Fisadi na Kiziwi

Bukayo jr

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
2,782
1,638
[h=6]Fisadi mmoja katili sana alikuwa kamuajiri mhasibu bubu, kiziwi. Alifanya hivyo ili kulinda siri za mapato yake. Siku moja akagundua kuwa kuna kama shilingi milioni mia moja zimeibiwa. Akajaribu kumuuliza mhasibu wakawa hawaelewani, akamtafuta mkalimani ambaye anafahamu lugha ya alama amuulize muhasibu pesa hizo ziko wapi...

Mtaalamu akamuuliza mhasibu fedha zi wapi,
Mhasibu akarudisha jibu kuwa hajui....

Fisadi akamwambia mkalimani,
‘Mwambie asiponiambia nampiga risasi sasa hivi...’

Mkalimani alifikisha ujumbe, Mhasibu aliposikia hivyo akajieleza,
’Pesa ziko kwenye mfuko wa plastiki nimezifukia nyuma ya nyumba yangu chini ya pipa la maji...’

Mkalimani akamgeukia bosi na kumwambia,
‘Mhasibu wako kasema wewe mwoga, tena **** kabisa, huna jeuri ya kufyatua risasi na wala humbabaishi kwa lolote, kama unaweza fanya unavyotaka!!!!’

[/h]
 
Mkalimani nimemwacha anatoa hela kwenye pipa sasa hivi naelekea kwenye mazishi ya mhasibu nikimaliza kumzika mhasibu nakwenda moja kwa moja gerezani kumtembelea fisadi
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom