari geti la mbele au nyuma ni kazi za walinzi au watu wa protocal hivyo ni non issue

3. Tangu lini ikulu ikawa ya Nyerere? Ikulu ni ya waTanzania wote au ushasahau kama nyerer naye alikuwa na secretary wake ambaye alikuwa CIA kwenye hiyo hiyo ikulu yetu?

4. Wikileaks doc...hosea mwenyewe anasema tatizo sio watu kupewa kamisheni ya 30% bali je ni halali?

5. Dont hate the player, hate the game...considering huyo Hosea naye ana kashfa za kifisadi pia

Wakati wengine wamechangia pointi nyingine mimi nataka kuchangia namba mbili. What do you mean by saying its "non issue"? Unataka kutuambia kuwa hawa jamaa wa protocal walitoa maagizo kuwa wageni wengine wote wapaki nje ila huyo mmoja tu ndiyo apaki ndani pasipo kuhisi au kufahamu kuwa kuna uhusiano usio wa kawaida wa uongozi wa juu?? Nataka nikukumbushe tu kuwa watu wa protocal hawafanyi vitu vya kubahatisha. Unadhani mlinzi wa ikulu anaweza kuwa amepewa maagizo asiruhusu gari kuingilia mlango mkuu halafu akaidi na kufungulia mgeni mmoja tu?? Na awe huyo? Tafadhali tafakari mambo vizuri zaidi. Sijapata hata kunusa ndani ya hilo eneo mimi mtoto wa mkulima wa jembe la mkono, lakini hakuna hata picha iliyopigwa siku hiyo inayoweza kuonyesha hata sehemu tu ya hiyo Ferarri?? hata iliyopigwa kwa simu jamani?? Hebu jaribuni kutafuta picha nyingi za hiyo sherehe huenda mahali linaonekana ili ubishi uishe.
 
Comment kama hizi huwa zinaninyima raha kabisa......(and I always ask myself ni wangapi tuliobaki wenye uchungu na hii nchi) kwahiyo kama Hosea ana kashfa so its okay kwa wengine kuwa na kashfa????? au kuwa na kashfa kwa hosea inajustify huu upuuzi........ brother "Two wrongs dont make a right"

And what kind of a game is being played???? am sure wananchi are nor part of this game... they are just on the loosing end
Ukiona comments kama hizo ujue mtoto wa fisadi yuko kazini.
 
Je wewe ulikuwepo??? Au wee ndio ulikuwa zamu ya ulinzi siku hiyo??? Hata hivyo mwandishi nawe wa story hii kiasi fulani unatia wasiwasi, iweje toka siku ya Uhuru tarehe 9/Dec, hadi hii leo ndio unaitoa hii story, kweli ???? Siku zote hizo ulikuwa wapi????? Unatia wasiwasi!!

Kibopa aliyehudhuria tafrija ya uhuru wa Tanganyika alikuwa nje ya nchi. Nilikutana naye jana ndio akananipa taarifa hizi kwa uchungu mkubwa. Yeye anamfahamu vizuri Tanil na anaijua Ferrari yake ndio maana ikawa rahisi kwake kushuhudia tukio hili la kihistoria. In fact, Tanil ndiyo tajiri pekee mwenye Ferrari hapa Dar es Salaam. The shiny red car was very conspicuous pale mbele ya Ikulu. Lakini kwa mtu wa kawaida, tena ambaye hana interest na magari inaweza kuwa ni vigumu kwake ku-notice mambo kama haya. Nina hakika kuwa cctv image za Ikulu na huenda hata footage za tv kama TBC, ITV, Chanel Ten, Star TV, na Mlimani TV wanaweza kuwa walipata picha za gari hili jekundu mbele ya lango la Ikulu. Kibopa huyo kaniambia kuwa Tanil huwa anatamba kwa wahindi wenzake kuwa Rais ni rafiki wake wa karibu. "The president once asked me to give one of his girlfriends from South Africa a ride on my yatch," alisikika Tanil akitamba kwa watu. Tanil anasema kuwa yuko in regular contact with the president. Huwa anawasiliana na mkuu wa nchi kwa simu na sms kila mara. Hata walinzi wa Ikulu wanamfahamu sana ndiyo maana alipoingia na red Ferrari yake walibaki kumpungia mkono tu na kumruhusu apaki mbele ya lango kuu la Ikulu. Kwa ufupi, Ikulu ya nchi is his little playground.
 
Kishongo inaelekea wewe receptionist Ikulu, kama si hivyo unaishi kwa salma, haya tupe facts tukuamini.
 
Sikio la Kufa halisii dawa.
Tangu awamu ya kwanza, kikwete hakuwahi kuwa na dhamira ya dhati, ya kutumia umma wa watanzania,
ni mtu anayependa sifa za kijinga hasa zinazoambatana na ukuu wa uongozi.

Kwa taarifa action kama hii kwa kikwete ni furaha sana kwamba amezungukwa na wafanyabiashara,
huyu mkwere ni masikini sana wa mawazo na mali, He is not a presential materal

Tunalo hili
 
wana Jf ninaumia moyo kuona habari kama hizi,naumia to the point where i have got no words to express myself,najuta kuwa mtanzania,najuta,au wamemloga rais wetu awe kilaza ivo ndugu zangu,wale wakali wa mambo hayo mfungueni macho rais wetu,inasikitisha sana.
 
Hiyo kweli ni noma sisi hatuna Rais hata kidogo bali tuna genge la mafisadi ndio wanaongoza nchi na kuamua nani awe kiongozi, Lakini hao wote mwisho wake umefika tuiunge mkono CDM maana watakimbia inchi Dr. Slaa au mbowe akiingia madarakani.

Peoples Power
 
Nafuu Baba wa taifa JK Nyerere alijifia, sijui angefanyeje kuona sehemu takatifu kama ile ikichezewa na MAFISADI KAMA SOMAIYA. ........ NADHANI HATA SASA ANGEPEWA NAFASI YA KUFUFUKA NA KUSHUHUDIA MAMBO YANAYO FANYIKA, ANGESEMA BORA AENDELEE KUPUMZIKA KUZIMU.

HALAFU MOD KUFUTA POSTI ZA WENZAKO BILA KUTOA SABABU SI UUNGWANA. UMEZOEA SANA KUFUTA MICHANGO YANGU BILA KUTAJA SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA HIVYO.
jamani hivi ikulu inautakatifu gani?? acheni kufuru bwana.
 
nadhani wakati wa kulalamika umekwisha sasa sisi kama wananchi lazima tuchukue hatua kama nikueneza elimu ya uzalendo kwa watu waliokaribu na sisi ,ukitoa mifano ya jinsi mafedhuli walivyo na nguvu nchi hii wanaweza wakaamua nani awekwe madarakani ,nani atoke ,kupitishwa mbele na kinyume cha utaratibu uliowekwa kwa wanadiplomasia hii taabu sana hata kumeza,inauma lakini roho yangu inaniambia tuta vuk siku moja na watalia na kusaga meno

Mimi naamini nimeandika mara nyingi kuwa mbegu haioti mpaka kwanza ife; na nchi yetu vile vile haiwezi kujikomboa kutoka kwa makucha ya hawa mafedhuli mpaka watu wamejitoa mhanga!! Haya makerere tunayopiga hayawakoseshi usingizi kama wenyewe wanavyosema; tunahitaji watu wenye uchungu na nchi yao ambao wako radhi kujitolea kwa niaba ya vizazi vijavyo kama wakina Mkwawa walivyowakomalia wajerumani!!
 
Kibopa aliyehudhuria tafrija ya uhuru wa Tanganyika alikuwa nje ya nchi. Nilikutana naye jana ndio akananipa taarifa hizi kwa uchungu mkubwa. Yeye anamfahamu vizuri Tanil na anaijua Ferrari yake ndio maana ikawa rahisi kwake kushuhudia tukio hili la kihistoria. In fact, Tanil ndiyo tajiri pekee mwenye Ferrari hapa Dar es Salaam. The shiny red car was very conspicuous pale mbele ya Ikulu. Lakini kwa mtu wa kawaida, tena ambaye hana interest na magari inaweza kuwa ni vigumu kwake ku-notice mambo kama haya. Nina hakika kuwa cctv image za Ikulu na huenda hata footage za tv kama TBC, ITV, Chanel Ten, Star TV, na Mlimani TV wanaweza kuwa walipata picha za gari hili jekundu mbele ya lango la Ikulu. Kibopa huyo kaniambia kuwa Tanil huwa anatamba kwa wahindi wenzake kuwa Rais ni rafiki wake wa karibu. "The president once asked me to give one of his girlfriends from South Africa a ride on my yatch," alisikika Tanil akitamba kwa watu. Tanil anasema kuwa yuko in regular contact with the president. Huwa anawasiliana na mkuu wa nchi kwa simu na sms kila mara. Hata walinzi wa Ikulu wanamfahamu sana ndiyo maana alipoingia na red Ferrari yake walibaki kumpungia mkono tu na kumruhusu apaki mbele ya lango kuu la Ikulu. Kwa ufupi, Ikulu ya nchi is his little playground.

Mkuu Fareed,

Usitumie nguvu nyingi sana kuelezea uwepo wa "gari nyekundu" lango kuu la ikulu!

Ni asilimia ndogo sana ya wale waliokuwepo kwenye "dhifa" walikuwa "interested" na hiyo "gari nyekundu" - To many of them it was "business as usual" - hakuna aliyejiuliza ni kwanini "wao" wameacha magari nje na kutembea kwa miguu mpaka kwenye gardens za ikulu?

Kitu ambacho "probably" kiliweza ku-attract attention ya baadhi yao ni ile "gari nyekundu" kufika imechelewa saana na pengine wenye ukabila kama mimi kuona anayetelemka ni "mdosi"!

The hard fact is - Tanil ndiye mgeni pekee mualikwa aliyeingia Geti Kuu la Ikulu na "Gari Nyekundu" na kuiegesha kwenye maegesho rasmi ya VIP! Wengi walichukulia kirahisi sana swala hili, but there one thing that we have to ponder - Why Tanil is/was so special to the point of "driving in" into the state house?

Nimetumia neno "Gari Nyekundu" kwa maana ya kuwa angalau kila mtu aliyeudhuria "dhifa" ile rangi ya gari ilikuwa inaonekana "visibly"!
 
Kibopa aliyehudhuria tafrija ya uhuru wa Tanganyika alikuwa nje ya nchi. Nilikutana naye jana ndio akananipa taarifa hizi kwa uchungu mkubwa. Yeye anamfahamu vizuri Tanil na anaijua Ferrari yake ndio maana ikawa rahisi kwake kushuhudia tukio hili la kihistoria. In fact, Tanil ndiyo tajiri pekee mwenye Ferrari hapa Dar es Salaam. The shiny red car was very conspicuous pale mbele ya Ikulu. Lakini kwa mtu wa kawaida, tena ambaye hana interest na magari inaweza kuwa ni vigumu kwake ku-notice mambo kama haya. Nina hakika kuwa cctv image za Ikulu na huenda hata footage za tv kama TBC, ITV, Chanel Ten, Star TV, na Mlimani TV wanaweza kuwa walipata picha za gari hili jekundu mbele ya lango la Ikulu. Kibopa huyo kaniambia kuwa Tanil huwa anatamba kwa wahindi wenzake kuwa Rais ni rafiki wake wa karibu. "The president once asked me to give one of his girlfriends from South Africa a ride on my yatch," alisikika Tanil akitamba kwa watu. Tanil anasema kuwa yuko in regular contact with the president. Huwa anawasiliana na mkuu wa nchi kwa simu na sms kila mara. Hata walinzi wa Ikulu wanamfahamu sana ndiyo maana alipoingia na red Ferrari yake walibaki kumpungia mkono tu na kumruhusu apaki mbele ya lango kuu la Ikulu. Kwa ufupi, Ikulu ya nchi is his little playground.
nimeanzaje kusoma hapa napata hasira sana mimi! HALAFU EEETI WENGINE WANAPAITA PATAKATIFU ALAAAAAAAAAAAA!
 
jakaya kikwete uku kwetu wanamwita kubwa jinga...
kifupi kapoteza heshima yake, hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba 10

ivi nyie si ndo juzi tuu mmempigia kura?? watz bwana au mshasahau wakati hata miezi minne haijaisha tangu uchaguzi na mkamchagua huyo huyo kubwa jinga....ahahahahah na mtajibeba mwaka huu na huyo raisi wenu..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom