Ilumine
Senior Member
- Dec 27, 2008
- 196
- 4
Asante mkuu, kwa kuniunga mkono hoja.
Kweli tatizo lipo, na tunatakiwa kukabiliana nalo.
Mtazamo wangu mimi ni huu, kwamba, filamu zetu nzuri kabisa, za kawaida, zenye mafunzo mazuri, zinaelekea 'kusiko'. Hizo filamu za ngono zinaeleweka wazi na tena kwa hapa Tanzania zinatazamwa kwa kificho. Sasa hizi zetu, za kawaida zinapenda kuiga mambo fulanifulani ambayo hayatakiwi kuonekana katika aina hizi za filamu za kawaida.
Ombi langu kwa wasanii wetu, ni hili: wajitahidi kuheshimu utamaduni wetu.
Dada mmoja alikuwa akitazama filamu mojawapo, pembeni yake alikuwa na mdogo wake wa kiume. Nilimwuliza ilikuwaje...akaniambia kuwa ilimblazimu mdogo wake huyo kuwa na busara; wakati fulani alijifanya kama vile anasinzia. Kijana alijisikia aibu kukaa na dada yake kutazama ile filamu.
Thanks!