Filikunjombe atoa mitego ya kunasa wanyama waharibufu wa mazao Ludewa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Nyani_bmp3.jpg


Wananchi wa kitongoji cha Maramba kata ya Luilo walisema kuwa wanampongeza mbunge Filikunjombe kwa msaada wake wa nyavu ya kutegea nyani( Lipilipili) ambayo imewawezesha kutega nyani zaidi ya 80 hadi sasa toka zilipotolewa miezi miwili iliyopita.

Maeneo mengine ambayo mbunge Filikunjombe alitoa msaada wa Lipilili kwa ajili ya kutega nyani hao ni pamoja na Liughai na Lifuma kata ya Luilo ambako pia wamefanikiwa kutega nyani zaidi ya 50.

Huku wananchi wa kata ya Rupingu katika kijiji cha Nindi na kata ya Lifuma kijiji cha Mtalawamba walisema kuwa msaada huo wa mbunge wa mitego ya nyani umeongeza kasi ya wananchi kuanza kulima zaidi mazao ya chakula kutokana na awali kuogopa kulima kutokana na nyani hao kutishia usalama wa zao.
 
[h=3]WANANCHI LUDEWA WAFURAHIA KITOWEO CHA NYAMA YA NYANI[/h]

WANANCHI Ludewa mkoa mpya wa Njombe wafurahia zawadi ya mbunge wao Deo Filikunjombe ya mitego ya nyani wanaokula mazao yao kuwa imewasaidia kupata kitoweo cha nyama ya Nyani zaidi ya 100 waliouwawa hadi sasa.

Hata hivyo kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa vya kutegea nyani hao wananchi hao wamedai kuwa ulaji wa nyama ya ng'ombe katika maeneo hayo umeshuka zaidi baada ya upatikanaji wa nyama ya nyani kuwa wa rahisi zaidi na nyama yake ni gharama ndogo kuliko ya ng'ombe.

Wananchi wa kitongoji cha Maramba kata ya Luilo walisema kuwa wanampongeza mbunge Filikunjombe kwa msaada wake wa nyavu ya kutegea nyani( Lipilipili) ambayo imewawezesha kutega nyani zaidi ya 80 hadi sasa toka zilipotolewa miezi miwili iliyopita.

Afisa Maliasili wa Wilaya hiyo, Japhet Mnyagala alisema matumizi ya nyama ya nyani yameanza kuhatarisha uwepo wa wanyama hao katika misitu mbalimbali ya wilaya hiyo.

Baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo waliozungumza kwa sharti la kutotaja majina yao gazetini, walisema nyama hiyo ni mkombozi mkubwa katika familia zao kwasababu inauzwa kwa bei nafuu.

"Tunaomba Mungu wanyama hawa waendelee kuwepo katika mapori yetu kwasababu sisi tusio na uwezo wa kununua nyama ya ng'ombe na mbuzi, tutaendelea kuila nyama ya nyani," alisema mmoja wao.

Alisema nyama hiyo imekuwa ikuzwa kwa kati ya Sh 2,000 na 3,000 kwa kilo wakati ile ya ngombe imekuwa ikiuzwa kwa kati ya Sh 6,000 na Sh 7,000.

Mkazi mwingine anayetumia nyama hiyo alisema mbali na utamu wake kuuzidi ule wa nyama ya mbuzi, haina madhara yoyote ya kiafya kwa matumizi ya binadamu na akaomba serikali ihalalishe.

Alisema nyama ya mbuzi ambayo matumizi yake sio makubwa sana katika maeneo mengi wilayani humo inauzwa kwa Sh 6,000 kwa kilo huku kuku mmoja akiuzwa kwa zaidi ya Sh 15,000.

Akizungumzia mikakati ya serikali ya kukukabiliana na uwindaji haramu wa nyani, Afisa Maliasili wa wilaya hiyo alisema wanashilikiana na jeshi la Polisi kuwasaka wahusika.

Hata hivyo alisema kazi ya kuwakamata watu hao ngumu kwasababu wanaokosa ushirikiano kutoka kwa jamii inayotunza siri za wawindaji hao.

Alisema taarifa walizonazo zinadai kwamba nyama hiyo inauzwa kama nyama ya mbuzi majumbani mwa watu na kwenye baadhi ya vilabu vya pombe.

Alisema maeneo yenye taarifa zilizokithiri kwa uuzaji wa nyama hiyo ni ya kijiji cha Ludewa kilichopo katika kata ya Ludewa, na vijiji mbalimbali vya kata za Mkomang'ombe na Kilondo.

Alisema katika maeneo hayo wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi ili washirikiane na serikali kuwabaini wawindaji haramu kwasababu nyani kama ilivyo kwa wanyamapori wengine wanapaswa kuhifadhiwa kwasababu za kimazingira na shughuli za utalii.
 
Back
Top Bottom