Filikunjombe: Sikwenda Kigoma kumsafishia yeyote njia

Mh. Mh. Deo Filikunjombe amestushwa sana na swala la yeye kumsafishia Zitto njia ya Urais. 'Hayo ya Zitto ni ya kupikwa, something wrong somewhere" Anashangaa kwa nini kawekewa maneno mdomoni ambayo namna au nyingine imemdhalilisha kwa wapiga kura wake na kuonekana kama kibaraka fulani?

Atazungumza na waandishi wa Habari/atatoa tamko lake hivi karibuni. Mh. Jembe Mh. Deo Filikunjombe anasema kwamba ametumwa na watu wake kuwawakilisha na siyo kuzungumzia mambo yasiyo na msingi tena ya kuropokwa.hakwenda kigoma mumsafishia yeyote njia... Stay tuned.

source mshirika wa Mheshimiwa

**** **** ****.......kutumia jina la wananchi mambo yanapokuwa yamekaa tenge.....kama katumwa kuwawakilisha wananchi huko kigoma kulikuwa na maslahi kuliko kubaki bungeni kwenye budget ambayo inatoa mustakabali wa Taifa?????

Mwambie akiita waandishi alete na ushahidi wa kimazingira as well
 
By Ester Bulaya

Nasikitika sana kuambiwa kuwa nimempigia debe urais Mh Zitto Kabwe. huu ni uwongo wa kutubwa tulienda kigoma kuwaunga mkono wasanii wa kigoma walioamuwa kwenda kUchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha vijana. nilienda kama mbunge wa vijana kwa ajili ya kuunga mkono vijana wenzangu. huu ni uzushi mkubwa. natambua kila chama kinautaratibu wa kupata mgombea urahisi.

Tusubiri video sasa.
 
Mh. Mh. Deo Filikunjombe amestushwa sana na swala la yeye kumsafishia Zitto njia ya Urais. 'Hayo ya Zitto ni ya kupikwa, something wrong somewhere" Anashangaa kwa nini kawekewa maneno mdomoni ambayo namna au nyingine imemdhalilisha kwa wapiga kura wake na kuonekana kama kibaraka fulani?

Atazungumza na waandishi wa Habari/atatoa tamko lake hivi karibuni. Mh. Jembe Mh. Deo Filikunjombe anasema kwamba ametumwa na watu wake kuwawakilisha na siyo kuzungumzia mambo yasiyo na msingi tena ya kuropokwa.hakwenda kigoma mumsafishia yeyote njia... Stay tuned.

source mshirika wa Mheshimiwa

Siwezi na nivigumu kwangu kuamini kuwa Zito ni mnafiki siwezi kuunga mkono suala hilo lakini pia siwezi kutetea hadi mwenyewe aseme nashauri aweke msimamo wake watu wauelewe. Wanafiki wengi wamekufa kisiasa na heshima yao imepotea kabisa katika jamii. Unafiki ni dhambi mbaya sana hasa unapowayumbisha watu wenye shida na dhiki waliokutuma uwatetee halafu uwe unafuatilia mambo yako kwa masilahi yako. Urais ni mzuri ukiungwa mkono na waliokuchagua ukiukimbilia utatamani kuukimbia angalia maraisi maalufu kama Gadafi, Hosen Mubarack, Mobutu na wengine wengi sana waliouona uichungu wa urais.

Najua kuwa urais ni haki ya kila mtu lakini ni vizuri kama ukipiganiwa kwa haki bila kuathili nguvu ya chama ambacho ndo mkombozi wa watu waliowengi. CCM, CUF zimefikia hapo kwasababu ya kupigania urais nadhani hali kama hiyo haitakiwi kufika kwetu.
 
Ningekuwa mimi ni yeyote kati ya waliotajwa kwa majina ningelipeleka hili suala mahakamani ili muache kuongea ongea...na suala la urais ningelipeleka mahakamani....suala la Pension peleka mahakamani, safari za rais peleka mahakamani (hakuna kuzi hoji hoji), yaani sasa hivi ni mahakamani tu.
 
Kidemokrasia Zitto ni positive change Tanzania. Anahamasisha vijana kuwa huru katika kuenjoy haki zao za kikatiba. Sijaona mahali Zitto akikataza watu kuexercise their freedom. Zitto anatuma ujumbe kwa wapenda demokrasia kuwa CHADEMA haina de facto mgombea wa urais na mgombea atapatikana baada ya mchakato maalum unaoheshimu katiba ya chama. Asiyekubali hilo ndio "hatari kwa mstakabali wa taifa letu kidemokrasia!".

Mtu ambaye hajui aseme nini, wakati gani, katika jamii gani, n.k. huyo siyo kiongozi, hafai. Kama utaenda kwenye mkusanyiko wa maziko ya marehemu, na wewe ukaanza kutangaza sherehe za tamasha la vijana, lazima wewe tukuone mwehu, ndivyo ambavyo Zitto anavyofanya. Demokrasia na uhuru haimaanishi kusema chochote, wakati wowote, kwa mtu yeyote. Ukifanya hivyo hutakuwa umevunja sheria lakini jamii lazima ikuone kuwa hupo sawasawa.
 
Tusubiri video sasa.

Hata mahakamani, kinachoangaliwa ni ushahidi. Ushahidi tumekwishaupata, wote wanne wamesema kuwa gazeti la mwananchi limeongopa. Tunataka ushahidi gani tena? Afadhali kama ingekuwa wawili wamesema kuwa walisema, wawili wanasema hawakusema, hapo tungeihitaji hiyo video ili tujue katika hawa wanne, ni nani anasema ukweli na nani mwongo. Sasa wote wanne wanasema hawakusema, tunahitaji tu ushahidi mwingine zaidi ya hizi kauli za waliotajwa?
 
Heehe kwa sasa hawezi kupingana na hao watu wanne akabadili upepo

Kwanza maelezo ya Zitto mwenyewe alionesha kuwa alikuwa anatudanganya.

Alisema kuwa yeye hakumualika mwanahabari yeyote.

Anasema kuwa yeye hakuwa mwandaaji wa huo mkusanyiko bali na yeye alikuwa mualikwa kama walivyoalikwa wengine.

Anasema kuwa wabunge waliohudhuria walialikwa na waandaaji na siyo yeye.

Wakati huo huo anasema ana video, cha kujiuliza kama wewe ni mgeni mwalikwa utafika kwenye sherehe ya watu ukaanza tu kuchukua picha za video? Anadai kuwa gazeti la mwananchi ni gazeti makini ambalo haliwezi kuandika habari za uwongo lakini jana tu gazeti hilo hilo limemwomba radhi Bernard Membe. Anasema hajawahi kumhonga mwandishi yeyote ili kuziweka habari zake gazetini lakini hajaeleza ni kwa nini habari zake zote za kutaka madaraka ndani ya chama na tamaa yake ya urais kwenye gazeti la mwananchi zinaandikwa na mtu mmoja tu.
 
Hata mahakamani, kinachoangaliwa ni ushahidi. Ushahidi tumekwishaupata, wote wanne wamesema kuwa gazeti la mwananchi limeongopa. Tunataka ushahidi gani tena? Afadhali kama ingekuwa wawili wamesema kuwa walisema, wawili wanasema hawakusema, hapo tungeihitaji hiyo video ili tujue katika hawa wanne, ni nani anasema ukweli na nani mwongo. Sasa wote wanne wanasema hawakusema, tunahitaji tu ushahidi mwingine zaidi ya hizi kauli za waliotajwa?

Hao wanne wote wako upande mmoja, tuwe wavumilivu tupate na maelezo kutoka upande wa pili, tatizo ni nini? kumbuka hili swala hatuwezi kulifanyia maamuzi kama vile tunapiga kura, kwamba hoja ya wengi ndio ipite, hapa ni fact tu.
 
Haya sasa, mimi binafsi bila kumung'unya maneno nilishasema na nitasema daima (mpaka siku ABADILIKE) kuwa Zitto Kabwe ni MNAFIKI, na ni kijana hatari kwa mstakabali wa taifa letu kidemokrasia!

Sipingi wazo/ndoto yake ya kuwa rais bali njia anazotumia kuifikia ndoto hiyo ni ya kipuuzi na haikubaliki tuikemee na kuipinga, italiingiza taifa hili kwenye machafuko,

Atambue kuwa yeye amebeba dhamana ya tumaini la vijana wengi tena wakware wa fikra machipuko ambao ni hatari zaidi hasa walishwapo hata uongo tu!

Propaganda zake na ccm za kuivuruga chadema zimekuwa zikimulikwa usiku na mchana na kila hatua ya unyayo wake inahesabiwa kwa umakini mkubwa!

Wenzake ndani ya chadema wapo kila kona ya Tz wakikijenga chama (M4C) tena kwakujitolea wakila kwa mama ntilie, lakini yeye hata siku moja hajahudhuria mikutano ya chadema tangu alipoenda Songea na Mwanza kuipiga kampeni za udiwani mwezi wa pili kama si kosei! Amekuwa ni mtu wa ziara binafsi tu kila wiki yupo kwenye ndege, hana tofauti sasa na Rais wetu kwa ziara zilivyo:

Hivyo arejee kwenye mikingamo huru ya chama na tafakuri sahihi za ukombozi mororo bila kutumia mbinyo wa kuligawa taifa kwa makundi ya vijana, wazee na watoto!

Tunataka taifa lisimame pamoja, liongee lugha moja na litamalaki pamoja, huku tukijisifu uwepo wa uongozi safi wa kijana mwenzetu Zitto Zuberi Kabwe!!

Mbona hizo hoja zako ni dhaifu?? au ndio mambo ya ukanda mmeanza?????akitaka kugombea wa kanda fulani mnayaanzisha, zitto ni wetu anakubalika
 
Mbona hizo hoja zako ni dhaifu?? au ndio mambo ya ukanda mmeanza?????akitaka kugombea wa kanda fulani mnayaanzisha, zitto ni wetu anakubalika

Bado sijaelewa mantiki ya maoni yako, ukanda unautoa wapi ktk maandiko yangu hapo?
 
nimezungumza na mhe. filikunjombe yeye anasema ni kweli alikwenda kigoma na kwamba akiwa jukwaani ni kweli yeye (filikunjombe) na mhe. nasari walisema, "kwa mshikamano huu mlio nao wana kigoma, kigoma inawez kumtoa rais."

sasa maneno haya yana ubaya gani? kwani kigoma haiwezi kumtoa rais?
 
Haya sasa, mimi binafsi bila kumung'unya maneno nilishasema na nitasema daima (mpaka siku ABADILIKE) kuwa Zitto Kabwe ni MNAFIKI, na ni kijana hatari kwa mstakabali wa taifa letu kidemokrasia!

Sipingi wazo/ndoto yake ya kuwa rais bali njia anazotumia kuifikia ndoto hiyo ni ya kipuuzi na haikubaliki tuikemee na kuipinga, italiingiza taifa hili kwenye machafuko,

Atambue kuwa yeye amebeba dhamana ya tumaini la vijana wengi tena wakware wa fikra machipuko ambao ni hatari zaidi hasa walishwapo hata uongo tu!

Propaganda zake na ccm za kuivuruga chadema zimekuwa zikimulikwa usiku na mchana na kila hatua ya unyayo wake inahesabiwa kwa umakini mkubwa!

Wenzake ndani ya chadema wapo kila kona ya Tz wakikijenga chama (M4C) tena kwakujitolea wakila kwa mama ntilie, lakini yeye hata siku moja hajahudhuria mikutano ya chadema tangu alipoenda Songea na Mwanza kuipiga kampeni za udiwani mwezi wa pili kama si kosei! Amekuwa ni mtu wa ziara binafsi tu kila wiki yupo kwenye ndege, hana tofauti sasa na Rais wetu kwa ziara zilivyo:

Hivyo arejee kwenye mikingamo huru ya chama na tafakuri sahihi za ukombozi mororo bila kutumia mbinyo wa kuligawa taifa kwa makundi ya vijana, wazee na watoto!

Tunataka taifa lisimame pamoja, liongee lugha moja na litamalaki pamoja, huku tukijisifu uwepo wa uongozi safi wa kijana mwenzetu Zitto Zuberi Kabwe!!

Wakati tuko chuo Zito alishawahi kutmka kuwa lazima aje kuwa Rais. Tuliofanya siasa na Zito pale UDSM tunamjua. Jamaa ni makeke kwa kwenda mbele nadhani hiyo dhamira yake bado iko moyoni na lazim je jitutumue muda si mrefu iwe ndani ya chadema au nje y cdm, lazima atakuja kugombea Urais-believe me!
 
Ukisoma maantiki ya maandiko yangu wala sijapinga yeye kugombea urais au kuwa rais,

Hofu yangu ni njia apitiazo na wakati stahiki wa kuutafuta urais huo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom