Filamu za kitanzania: Mazuri na mabaya

Nimeshindwaaaaa, nimevumilia; Oooops, ulimi hauna mfupa-kumbe inawezekana ndo tatizo linalowakabili watengeneza sub-titles za filamu za kibongo!Nilichokususdia kusema ni kwamba, nimevumiliaaa; nimeshindwa na sasa nimeamua kuweka wazi!hivi, ni nani anatengeneza sub-titles za filamu zetu? Ni kwamba kidhungu kimewapiga chenga kiasi hicho au ni haraka ya kuiwaisha filamu sokoni? Au ndo tuseme mambo ya kufupisha maneno kama tulivyozoea kwenye sms ( kwa simu za mkononi)?Binafsi, hamna sababu yoyote kati hizo ambayo ni ya msingi zaidi ya kuonesha kwamba watengenezaji wa subtitles na filamu zetu kwa ujumla, hawapo serious katika kazi zao. Hivi sasa, kwenye filamu nyingi wanajitahidi ku-include na subtitles, bila shaka ili kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu! GOOD IDEA!! Sasa kama lengo ni kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu; sasa mbona hawapo serious kwenye subtitles zenyewe? Wacha nitoe mfano wa filamu moja ambayo jana nimeiona kupitia kituo cha televisheni ya CITIZEN. Jina la filamu hii silifahamu, isipokuwa muhusika mkuu ni Blandina Chagula/Johari (lakini katumia jina la Martha). Martha alianza kama msichana mdogo mwenye kufurahia maisha kabla baba yake hajafungwa jela kwa miaka 7 na mama yake kufariki kutokana na mshituko kufuatia kifungo cha mumewe! Baada ya tukio hilo, shangazi wa Martha akahodhi mali zote za kaka yake(baba yake Martha) na Martha kupelekwa kijijini ambako baada ya kumaliza elimu ya msingi tu akawa analazimishwa kuolewa na chapombe mmoja hivi( nazani huyu bwana anajiitaga Kenyatta(sina hakika sana)! Baada ya kufuatilia subtitles hizo, niligundua kwamba katika kila subtitles 3 zinazotokea kwenye screen, basi 2 zina mapungufu makubwa ambayo mengine ni ya kubadilisha maana mzima(na kuweka opposite meaning). Sikufuatilia sana, lakini pamoja na hayo, niliziona zifuatazo:
· Nina she was going……hivi tangu lini noun na pronoun zikakaa pamoja?
· You are a big layer, wakimaanisha huyo mtu ni muongo mkubwa na badala yake kawa mtaga mayai mkubwa!
· I promise I never let me down…eti wakimaanisha siwezi kukuangusha!
· You show as good discipline… wakimaanisha Martha anaonesha nidhamu mzuri
· Hello my fiancé …ni Martha huyo anakuwa fiancé, yaani mchumba!
· I waiting to you….wala sijajua walitaka kusema nini!
· Why you fos me…jamani, hivi si utani huu ikiwa lengo ni ku-capture international market?
· You parents…eti walikuwa na maana ya "wazazi wako"!!
· Stand up out….jamani, inawezekana ni punctuation problem, lakini kwanini wasiwe serious kwenye mambo muhimu kama haya?
· Thans so much…si mzaha huu?mnakimbilia wapi jamani?
· As long as your here…..sehemu nyingi sana kuna tatizo kati ya "you are" na "your"!
· Next week your going…..hata mimi kidhungu sikifahamu, but this is too much!
· What ca I do…..? acha wajanja wawaibie filamu zenu kwavile mnafanya mchezo kwenye kazi, manake hii "ca" imetumika sehemu nyingi sana!
· Your doing good……au ndo mimi nisiyejua ninachoongea?!
· I can't leave in this life……eti nasikia kuna baadhi ya shule wanataka kufundisha kijeremani huku bado tukifahamu leave ni kuishi!

Sawa, Kiingereza sio lugha yetu, lakini utafanyaje masihara kwenye serious issues namna hii? Kwanini hiyo kazi wasipewe watu wanaofahamu lugha kidogo? Wahusika wa filamu hii ni miongoni mwa waigizaji wakubwa hapa TZ (Kuna Blandina, Dr. Cheni, kuna akina mama wawili ambao nao ni waigizaji wakubwa tu, kuna Aunt Ezekiel, Issa (nimesahau jina lake la kisanii, ila nazani ni m zanzabri huyu bwana kutokana na lafudhi na rangi yake, na ni muigizaji mkubwa tu); vilevile kuna binti mmoja mdogo ambae ambae ali-act kama Martha alipkuwa mdogo; zamani alikuwa mtangazaji wa kipindi cha watoto ITV, nae ni muigizaji mkubwa tu haya kama ni binti mdogo!Nimetaja wahusika hao kuonesha kwamba naamini waandaji wa filamu hi wababaishaji vinginevyo wasingeweza kuwa-recruit wasanii wakubwa hivyo! Sasa kama hivyo ndivyo, kwanini wameshindwa kuwa serious kwenye issue muhimu ya subtitles? NAJENGA HOJA!

kuna movie ta kibongo pia niliiona yaani hizo subtitles ni kichekesho..toka siku hiyo wala siangalii picha za kibongo ni vichekesho...we're not serious at all,ubabaishaji/usanii kila eneo.
 
Ndugu Wana JF, ni wakati wa kuwanyoshea vidole hawa waigizaji wetu a.k.a Celebrities wetu.
Kwanini hawajifunzi kwa Wanigeria au Ghana? Nimecheki filamu moja ya Ndugu Richard wa BBA ni Uoza mtupu, inaitwa Another Wife nilitegemea kwamba Richard angeleta mabadililko coz ametembea tembea huko ng’ambo kidogo na pia ana exposure kumbe ni yale yale, Kuna sehemu anaonekana kijijini akiwa anabadilisha badisha magari ili ampe huyo another wife, sikuelewa kama hayo magari aliyapeleka vipi huko kijijini, pia muda wa filamu ni mfupi sana then wanakundikia usikose toleo lijalo a.k.a PART TWO. Nadhani haya magazeti ya Udaku chini ya Mdau Shigongo yanawapotosha vijana wetu wenye vipaji coz ukisoma sifa zinatolewa ktk magazeti ya udaku na hali halisi ya Movies zenyewe ni kama mbingu na Ardhi.
Nawakilisha kwenu wana Jamii.
 
'm a big critic wa picha za kibongo sabab naonaga upotoshaji wa reality ya maisha yetu.
1. They potray a life ya kimarekani, nigeria and south africa kama maisha yetu wa bongo. that violent scene.
2. There's no emotion in their acting inapoitajika.
3. they put wrong people i the scenes. mfano, kijana mdogo wanamuweka ndie tajiri kweli. sasa angalia maisha yetu ya tz, kweli tunavijana wenye utajiri wakupindukia wadogo?
4. they think u superstar ni passport yakuwa better actor. hii ipo hata USA and 'm a critic of musicians wanae act eti sabab tu wao wanawajua directors wa hollywood.
5. JB anakunja uso all the time hata sehem hatakiwi.
6. tajiri na nyumba ya gorofa anaendesha mark 2 GX90. y hawatumii gari inaelingana na hadhi ya maisha yake?
I only give them credit wakiact maisha ya vijijini. Hapo wanaweza.
Lakin tuna kazi kweli.
 
thatha wale wenzetu wa-Nigeria ukiziangalia profile zao wengine wana PHD za sanaa utawalinganisha na hawa wetu .movie zetu jamani watanisamehe huwa sinunui labda nikaangalie kwa jirani ..Sababu kubwa inayonifanya nishindwe kununua mala nyingi zinakuwa kama copy na za Nigeria (wanaziigiza nyingi)
 
naamini wenye makosa na ambao ni wakulaumu kufuatia kuporomoka na kutokuendelea kwa soko la filamu Tanzania ni MADIRECTORS. kuna makosa ya editimg pia, kuna vitu ambavyo havikufanyi uwe na taaluma maalumu kuweza kujua kua kuna ushamba katika utengenezaji wetu wa filamu.
 
thatha wale wenzetu wa-Nigeria ukiziangalia profile zao wengine wana PHD za sanaa utawalinganisha na hawa wetu .movie zetu jamani watanisamehe huwa sinunui labda nikaangalie kwa jirani ..Sababu kubwa inayonifanya nishindwe kununua mala nyingi zinakuwa kama copy na za Nigeria (wanaziigiza nyingi)

aaghaghaaghaaaaa, kazi kaziiiiiiiiiii kweli kweli!

Hapa FL wan'rusha matumbo kwa kicheko mhmmmm,. Yaani na wewe unakuwa kama wale jamaa ambao hawataki kununua magazeti, ila we ukirogwa tu kununua, "upo front page" yeye anataka umpe ukurasa wa Michezo,,,,na tabia zao ni kusoma gazeti lote mpka vile vijitangazo vidogovidogo vya biashara!...na akimaliza, duh, simulizi lake mtaani utadhani ndo Mhariri wa hilo gazeti...kelele nyiiingi, na akiwa mshabiki wa timu fulani iliyofanya vizuri na ameona kwenye hilo gazeti basi hapo tena atakutukana mpaka na wewe uliye nunua gazeti ukampa asome!.

Nunua bana movie zetu tusaidie vijana, wasitukabe!.Hata Nollywood nao walianza hivi hivi!.
 
hahaha asante Ngoshwe kwa msisitizo nitaanza kununua jamani
 
thatha wale wenzetu wa-Nigeria ukiziangalia profile zao wengine wana PHD za sanaa utawalinganisha na hawa wetu .movie zetu jamani watanisamehe huwa sinunui labda nikaangalie kwa jirani ..Sababu kubwa inayonifanya nishindwe kununua mala nyingi zinakuwa kama copy na za Nigeria (wanaziigiza nyingi)

FL: Umenena, kuna movie unaweza kuangalia ukaanza kujiuliza hili picha nishaliona wapi, ukivuta kumbukumbu unakumbuka kumbe ni picha ya kinigeria.
 
aaghaghaaghaaaaa, kazi kaziiiiiiiiiii kweli kweli!

Hapa FL wan'rusha matumbo kwa kicheko mhmmmm,. Yaani na wewe unakuwa kama wale jamaa ambao hawataki kununua magazeti, ila we ukirogwa tu kununua, "upo front page" yeye anataka umpe ukurasa wa Michezo,,,,na tabia zao ni kusoma gazeti lote mpka vile vijitangazo vidogovidogo vya biashara!...na akimaliza, duh, simulizi lake mtaani utadhani ndo Mhariri wa hilo gazeti...kelele nyiiingi, na akiwa mshabiki wa timu fulani iliyofanya vizuri na ameona kwenye hilo gazeti basi hapo tena atakutukana mpaka na wewe uliye nunua gazeti ukampa asome!.

Nunua bana movie zetu tusaidie vijana, wasitukabe!.Hata Nollywood nao walianza hivi hivi!.
So anunue hata kama ni pumba? kisa vijana wetu wasiwe wezi au vibaka mtaani? Nadhani kuna mambo mengi kufanya si lazima kufanya Filamuz. wakajifue katika soka ili kaka Mziray akichukua timu baada Maximo anaweza kuwaita Taifa Staz kwenye Neema.
 
waghana wala wanaijeria bado. filam simpo na zenye akili ni zile za Black American Movies. they are so real na sidhani kama zina gharama kiivyo
 
Mi kwahili naomba nisisme kitu maana nina hasira sana

Hasira za nini wee kaka?? Sema tu kilicho moyoni usijepata vidonda vya tumbo.

Labda nadhani wacheza sinema wetu wanawahi mno kuingia katika soko na kujitangaza kama mastaa wakati bado hawajafikia viwango stahiki. Mtu unakuta alikuwa mwingizaji (sanaa za kuingiza) siku mbili unasikia ametoa “movie” tena kwa lugha ya kigeni!.

Wanahitaji kujifunza sana. Hili la kulimbuka lipo katika sekta zote hapa nchini, hata kwenye soka na sekta ya muziki hali ni hivi hivi ya kutaka umaarufu wa haraka na ndo linaua vipaji vya vijana wetu….
 
2)English subtitles - Hapa ndio kuna vituko kweli. Yaani unasoma hizo tafsiri ya English kwenye hii movie mpaka unabaki kushangaa. Ndio najua wengi tunachemsha kwenye English, lakini kama film industry ya Bongo inataka kuwa serious (kujiingiza kwenye soko la nje), basi haitakiwi kuruhusu makosa kama yale. Kuna part moja ndio iliniacha hoi kabisa. Steve na Irene walikuwa restaurant, Zanzibar. Basi Steve akawa anamwambia Irene "tafuna…tafuna…tafuna," akimsisitizia kuwa atafune chakula anamchomlisha. Sasa kwenye subtitles tafsiri yake ikawa "cat…cat….cat."……I was like ‘enhe!' Mwanzo sikujua walikuwa wanajaribu kuandika nini, lakini nikaja kugundua kuwa dhamira yao ilikuwa kuandika "cut…cut…cut," neno ambalo bado sio tafsiri sahihi ya tafuna.

Mimi huwa nachoka hapo kwenye subtitles yaani ni vituko vitupu halafu ukizingatia siku hizi muvi hizi zimeanza kufika kimataifa kama African Magic sasa wanawakanganya watu wanapokiswahilisha kiingereza. Hivi huwa wanafanya review hawa watu kweli? Ukweli unabaki pale pale wahusishe wataalamu mbalimbali katika kazi zao
 
Mi napendekeza lianzishwe jukwaa rasmi la kuhakiki au ukosowaji wa filamu na nyimbo za bongo ndani ya JF. Labda wanaweza kujirekebisha!
 
Kuna kitu watu wanasema! Elimu ndogo ni sumu! Sidharau elimu ya mtu hapa lakini ukweli ni kwamba hata siku moja wewe huwezi kuwa actor halafu hapo hapo wewe unageuka kuwa editor kesho kutwa wewe ndo sound engineer! Ufanisi wake ni zero! Hicho ndio kinafanyika Bongo! Sinema za wenzetu ni vigumu sana kupata makosa ya kiufundi kama hayo! Kila kitengo kina mtaaluma wake! Uigizaji ni taaluma pia! Sio kimbilio la walioshindwa shule!!!!!! Yapo matukio kwenye Bongo Movie unaweza lia! Unajiuliza hapa walikuwa hawaoni jamani! Niliwahi ona movie moja Mgojwa napelekwa hospital ndugu na jamaa wa mgojwa,. moja kwa moja mpaka kwa chumba cha operation! Practically hilo halipo! Kuuvaa uhusika ni sifuri yaaani jamaa ataendelea kukukumbusha kwamba anaigiza! Lugha za kitaaluma mfano Dk anaelezea maendeleo ya mgojwa au progress ya ugonjwa vitasemwa vitu hapo mpaka unazima kwanza movie!

Lakini mimi nawalaumu wenye taaluma zao za sanaaa ambao wamekailia maofisini wamewaachia laymen taaluma hii! Mko wapi wasomi wa fani za uigizaji! Tanzania tuna kiu na movie zenye kiwango sio maigizo
 
Back
Top Bottom