Filamu za kitanzania: Mazuri na mabaya

2. kulikuwa hakuna colour filter hata kidogo in day light alafu usiku wanaweka filter la ajabu eti wameweka filter ya pembeni kuna jiza katikati kuna mwanga yaani kama vile mtu anaota
(Watanzania mmeshinndwa kuingia youtube muangalie jinsi ya kutengeneza filter kwenye movie???)
mkuu muda wa kuingia youtube hawana wako utamu wanajibu comments......
 
Ni miaka mingi sasa tunaendekeza upuuzi katika filamu zetu za kitanzania ni lini tutabadilika?
juzi hapa nimejiloga nikaangalia movie ya kitanzania inayoitwa oprah
nikakuta makosa ya kipuuzi ambayo sikutegemmea kuyakuta matika movies za 2008

Niliangalia ile movie part 1 and 2 nilivyomaliza nikavunja cd zote cauz ni aibu

makosa:-

1. walikuwa wanachovya mic kila dakika ndani ya screen
(seriously ni kwamba zile movies hazina reshot kama maizigo au?)

2. kulikuwa hakuna colour filter hata kidogo in day light alafu usiku wanaweka filter la ajabu eti wameweka filter ya pembeni kuna jiza katikati kuna mwanga yaani kama vile mtu anaota
(Watanzania mmeshinndwa kuingia youtube muangalie jinsi ya kutengeneza filter kwenye movie???)

3. scene nyingine hazina maana. kama scene moja ilikuwa inarudiwa kila dakika [ ile ya kuingiza gari ndani kupark ile scene ilikuwa inachukua more than a minute alafu haikuwa ya maana alafu inarudiwa kila dakika na car parking scene hazionyoshwagi zotee kwa mmda mrefu vile

4.scene ya kuonyesha magari yanatokea sehem kuanzia mwanzo mpaka inapofika sommetimes inachukua more than 5mins to show that scene (wow we sure have directors)

5. aliyeandika script alikuwa anakimbizwa script haikuwa imenyooka hata secunde. kama ile scene mwanzoni mshkaj anakutana na rafiki yake alafu yule rafiki yake anabakia kushangaa kama kaona shetani na alikaa more than 2mins anajidai hamjui mtu ambae alikuwa ni rafiki yake wa karibu sanaaaa
( hivi kuna mtu anamsahau mtu ambae alikuwa ni rafiki wake tena wa kushibana tena seconndari afathali ungeniambia primary)

6.wameshirikisha watu wachache sana kwenye movie. [ naweza kulikubali hili kama ni mambo ya budjet] but hivi yule miriam walimueka wa nini pale? cauz kitu miriam alichokifanya ni kumwambia tu yule oprah kuwa unabahati kupata mwanaume anayekupenda, and nothing else hawajaweza kuweka mtu mwenye activity nyingine hata moja yaani kama maigizo

7.sound tracks zilikuwa hovyo [ Nathani tunawaigiza watu wa western(nigerians)] na its stupid cauz utakuta sehem ya starehe wenyewe wanaweka soud track ya mazishi
( programs za kutengeneza sound trcks ziko nyingi sana kwenye internet it the matter of downloading them and playing with them)

8. ubahili wa kurefusha scene kuna sehem yule oprah aliondoka na yule mshkaj wakaenda zanzibar ile scene waliweka sound track na kuonyesha shots more than 20mins. (ni director kafanya hivi au aliyetengeneza script?)

9.kuna makosa mengi sana niliyoyaspot that day nilitamani kulia lakini kuna kimoja walikipatia

10. walichopatia ni make up ya yule demu always alikua anaonekana poa walichokosea kuhusu make up wanaume kuna wakati walikuwa wanaongezewa sana makeup wakawa wanatokea kama vinyago

Niliiona movie hiyo nikaona kweli upumbavu mtupu; sijaona movie nyingine nyingi ila nilipata kopi ya hiyo OPRAH kutokana na matangazo yake nikadhani huenda itakuwa nzuri. Hakuna professionalism yoyote hata chembe moja. Wangemwoma jamaa wa Bongoland awe anawasaidia kutengeza movie zao.
 
My take to Bongos movies:

Actors/actresses are school dropouts who seek refuge in the industry to swindle easy monies. The so called movie directors are mere conmen!!

There is no professionalism at all. My suggestion if at all they plan to understand me is that they should start with DRAMA. oh, wait a minute... do we have drama theaters? No! So, no movies, no industry! Wizi mtupu!!!!
 
Movie Bongo!!! Msinitapishe Nyie hizo ni Video Game Ndugu zangu Movie mchezo! ....Filamu iliotengenezwa nchini Kenya Mwaka 1977 MLEVI Mpaka leo ipo katika mahadhi ya Kifilamu Kuliko hizi Tamthilia zenu za Leo.
Hiyo movie ya Mlevi kwa kweli ilitengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hakuna ubishi katika hilo.
 
Ni kweli kabisa filamu zetu zina ubora mdogo na maudhui ambayo hayakupangika hata kidogo. kila siku utaona watu katika magari na nyumba kama wanigeria vile. Nafikiri kwa mazingira yetu tuna kazi ya kufanya. Ni hawa hawa wanatayarisha video za wanamuziki wetu ambazo hazina ubora kabisa. utakuta video iliyopigwa na Komedi Original ni nzuri kuliko ile halisi ya mwanamuziki wanayemuigiza. lazima tufanye kazi ya ziada na kuwekeza katika ulimwengu wa filamu.
 
Nina shangazwa na tabia ya watanzania,tunapenda sana kusifia vitu vya wengine badala ya kusifia vyakwetu.Vijana hawa wanaotengeneza sinema au maigizo wanajitahidi kwa sehemu yao.kama vile ulivyozaliwa na hukuanza kutembea siku hiyohiyo mwana/bibi Makundi ndivyo nao wanaendelea.Siku zote tunajifunza kutokana na makosa kadri mnavyo wasaidia katika kuwarekebisha badala ya kuwashutumu ndivyo wanavyoendelea kutengeneza kitu kizuri zaidi.Tuache tabia kama hii ya kuto dhamini kazi ya mtu. mimi ningekudhamini kama ungeanza na wewe zakwako ili uwape hiyo changamoto.
Nadhani unakasumba ya kina Rambo,na wengine wote ukisahau kuwa nao walianza hivyo hivyo.

If the wheel is invented, you dont have to re-invent. Kwanini wewe upitie uchuro huo huo wakati unajua kuna jinsi ya kuruka? usilete sababu za namna hii, kwani ndio maana waafrika hatuendelei.
 
Haha kuna Movie moja nilikua naangalia kuna scene jamaa yuko chumbani na demu, sasa mle chumbani kuna kabati lenye kioo, basi camera man na yule sound tech wakawa wanaonekana full length!!! na sio for a few seconds ilikua ni karibu scene nzima!!
Sidhani kama inawezekana kuwa hawakugungua hilo, kweli hawapo serious na kazi!!!
 
I am a big movie fan. I am a big Nollywood (Nigeria) and Bongowood (Tanzania) films. Ama kwa hakika mwanzo mgumu kwa wote.

Nadhani kitu kimoja lazima tuangalie between Nollywood and Bongowood ni kwamba they are both African stories and they are bound to be the same! Bollywood has copied tremendously from Hollywood, Hollywood has copied tremendously from Hong Kong movies. These are from different continents but us here in Afrika our stories are the same, these movies, though I agree they are sometimes not of the best quality, are truly African.

To those who are exposed to WWE, many say its fake but they are missing the point! Its about entertainment - watch it for the entertainment value and don't watch it searching for the falseness. Watch Bongowood with the facts that the movies are made on limited budgets, technology, and maybe even newness. Zina makosa madogomadogo lakini how many western movies you also see mistakes or even microphones etc? Remember the bogus movie "Belly" starring Nas - there was a couple of scenes in there that showed the mic. In "Commando" after Arnold rolled a yellow Porsche denting it he was seen driving it off as if new! and many more.

Bongowood is suffering from kutokuwa makini but actually there are some gems - have you watched "Masaa 24"? Some of the movies written and starring Lucy Komba are pretty good. The acting groups such as those like Kaole or that which has Mzee Small and Bi Chau and Kingwendu are also good entertainment. "Simu ya Kifo" and if you fail you can't miss Bongoland II - afterall it is a Bongowood film isn't it?
 
Mkuu Vindunda thanks a million times kwa mchango wako ndugu na ubarikiwe.
You said it all mkuu.

Ni kweli kuna factors nyingi sana zinazofanya movies za kibongo zinaonekane na katika kiwango kisichoridhisha ikiwa mojawapo ni budget finyu, uzoefu mdogo kny sanaa hii, soko la sanaa hiyo etc. Hata na hivyo sijui mtoa mada hii ameshaangalia movie ngapi za kibongo, mi naamini sio zote ni mbaya zipo ambazo ni nzuri sana kama zile zilizo washilikisha kina Kanumba, Kigosi etc so kuzijumlisha zote kuwa ni bomu tunakuwa hatuwatendei haki wasanii wetu wanaojitahidi kujikwamua kutokana na umasikini kwa njia hii.
 
Tatizo letu tunapenda mno kukurupuka, mtu ukiwa na camcorder moja na computer yenye adobe premiere au final cut tayari unataka kuwa movie producer halafu unkimbilia kutengeneza film iishe in one week sababu unabana matumizi. Pia hatutaki kujifunza kuhusu utengenezaji filamu, internet hii hii ina materials za kumwaga kuhusu film making (tafuta hata kwenye google) lakini do we do that? nooooo....tunaishia kwenye ze utamu!

Tuache kuangalia nigeria kama ndio waalimu wetu pekee katika filamu za africa. Tuwe na vitu original kutoka hapa hapa kwetu na sio kung'ang'ania themes za nollywood (uganga, uchawi, mashetani na majini)...uigizaji wetu tunawaiga wanigeria wanavyoongea kwa msisitizo huku wametoa mimacho, uvaaji tunawaiga wao pia ili mradi vurugu tupu!

Kuna nchi nyingi za africa zinatengeneza film nzuri sana kuanzia misri, algeria, senegal, mali, afrika kusini nk...kuna watengenezaji filamu magwiji wa kiafrika kama Sembene Ousmane... tujifunze kutoka kwao pia. Hivi karibuni tu kulikuwa na Pan African Film festival huko Burkina Faso, natumaini tumeweza kujifunza chochote toka huko.
 
movie za kibongo ni za kisenge sana...
i dont watch them...ni usenge mtupu...
i'd rather go for american movies...
thats all

Duh post ya kwanza na matusi makubwa hivi... Mkuu nadhani ndani ya JF kuna watu wana matusi zaidi yako ila sio mahala pake... people are here kujifunza na kupata consrtuctive criticism - JARIBU KU-EDIT POST YAKO MKUU

Back to the point, ni kweli movie za bongo bado, lakini nadhani tujitahidi kukosoa na kuwapa feedback waandishi, waongozaji na mabaraza husika ili kuweza kuwashauri... Nimeangalia africa movie kwenye dstv kuna baadhi ya hizo movie sio mbaya sana

na pia tugundue bado tuko kwenye home video status, safari bado ndefu na kuwasaidies hao wasanii kusonga mbele
 
Huwa ninapenda kuangalia movie za kibongo.

Ingawaje tunajitahidi kwenda na wakati, lakini naona kuna makosa kibao ya wazi tunayafanya ambayo yangeweza kuepukika.

Editing
Kosa kubwa la kwanza ambalo tunafanya ni kukosa Editors ambao wako serious na kazi zao. Unategemea Editor ndio ambaye angefanya kazi mzuri ya kureview movie , yet bado kuna makosa madogo madogo kibao ambayo yananakera sana kuyaona.

Mfano – Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)

1)Sauti - sauti ya hii movie inatoka kama sauti ya mwangwi (echo). Ni kama vile walikuwa wana record kwenye chumba cha mwangwi, halafu baada ya kuchukua sauti za waigizaji wenyewe, wakachukua sauti za ule mwangwi wenyewe. Yaani sauti inatoka kama ya mtu unayeongea naye kwenye simu ambaye amejifungia chumbani au kwenye kopo.

2)English subtitles - Hapa ndio kuna vituko kweli. Yaani unasoma hizo tafsiri ya English kwenye hii movie mpaka unabaki kushangaa. Ndio najua wengi tunachemsha kwenye English, lakini kama film industry ya Bongo inataka kuwa serious (kujiingiza kwenye soko la nje), basi haitakiwi kuruhusu makosa kama yale. Kuna part moja ndio iliniacha hoi kabisa. Steve na Irene walikuwa restaurant, Zanzibar. Basi Steve akawa anamwambia Irene “tafuna…tafuna…tafuna,” akimsisitizia kuwa atafune chakula anamchomlisha. Sasa kwenye subtitles tafsiri yake ikawa “cat…cat….cat.”……I was like ‘enhe!’ Mwanzo sikujua walikuwa wanajaribu kuandika nini, lakini nikaja kugundua kuwa dhamira yao ilikuwa kuandika “cut…cut…cut,” neno ambalo bado sio tafsiri sahihi ya tafuna.

Sasa makosa mawili kama haya yalitakiwa yashughulikiwe na editor. Hapa ndipo editor anapo onyesha umahili wake katika fani hii. Udhaifu wa makosa kama haya unaonyesha jinsi gani editors wa kibongo wasivyo serious na kazi zao.

Wardrobes
Ukweli ni kwamba waigizaji wana overdress mno. Sasa sijui wanajaribu kuonyesha kuwa wanajua kuvaa sana au vipi? Lakini mara nyingi wanavaa ‘loud clothes’ mno kulingana na scenes/story za movies.

Mfano - Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)

Vincent - anavaa very loud suits just kwenda kazini tu. Tena ana match na fancy shoes na hat kabisa. Unakuta kakupigia all white, kuanzia viatu, suruali, koti, kofi, na kakupigia shati moja kali jeusi…. Halafu anaishia kwenda kazini mchana kweupe. I mean, watu upiga hayo mavazi wakiwa wanakwenda kwenye mtoko jioni.

Steve – huyu yeye anakuvalia jacket moja zito la nguvu kwenye 100 degrees condition. Pia anakupigia miwani moja kubwa sana…Anavaa hivyo vyote only kwenda chuo.

Miss Uwoya - Huyu ndio alikuwa anafunga kazi kabisa. Well, lazima nikubali kwanza, kuvaa tu anajua. Maana baadhi ya mavazi yake yalikuwa yananifanya niweweseke ile mbaya…lol. Anyway, bibie huyu alikuwa anavaa pamba kali kama zile tulizozizoea kuwaona dada zetu wanugu wakivaa clubs (huku waki drop-it-like-its-hot). Yaani anakupigia capri ya nguvu, huku akimachisha na sleeveless top na fancy cowgirl hat (or whatever it’s called) mchana kweupe…..halafu huyo anaelekea sokoni kwenda kununua nyanya.

Scenes
Hawazingatii umuhimu wa mazingira wanayofanyia baadhi ya settings.

Mfano - Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)

Vincent supposedly ana ofisi pale kwenye jengo la Millenuim Tower. Sasa unakuta kila anapoenda kupaki pale juu, hakuna hata gari jingine kwenye ile parking. Well, inavyoonekana ile sehemu ya scene walitengeneza either jumamosi or jumapili. Lakini katika hali ya kuongeza ufanisi wa utengenezaji wa fialmu, ningetegemea pengine wangetengeneza scene ya ile sehemu angalu kwa siku mbili tofauti. Yaani, kwa sababu wameazima ofisi ya mtu kutengeneza filamu, basi wangefanya shooting ndani ya hiyo ofisi siku ambayo hakuna wenyeji (jumamosi au jumapili). Halafu wakafanya shooting ya kwenye parking siku ya weekday ambayo kuna magari yamepaki. Hiyo ingeipa movie ufanisi wa reality. I mean, hutegemei parking ya jengo kama lile kuwa empty siku ya kazi.

All in all, kwa mtazamo wangu, hili hawa wasanii wetu wa filamu waweze kuendelea na kutengeneza filamu zenye angalau standard quality, basi inabidi kuwe na panel ya critics. Ukosoajia utakaotoka kwa panel hii utawasaidia sana wasanii hawa kuzingatia kanuni za uigizaji. Ningependekeza baraza la wasanii Tanzania (kama lipo) liunde hii panel. Njia nyingine ni wadau kuunda a private panel of critics.
Well said,

Nimeunganisha hizi topics na naamini hii itakuwa mada ambayo ni fundisho kwa watengenezaji wa filamu zetu na waigizaji wake.

Kila la heri wakuu katika kuzipitia filamu zetu na kuwaonesha wapi wanakosea na wapi wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi.
 
Nimeshindwaaaaa, nimevumilia; Oooops, ulimi hauna mfupa-kumbe inawezekana ndo tatizo linalowakabili watengeneza sub-titles za filamu za kibongo!Nilichokususdia kusema ni kwamba, nimevumiliaaa; nimeshindwa na sasa nimeamua kuweka wazi!hivi, ni nani anatengeneza sub-titles za filamu zetu? Ni kwamba kidhungu kimewapiga chenga kiasi hicho au ni haraka ya kuiwaisha filamu sokoni? Au ndo tuseme mambo ya kufupisha maneno kama tulivyozoea kwenye sms ( kwa simu za mkononi)?Binafsi, hamna sababu yoyote kati hizo ambayo ni ya msingi zaidi ya kuonesha kwamba watengenezaji wa subtitles na filamu zetu kwa ujumla, hawapo serious katika kazi zao. Hivi sasa, kwenye filamu nyingi wanajitahidi ku-include na subtitles, bila shaka ili kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu! GOOD IDEA!! Sasa kama lengo ni kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu; sasa mbona hawapo serious kwenye subtitles zenyewe? Wacha nitoe mfano wa filamu moja ambayo jana nimeiona kupitia kituo cha televisheni ya CITIZEN. Jina la filamu hii silifahamu, isipokuwa muhusika mkuu ni Blandina Chagula/Johari (lakini katumia jina la Martha). Martha alianza kama msichana mdogo mwenye kufurahia maisha kabla baba yake hajafungwa jela kwa miaka 7 na mama yake kufariki kutokana na mshituko kufuatia kifungo cha mumewe! Baada ya tukio hilo, shangazi wa Martha akahodhi mali zote za kaka yake(baba yake Martha) na Martha kupelekwa kijijini ambako baada ya kumaliza elimu ya msingi tu akawa analazimishwa kuolewa na chapombe mmoja hivi( nazani huyu bwana anajiitaga Kenyatta(sina hakika sana)! Baada ya kufuatilia subtitles hizo, niligundua kwamba katika kila subtitles 3 zinazotokea kwenye screen, basi 2 zina mapungufu makubwa ambayo mengine ni ya kubadilisha maana mzima(na kuweka opposite meaning). Sikufuatilia sana, lakini pamoja na hayo, niliziona zifuatazo:
· Nina she was going……hivi tangu lini noun na pronoun zikakaa pamoja?
· You are a big layer, wakimaanisha huyo mtu ni muongo mkubwa na badala yake kawa mtaga mayai mkubwa!
· I promise I never let me down…eti wakimaanisha siwezi kukuangusha!
· You show as good discipline… wakimaanisha Martha anaonesha nidhamu mzuri
· Hello my fiancé …ni Martha huyo anakuwa fiancé, yaani mchumba!
· I waiting to you….wala sijajua walitaka kusema nini!
· Why you fos me…jamani, hivi si utani huu ikiwa lengo ni ku-capture international market?
· You parents…eti walikuwa na maana ya “wazazi wako”!!
· Stand up out….jamani, inawezekana ni punctuation problem, lakini kwanini wasiwe serious kwenye mambo muhimu kama haya?
· Thans so much…si mzaha huu?mnakimbilia wapi jamani?
· As long as your here…..sehemu nyingi sana kuna tatizo kati ya “you are” na “your”!
· Next week your going…..hata mimi kidhungu sikifahamu, but this is too much!
· What ca I do…..? acha wajanja wawaibie filamu zenu kwavile mnafanya mchezo kwenye kazi, manake hii “ca” imetumika sehemu nyingi sana!
· Your doing good……au ndo mimi nisiyejua ninachoongea?!
· I can’t leave in this life……eti nasikia kuna baadhi ya shule wanataka kufundisha kijeremani huku bado tukifahamu leave ni kuishi!

Sawa, Kiingereza sio lugha yetu, lakini utafanyaje masihara kwenye serious issues namna hii? Kwanini hiyo kazi wasipewe watu wanaofahamu lugha kidogo? Wahusika wa filamu hii ni miongoni mwa waigizaji wakubwa hapa TZ (Kuna Blandina, Dr. Cheni, kuna akina mama wawili ambao nao ni waigizaji wakubwa tu, kuna Aunt Ezekiel, Issa (nimesahau jina lake la kisanii, ila nazani ni m zanzabri huyu bwana kutokana na lafudhi na rangi yake, na ni muigizaji mkubwa tu); vilevile kuna binti mmoja mdogo ambae ambae ali-act kama Martha alipkuwa mdogo; zamani alikuwa mtangazaji wa kipindi cha watoto ITV, nae ni muigizaji mkubwa tu haya kama ni binti mdogo!Nimetaja wahusika hao kuonesha kwamba naamini waandaji wa filamu hi wababaishaji vinginevyo wasingeweza kuwa-recruit wasanii wakubwa hivyo! Sasa kama hivyo ndivyo, kwanini wameshindwa kuwa serious kwenye issue muhimu ya subtitles? NAJENGA HOJA!
 
Nimeshindwaaaaa, nimevumilia; Oooops, ulimi hauna mfupa-kumbe inawezekana ndo tatizo linalowakabili watengeneza sub-titles za filamu za kibongo!Nilichokususdia kusema ni kwamba, nimevumiliaaa; nimeshindwa na sasa nimeamua kuweka wazi!hivi, ni nani anatengeneza sub-titles za filamu zetu? Ni kwamba kidhungu kimewapiga chenga kiasi hicho au ni haraka ya kuiwaisha filamu sokoni? Au ndo tuseme mambo ya kufupisha maneno kama tulivyozoea kwenye sms ( kwa simu za mkononi)?Binafsi, hamna sababu yoyote kati hizo ambayo ni ya msingi zaidi ya kuonesha kwamba watengenezaji wa subtitles na filamu zetu kwa ujumla, hawapo serious katika kazi zao. Hivi sasa, kwenye filamu nyingi wanajitahidi ku-include na subtitles, bila shaka ili kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu! GOOD IDEA!! Sasa kama lengo ni kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu; sasa mbona hawapo serious kwenye subtitles zenyewe? Wacha nitoe mfano wa filamu moja ambayo jana nimeiona kupitia kituo cha televisheni ya CITIZEN. Jina la filamu hii silifahamu, isipokuwa muhusika mkuu ni Blandina Chagula/Johari (lakini katumia jina la Martha). Martha alianza kama msichana mdogo mwenye kufurahia maisha kabla baba yake hajafungwa jela kwa miaka 7 na mama yake kufariki kutokana na mshituko kufuatia kifungo cha mumewe! Baada ya tukio hilo, shangazi wa Martha akahodhi mali zote za kaka yake(baba yake Martha) na Martha kupelekwa kijijini ambako baada ya kumaliza elimu ya msingi tu akawa analazimishwa kuolewa na chapombe mmoja hivi( nazani huyu bwana anajiitaga Kenyatta(sina hakika sana)! Baada ya kufuatilia subtitles hizo, niligundua kwamba katika kila subtitles 3 zinazotokea kwenye screen, basi 2 zina mapungufu makubwa ambayo mengine ni ya kubadilisha maana mzima(na kuweka opposite meaning). Sikufuatilia sana, lakini pamoja na hayo, niliziona zifuatazo:
· Nina she was going……hivi tangu lini noun na pronoun zikakaa pamoja?
· You are a big layer, wakimaanisha huyo mtu ni muongo mkubwa na badala yake kawa mtaga mayai mkubwa!
· I promise I never let me down…eti wakimaanisha siwezi kukuangusha!
· You show as good discipline… wakimaanisha Martha anaonesha nidhamu mzuri
· Hello my fiancé …ni Martha huyo anakuwa fiancé, yaani mchumba!
· I waiting to you….wala sijajua walitaka kusema nini!
· Why you fos me…jamani, hivi si utani huu ikiwa lengo ni ku-capture international market?
· You parents…eti walikuwa na maana ya "wazazi wako"!!
· Stand up out….jamani, inawezekana ni punctuation problem, lakini kwanini wasiwe serious kwenye mambo muhimu kama haya?
· Thans so much…si mzaha huu?mnakimbilia wapi jamani?
· As long as your here…..sehemu nyingi sana kuna tatizo kati ya "you are" na "your"!
· Next week your going…..hata mimi kidhungu sikifahamu, but this is too much!
· What ca I do…..? acha wajanja wawaibie filamu zenu kwavile mnafanya mchezo kwenye kazi, manake hii "ca" imetumika sehemu nyingi sana!
· Your doing good……au ndo mimi nisiyejua ninachoongea?!
· I can't leave in this life……eti nasikia kuna baadhi ya shule wanataka kufundisha kijeremani huku bado tukifahamu leave ni kuishi!

Sawa, Kiingereza sio lugha yetu, lakini utafanyaje masihara kwenye serious issues namna hii? Kwanini hiyo kazi wasipewe watu wanaofahamu lugha kidogo? Wahusika wa filamu hii ni miongoni mwa waigizaji wakubwa hapa TZ (Kuna Blandina, Dr. Cheni, kuna akina mama wawili ambao nao ni waigizaji wakubwa tu, kuna Aunt Ezekiel, Issa (nimesahau jina lake la kisanii, ila nazani ni m zanzabri huyu bwana kutokana na lafudhi na rangi yake, na ni muigizaji mkubwa tu); vilevile kuna binti mmoja mdogo ambae ambae ali-act kama Martha alipkuwa mdogo; zamani alikuwa mtangazaji wa kipindi cha watoto ITV, nae ni muigizaji mkubwa tu haya kama ni binti mdogo!Nimetaja wahusika hao kuonesha kwamba naamini waandaji wa filamu hi wababaishaji vinginevyo wasingeweza kuwa-recruit wasanii wakubwa hivyo! Sasa kama hivyo ndivyo, kwanini wameshindwa kuwa serious kwenye issue muhimu ya subtitles? NAJENGA HOJA!

Nadhani tukiiwekea font nzuri kama hiyo itakuwa friendlier!..( iam playing with forties dear!)
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom