FikraPevu: Waziri Chami ajibu mapigo sakata la TBS Bungeni

Chami kazunguka sana kwenye maelezo yake. Ila nilivyomuelewa ni kwamba matatizo yapo kwa JK kuchagua watu wabovu kuongoza mashirika na bodi zake, kisha anakua mzito kutoa maamuzi pale anaposhauriwa awawajibishe.
Hata ikija cabinet nyingine mpya kama baba ni yule yule ni kazi bure tu.
Wacha niendelee kunywa bia yangu
 
hapa tatizo ni ulaji tu....Chami inawezekana hana dhambi ila wako ambao wanaona wamekosa kupata tenda za ukaguzi mizigo pre inspection basi wafanye majungu..wote ukweli wanatetea matumbo..tumekuwa wabinafsi sana watanzania.
tatizo kubwa ni kuwa pre-inspection imefanywa kuwa ni njia moja wapo ya mapato lengo kubwa ni mapato na sio kukagua bidhaa zinazokuja Tanzania ,tumeweka mbele zaidi serikali itapata kiasi gani kutokana na ukaguzi huu, hivyo lengo kuu ni pato.
kutokana na lendo kuu ni kuwa liwe pato kwa taifa kampuni zilizo chaguliwa hazifanyi kazi hiyo badala yake wanakubandikia sticker ya ukaguzi bila ya kukagua kama ni gari ama chakula , hatimae tunaletewa samaki kutoka japan , mara vifaa vibovu vya umeme nk.
asilimia 25 inayochukua serikali ni kubwa sana kama tu hawa wakaguzi wangekuwa wanafanya kazi yao sawa sawa, kwni gharama ni kubwa za ukaguzi na unahitaji vifaa vya kisasa kungamua uchakachuaji.
 
Mimi sioni kosa la ndugu chami ....kwani kwa maeleZo Yake ni kuwa bodi za mashirika ya umma ndio zenye mamlaka ya kushauri ..hatua za kinidhamu.......hajakataa kuchukua hatua ..ila anasubiri hatua zikamilike na hataki kukurupuka.....Nampa pole sana...ndio madhara ya kufanya kazi na rais msanii....kwake kuwatoa sadaka watendaji wake kwa mamlaka zilizo mikononi kwake imekuwa kawaida.....
Mnakumbuka waziri diallo aliondolewa barazani kati ya mambo aliyokuwa akilaumiwa ni kumfukuza kazi mkurugenzi wa idara ya wanyaama pori bila kupata kibali cha ikulu......kilichotokea ni nini....Yule mkurugenzi Alimgomea waziri ....na aliendelea kwenda ofisini wakawa wanapishana kwenye korido kwa karibu miezi miwili ...hadi taratibu za kumuadjibu zilipokubaliwa na hakufukuzwa Bali alipelekwa kuwa mkuu wa chuo mwika....

Fedheha hii ya kuogopa kuhitilafiana na mamlaka za uteuzi zilimkuta Pinda .....alipotamani kumfukuza kazi Jairo na asifukuzwe....akajifunza lilipokuja suala la mama Nyoni ...Pinda aliziba MDOMO wake...

Ifike mahali rais ache kuwatoa kafara watendaji wale........yeye pekee ndio mwenye uwezo wa kumsimamisha kazi mtu wakati wowote ...bila kulazimika kutoa sababu na simply akasema kwa manufaaa ya umma....kwenye tawala zilizopita habari Kama hizo zilikuwa maarufu taarifa za habari za saa Saba mchana....au mbili usiku..utasikia simply ..."dar es salaam....rais wa JAMHURI ya muungano wa Tanzania......Leo amemsimamisha .....kazi kwa manufaa ya umma ...kupisha uchunguzi.",,.."hakuna tarifa ya ziada iliyotolewa na ikulu." ......hii ni nguvu ya rais...yeye haitumii anataka mawaziri ambao hawana nguvu ya namna hiyo labda waamue kutumia ile staili ya Mrema enzi zile....ambayo inafaa tu pale nchi Inapokuwa chini ya mapinduzi ....na hiki ndicho kilichofanya mawaziri chini ya msuya wakamwambie Mwinyi hawawezi kufanya kazi na Mrema Kama naibu waziri mkuu.....

Nadhani rais anahusika kwa kiasi kikubwa na huu mchezo unaoendlea kwani sio Siri anayo mawasiliano makubwa sana na Chadema ie Zitto na Mbowe ....na hata Slaa......na anaweza kupenyeza Siri za namna hii indirect .......ili kuwapa wananchi ya kuongea .....ili kusogeza siku..,lakini kimsingi anawajenga Chadema na Kukimaliza chama chake .....na siku akikabidhi madaraka ...wana ccm wenzake watamfuata Msoga ........kumlilia kwa kukiangamiza kabisa chama ccm...na asilani wakimuacha.

Madraka makubwa ya Raisi ndo tatizo haya ni mambo ya kuyajadili kwa mapana na marefu ili upuuzi huu usirudie tena kwenye Katiba Mpya,mtamrundikiaje mtu mmoja madaraka yote hayo? Ndiyo maana Raisi anakuwa kiburi kwasababu anajua hakuna cha kumuwajibisha tusubiri Uchaguzi 2015:
 
All in all Chami is one of the ministers with integrity ......kama ameamua kuondoka wacha tu aondoke ...ukweli utakuja kumuweka huru,,.....ni ngumu sana kufanya kazi na usanii unaoendelea serikali hiii.
Nilitegemea watu kama Ngeleja na Adamu malima wawe wa kwanza kuondoka..kuokoa serikali

jaman wakuu hii ni too much kwan mawaziri ni vivuli tu hawana meno kabsaa. We kila kitu kaweka rais sasa hadi awatimue mabest zake ni lin. Just imagen hata kenya hawatak bidhaa ze2 ni akil au mav. Huyo ekelege ye kuzurura na v8 na wezi wengne wanaptsha uozo bandarin. Jaman rais apunguziwe madaraka iko ck utakuta halmashaur zetu kapewa mwarab kisa jamaa wameshindwa kulipa la magar mabov ya serkal.
 
Hivi kuandika maelezo marefu ndio kujibu mapigo nadhani kujibu mapigo ni kung'atuka tu.
 
Huyo muongo na maana anachukiwa na ofisi ya spika pamoja na kamati.
Kutopata hizo nyaraka ni sababu tosha ya kujiuzuru kwani hajui kazi.anataka tuamini kuwa ofisi yao inachukiwa na CAG?
Harafu hizi bodi zote ni za kizushi sinateuliwa ki siri mno sifa wala hazijulikani.
Maoni yangu yeye apishe wanao jua kazi wafanye
mbona barua ya kumutaka kumusimamisha mukurungenzi alipewa na vyombo vya habari vinayo.
Nashauri hivi riport ya CAG iwe inapelekwa mahakamani moja kwa moja huyo jamaa hayo maneno inatakiwa ayatolee huko aone cha moto swali ni moja tu wewe unajua job description yako?
 
Back
Top Bottom