WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
- Thread starter
- #21
Good to learn abt the history of FLs of USA.
Back to our own situation.Ukiacha Nyerere, marais waliofuatia sidhani walikuwa na " "ambition" au ndoto ya kuja kunyakua nafasi ya juu kupita zote katika uongozi wa taifa la Tanzania, kiasi kwamba "wajiandae" kuwapata wenzi watakaoweza kwenda sambamba na majukumu yaliyoko ikulu.Mkuu wa sasa kweli alikuwa na muda lakini inaelekea maandalizi yake hayakuhusisha pia kumwandaa FL.Utakumbuka kwa mfano Hillary Clinton na hata akina Nancy Regan walikuwa na usemi sana katika shughuli wafanyazo waume zao ikiwa ni mpaka hata kupitia hotuba zao na kuweka sawa.Ukija huku Africa, hasa Africa Magaribi baadhi ya wake wa marais kama Mrs Dr.Maryam Babangida, Madam Nana Rawlings na wengine waliweza kuwa na mvuto na hata kufanya waliyoweza kuyafanya ( hata kama hayakubaliki sana na wengi) kwa vile walikuwa na kisomo na hata hao waume zao walilijua hilo na kuwaaminisha wafanye.
Tukija huku Tz, wengi wa wale waliokuja kuchukua uongozi, tayari walishajipatia wenzi wao wa maisha ambao si ajabu walijikuta tu wanalazimika kufanya u FL bila hata maandalizi yoyote.Ningetegemea Serikali yetu na hasa Wizara za Mambo ya nje wakishirikiana na Wizara ya Wanawake wangeona umuhimu wa kutengeneza induction programme ya kuwasaidia wamama wa kwanza kwa kila hali - kuanzia kuwapa msasa wa mambo ya kidiplomasia, uendeshaji wa ikulu kama makazi rasmi ya rais, na stadi nyingine ikiwa ni pamoja na public speaking na hata kuongeza elimu.

Last edited: