Filikunjombe: wabunge wa CCM waoga wanajipendekeza kwa chama badala kwa wananchi

Source Mtanzania

Mh mbunge Filikunjombe kawachana wabunge wa CCM na kuwaita waoga na wanafiki kwa kuogopa chama zaidi kuliko wananchi walio watuma bungeni.

Hayo yamejiri baada ya wabunge hao kuwa waoga kutia saini ya kutokuwa na imani na waziri mkuu pinda na kukaa kuzungumzia mambo hayo chini chini.

Mbaya zaidi wamekuwa wabunge wa kujipendekeza kwa chama na viongozi wake na kuwatupa wananchi wao.

My take

Sishangai ndo maana hata JK kashindwa kuvunja baraza hadi apate idhini ya chama

Njiwa mwema haruki na kunguru, shuka kwenye TITANIC (CCM) upande SAFINA (CDM). Fanya haraka bado unayo nafasi.
 
Source Mtanzania

Mh mbunge Filikunjombe kawachana wabunge wa CCM na kuwaita waoga na wanafiki kwa kuogopa chama zaidi kuliko wananchi walio watuma bungeni.

Hayo yamejiri baada ya wabunge hao kuwa waoga kutia saini ya kutokuwa na imani na waziri mkuu pinda na kukaa kuzungumzia mambo hayo chini chini.

Mbaya zaidi wamekuwa wabunge wa kujipendekeza kwa chama na viongozi wake na kuwatupa wananchi wao.

My take

Sishangai ndo maana hata JK kashindwa kuvunja baraza hadi apate idhini ya chama

Mwalimu alishasema ccm isipokuwa imara nchi itateleka na inabidi wajue ccm sio baba yao wala mama yao
 
Ukiona watu wenye akili timamu tena Watanzania wanashabikia uchafu unaofanywa na serikali ya CCM..
Ukiona wabunge wa CCM wakitetea chama chao kwa wizi na rushwa....
Ukiona Mawaziri wanajitetea bungeni wengine hawana taarifa, wengine manaibu wezi....
Ukiona Waziri Mkuu anaongelea Simba badala ya adha za Watanzania na Matatizo yao ya msingi...

Ujue hapo Hakuna serikali...
Ujue hapo Hakuna Bunge...
Ujue hapo Hakuna Jeshi.....

Na mwisho wake ni nini????
 
Mimi siwezi mwamini muovu akiwa kwa shwetani hata akiwa na mazuri kiasi gani namshauri mh deo akate shuri na ijiunge na jeshi la ukombozi ;hapo tutajua kweli ni mpambanaji.angalia akina lembeli na yule mama wa same.
 
Endelea kumkubali kwakuwa safari yake ya kuhamia cdm imeanza siku ile aliyoweka siignature kwenye karatasi ya zitto. uchaguzi ujao magamba watamshibuda tu. kama hawatasema ana uraia wa botswana na hajaukana watasema utotoni aliugua degedege hivyo hafai kumbea. ndio hapo ss atakapohamia cdm
hapo kwenye DEGEDEGE umenitatiza
 
Mimi siwezi mwamini muovu akiwa kwa shwetani hata akiwa na mazuri kiasi gani namshauri mh deo akate shuri na ijiunge na jeshi la ukombozi ;hapo tutajua kweli ni mpambanaji.angalia akina lembeli na yule mama wa same.
Mkuu jeshi la ukombozi halilipwi posho. Kataeni kuchukua posho kwanza.
 
ameamua kuongea na kusema mawazo yake kuliko wengine walioko ccm kama yeye na bado wanafungwa kuongea mawazo ya chama hata kama ni mabaya badala yakuongea mawazo yao.
 
3.jpg

8.jpg
 
Candid mbona hii thread ilishakuwemo?labda ulichozidisha wewe ni kuweka na picha/bandiko la gazeti. Ni kweli ni waoga hawana maana kabisa! wanafiki mno!
 
Utetezi wa William Malechela kwamba asingetia sahihi angekuwa mbunge rasimu ya Zito kutokuwa na imani na serikali inajenga mazingira wazi ya woga kwa wanachama na viongozi wa CCM kuogopa rungu la chama kulindanda.

Kauli ya mbunge Kingwangala wa Nzega inaweka bayana kauli ya Filikunjombe kwamba Wabunge wa CCM ni waoga. Kwani wengi hawakutegemea Kingwangala alivyomtetezi wa wananchi awe kinyume cha rasimu ya Zito eti kwa ajili ya uwajibikaji wake chamani.
 
Candid mbona hii thread ilishakuwemo?labda ulichozidisha wewe ni kuweka na picha/bandiko la gazeti. Ni kweli ni waoga hawana maana kabisa! wanafiki mno!

Nimeleta uthibitisho wa mada ile, nimeshindwa kuipata haraka mada ile, Mod ataiunganisha. Asante.
 
kulikua na haja gani ya kuweka hilo li picha jeusi lilioungua?? si ungeweka source tuwatu tungetafuta?? ama unge andika ulichokielewa?? ndo nini sasa hii?
 
kulikua na haja gani ya kuweka hilo li picha jeusi lilioungua?? si ungeweka source tuwatu tungetafuta?? ama unge andika ulichokielewa?? ndo nini sasa hii?

Pole sana ndugu yangu, hapa ni jungu kuu, yahitaji kuwa mvumilivu, unaloona we ni taka wengine wanaona ni source nzuri ya habari ambayo inakubalika hata kuwa kielelezo mahamanai. Link huwa si wote wenye nafasi ya kusoma wengine hutumia simu ambazo hazina memory kubwa, bora tusaidiane kila mmoja apate kile anachotegemea.
 
Mko Lituhi au Litembo?
 
Back
Top Bottom