FIKRA PEVU: Slaa afufua ufisadi EPA na rada, awabana Kikwete, Mkapa, DPP

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amefufua upya tuhuma za ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), huku akiwalaumu Rais Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa chanzo cha kutochukuliwa hatua mafisadi.

Dk. Slaa mbali ya kuwashutumu Kikwete na Mkapa, alielekeza shutuma pia kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Beno Ndulu, akisema kuwa chanzo kikubwa cha Watanzania wengi kuwa masikini wa kutupwa, huku mafisadi wakiachwa wakimiliki uchumi mkubwa na kujenga majumba nje ya nchi.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema ambaye alikua mgombea Urais wa chama hicho mwaka 2010, ameshutumu vyombo vya dola na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Dk. Elieza Feleshi akivituhumu kwa kushindwa kumkamata na kumfikisha mahakamani, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Adrew Chenge, aliyehusishwa na tuhuma za rushwa iliyotokana na ununuzi wa rada nchini Uingereza hasa baada ya kukutwa na mamilioni ya fedha katika benki za nje ya nchi.

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo Jumapili Machi 17, 2012, alipozungumza kwenye kongamano la wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT), lililofanyika katika maeneo chuo hicho Nyegezi, Mwanza.

Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Slaa amesema Rais Kikwete na Serikali yake ameshindwa kuwasaidia wananchi wake katika kudhibiti mifumuko ya bei, pamoja na kushuka kwa uchumi wa nchi.

Kwa sasa nchi ipo pabaya sana, uchumi wa nchi umeshuka sana duniani. Ukiangalia Tanzania tulianza pamoja kiuchumi na nchi za Singapore na Malaysia.lakini kwa sasa nchi hizi zimetuacha mbali kiuchumi.

Tanzania kwa sasa inashikilia nafasi ya tatu kwa umasikini duniani. Na ndiyo inayoongoza kwa wananchi wake kuwa masikini katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC). Tunataka mabadiliko, na mwaka 2015 Chadema imejipanga vema kushika dola, alisema Dk. Slaa.

Alisema, Rais Kikwete ameshindwa kutekeleza ahadi ya Serikali yake ya kutoa fedha za kutosha kwa kila mwanafunzi na kwamba fedha nyingi zimekuwa zikiishia kwenye safari za Rais. Alisema hadi sasa amefikisha safari 325 tangu achaguliwe mwaka 2005.

Mbali na hayo, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kujitokeza hadharani kueleza fedha za EPA zilizopelekwa, kwani hakuna akaunti ya fedha hizo iliyofunguliwa na kuwekwa kwa fedha hizo, wala Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), na Bunge hawajui zilipo.

Rais alilitangazia taifa kwamba mafisadi wa EPA wamerudisha fedha walizokwapua. Fedha hizi hakuna akaunti zilipofunguliwa, CAG hajui na hata Bunge na wabunge wake hawajui hizo fedha zipo wapi, alihoji.

Katika hatua nyingine, aliishutumu Serikali ya Rais Kikwete kuwadanganya Watanzania juu ya mradi wa Kilimo Kwanza, akisema mradi huo umeasisiwa na watu fulani kwa maslahi yao, na alimuomba kiongozi huyo wa nchi ajitokeze aueleze umma iwapo Serikali yake ilikaa kuandaa mradi huo na nani waliokaa na tarehe gani.

Hata hivyo, alimtuhumu Rais Kikwete kutumia Baraza la Mawaziri kuligeuza kama sehemu ya ulaji wa siasa, kwani alisharuhusu Gavana BoT, Beno Ndulu kushiriki vikao vya Baraza hilo, wakati Gavana huyo haruhusiwi kuingia Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa sheria.

Alisema kinachofanyika hivi sasa ni danganya toto juu ya uchumi wa nchi, na kwamba takwimu zinazotolewa na benki Kuu hapa nchini si sahihi, alihoji kwamba: Kama Gavana wa benki kuu anaingia kwenye baraza la mawaziri, anaenda kufanya nini kama si kupika takwimu za kiuchumi?. Takwimu za uchumi kukua kwa asilimia 6 zinatoka wapi?.

Hata hivyo, alisema amekamata barua ya Rais Kikwete aliyoituma kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF), alilishukuru kwa kuisaidia Tanzania kifedha, na alisema hali hiyo inadhihirisha kwamba Tanzania ilivyoshamiri kwa kuombaomba.

Kuhusu Mkapa

Dk. Slaa alimtuhumu waziwazi Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kwa kile alichokiita kwamba kaharibu mfumo mzima wa uchumi wa nchi, kutokana na sera zake za ubinafsishaji ambapo baadaye alilazimika kujimilikisha mgodi wa mkaa ya mawe wa Kiwira.

Mkapa alibinsfsisha mashirika, makampuni na baadaye aliamua kujimilikisha Kiwira. Huyu Mkapa ni mmoja wa viongozi walioiharibu sana nchi yetu hii, alisema Katibu Mkuu huyo wa Chadema taifa.

Hata hivyo, alisema Rais huyo mstaafu pamoja na Rais Kikwete wamevunja rekodi duniani kwa kuruhusu makampuni ya kuchimba madini nchini kujenga viwanja vya ndege katika maeneo ya migodi kwa ajili ya kusafirisha madini, jambo alilosema kwamba ni kutoa njia ya kuruhusu kuibiwa kirahisi kwa madini.

Tembea dunia nzima huwezi kuona nchi inayoruhusu mwekezaji kujenga viwanja vya ndege katika maeneo ya migodi yao. Kwa hapa Tanzania wenye migodi wameruhusiwa kujenga viwanja vya ndege ili wachukuwe kirahisi madini yetu na kuwaacha hoi Watanzania, hivi ni nchi gani hii? alisema Dk. Slaa.

Gavana Ndulu

Slaa alisema Gavana wa Benki Kuu ameshindwa kuwashughulikia watu wanaotengeneza noti bandia, na kwamba Gavana huyo alishakabidhiwa mtuhumiwa na mashine ya kutengeneza noti bandia, lakini hadi sasa ameshindwa kulifanyia kazi suala hilo.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Gavana Ndulu na vyombo vya dola wakiwemo Makamanda wa Polisi nchini na Mkuu wa jeshi hilo (IGP), wameonekana dhahiri kuruhusu biashara ya kutengenezwa kwa noti bandia, hivyo kuharibu kabisa uchumi wa taifa.

Kuhusu Chenge
Dk. Slaa alihoji sababu ya Serikali ya CCM kushindwa kumkamata na kufikisha mahakamani, Andrew Chenge kwa tuhuma nzito zinazomkabili za ufisadi wa mamilioni ya fedha zilizokutwa katika akaunti huko nchini Uswisi.
Chenge alikutwa anamiliki fedha nyingi sana huko nje ya nchi. Ushahidi ulishawasilishwa kwa DPP, lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya Chenge, alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa kwa nguvu zote.
Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma Mwanza.

Slaa afufua ya EPA na rada, awabana Kikwete, Mkapa, DPP | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 
maswali yako mheshimiwa yalishajibiwa na mkurugenzi wa takukuru bw.Hosea alipokuwa akiongea na maafisa wa marekani kuwa Rais JK ndiye tatizo la ufisadi nchi kwani yeye ni sehemu ya mafisadi wa nchi hii kumbuka issue ya EPA pesa zake ndio zilitumika kumuingiza madarakani
 
Ipo siku kitaeleweka tu! Yupo mwingine huko Nigeria alikuwaga governor wa jimbo la delta enzi za raisi aliyetangulia mbele ya haki naye alijichoteaga mihela kibao laikini sasa yuko lupango!
 
Kikwete alipokutana na kupeana mkono na Dr Slaa Ikulu Dar alidhani yamekwisha.

Issue ya Wizi wa Mabilioni Tanzania haijaisha na haitakaa iishe kwa sababu ndilo jambo namba moja liilo tuingiza katika vurugu kubwa za kiuchumi.

Wananchi tuko Bussy kutafuta riziki ya mchana na jioni kiasi kwamba hatuna hamu kabisa kuzungumzia masuala makuu yaliyo dhoofisha ustawi wa familia zetu.

Mtu unaamka asubuhi na kuingia katika mishughuliko ili tu kukidhi mahitaji ya mlo wa siku moja.

Kesho kukicha unaingia katika shughui hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi.

Moja katika masuala ya ovyo ambayo CCM wamefanikiwa Tanzania ni kuwaingiza Watanzania katika mzunguko wa ufukara wa mawazo na wa hali.

Nilisha msikia mtu akisema kusimama kidete na kupinga Uharamia wa CCM hakuwezi kuleta Ugali mezani wala chenji mfukoni.Mtu huyu anasahau kwamba ni Uharamia huo huo wa CCM ndiyo umefanya uwezo wa Mtanzania kujitoshereza mahitaji yake kuyeyuka na kumwingiza katika songombingo ya kufukuza shilingi.

Ni usingizi gani huu tulio lala kiasi cha kushindwa kutambua ni vipi hali zetu ni mbaya na za kwao ni njema za kunona kinguruwe???

Tumebaki kuchuuza bidhaa katika viambaza vya nyumba zetu huku tukiwaachia wageni wanao kingiwa vifua na Serikali ya CCM kufanya biashara kubwa kwa mitaji kutoka katika account za serikali yetu wenyewe.

Kwa mgeni mtaji ni ugeni na utapeli kidogo tu wa kimataifa.

Kuna mahabithi watakuja hapa na kudai suala a EPA lilishaongelewa.

Ni kweli tulikwisha ongelea mtaani kwa nguvu sana akini mpaka leo serikali ya CCM imeingia kigugumizi kuchukua hatua a kisheria. Ni vipi serikali ya CC itachukua hatua ili hali chama chake cha CCM kilichukua sehemu kubwa ya fedha hizo na kuzitumia katika kampeni. Ni vipi serikali ya CCM itachukua hatua huku Viongozi wake wakuu akiwemo MH Jakaya Mrisho Kikwete na Kijana wake Riz kufaidika moja kwa moja na wizi huo wa mabilioni.
Riz sasa hivi ni Tajiri sana wakienda sambamba na Mtoto wa Kambo wa MH BenMkapa.( Si unajua Mama Anna kabla ya Beni alikata mtaa na Basil Mramba na kuzaa mtoto)

Watoto wa Marais hawa wawili ndiyo wenye pesa nyingi na nyodo za nguvu sana.

Hii ni kansa mpaka Tuma inyofolewe ndiyo tutaweka mnyanga chini.
 
Sasa tumeanza kuzungumza lakini twende mbele zaidi; Kikwete, Mkapa, Chenge, Ndulu wote hawa ni CCM. Ni mazao ya CCM. Huwezi kutenganisha hawa na chama tawala.
 
I am wondering how is he able of launching assaults on others while he has failed to respond to fraud allegations directed at him by TUNTEMEKE? The defected priest should know better that those who live in glass houses do not want to hurl rocks at others. And unless he starts putting into practice what he discourses, his boldness will soon backfire to degrade him to a cowardice crook politician.
 
Samahani ulijifunza wapi kiingereza na mimi nikapate ujuzi kidogo? Maana wanikumbusha enzi za Mwita25.kiuhalisia hauna tofauti na mtoto wa kidato cha kwanza anayedhani kuongea kiingereza kila mahali kutamfanya aoekane mweledi na anayejua sana kumbe hajui kuwa kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine ambayo yapaswa kutumiwa kwa wakati maalumu inapohitajika, mahali palipo na mjadala wa kiswahili ni vema kiswahili kitumike. Uliyonayo wewe ni kasumba tu 'ukikua' tunaamini kuna siku utaelewa kuwa unachokifanya sio sahihi na kuacha.

Kuhusu mada kwa kukusaidia tu ni kuwa Dr Slaa alishatoa majibu kuhusu shutuma za Tuntemeke, sasa kama hutaki kukubali majibu yake sisi hatuwezi kukulazimisha. Mwenyewe umesema 'allegations', hakuna sehemu mmethibitisha mara zote mnaandika hapa shutuma na kutishia kuwa 'aje akanushe ili mthibitishe zaidi' lakini hakuna siku mmetoa ushahidi ila mnaandika tu porojo na ninajua kuwa nafsi zenu zinawasuta kila muandikapo uongo wenu.

Tukuambieni uongo wenu utapita tu na Dr Slaa ataendelea kuwa imara kila siku. Mbona yameshasemwa mengi juu yake na wananchi wanajua ni utungaji wa CCM, kama mwadhani mnaweza kuwafanya wananchi waaamini kuwa Slaa naye ni fisadi kama CCM mwajidanganya. Dr Slaa atabaki kuwa mwanasiasa aliyeweza kutaja ufisadi wa serikali ya CCM na wanaccm bila uoga na kutoa ushahidi.
 
utangulizi mwingiiiiii. Kumbe ulitaka kuandika kwa kiswahili tuu. Mbaaffffffffffff
 
utangulizi mwingiiiiii. Kumbe ulitaka kuandika kwa kiswahili tuu. Mbaaffffffffffff

Asante sana MSOMI, nakuhakikishia hapa JF hakuna MSOMI kama wewe!! Hivi una digrii ngapi vile!!?
Hongera sana mtoto mzuri kwa busara, hekima na adabu ulonayo sidhani kama kuna zaidi yako kwenye ukoo wenu!!
JF inahitaji watu kama wewe ili kutunza heshima yake!!
HONGERA SANA!!

I 'LL BE BACK.
 
Umetumwa? Sura mbayaaaaa.......
 
I am wondering how is he able of launching assaults on others while he has failed to respond to fraud allegations directed at him by TUNTEMEKE? The defected priest should know better that those who live in glass houses do not want to hurl rocks at others. And unless he starts putting into practice what he discourses, his boldness will soon backfire to degrade him to a cowardice crook politician.

Hiki nacho ni kiingereza kweli ?Hivi lowasa aliamua kuacha kwa kushinikwa do we call him a defected PM ? Je si kwamba Slaa aliomba kuacha kazi za upadre kwa wakubwa wake na akakubaliwa ? Nini maana ya mtu ku defect ?
 
Umetumwa? Sura mbayaaaaa.......

Kosa langu ni nini hadi unishambulie wakati nimekusifia tu!!? "Toto baya zuri kwa mama'ke!!" Bila wewe Jf hakuna MSOMI, adabu, hekima na busara!
Tafadhari zingatia sheria za Jf japo una phd ya matusi uliyorithishwa!! Hapa ni jukwaa la Siasa na si la mipasho!!
Sawa mrembo?

I 'LL BE BACK
 
I am wondering how is he able of launching assaults on others while he has failed to respond to fraud allegations directed at him by TUNTEMEKE? The defected priest should know better that those who live in glass houses do not want to hurl rocks at others. And unless he starts putting into practice what he discourses, his boldness will soon backfire to degrade him to a cowardice crook politician.

wewe mama TUNTEMEKE ni mzigo mkubwa sana hapa Jf.ONYO!!, Usiwe unapita hapa Jf kama bado uko kwenye siku zako za MP sawa bibi?.Hata msikitini haturuhusu wanawake walio kwenye cku zao kuingia wala kusogeza tu pua zao kwenye eneo la msikiti..Mwikoooo!!!.
 
Unamshukuru nani magwaaandaaaaaaaaa??????????????

no dought, no qns, ww ni sweety wa tigo..... acha ujinga, don't expose ur ignorance hapa, harlot.... Ww mke wa Wasira nn..? Dr. Slaa aliacha upadre baada ya kuitwa na Wazee wa Kiiraqw pale Karatu, tena kupitia CCM wakati ule 1995 na alimshinda Qorro kupitia kura za maoni za CCM kwa 80%, ila Qorro aliyekuwa mbunge wa Karatu alikuwa hapendwi kabisa na wananchi those days hakuna alicho fanya miaka mingi ya ubunge wake, Qorro akaenda
KUSEMA KUWA Dr. Slaa si mzoefu wa siasa na hajulikani CCM that was 1995, Dr. Slaa akatolewa na Qorro kurudishwa kugombea ubunge thru CCM, na Dr. Slaa aliyeitwa na WAZEE WA KARATU na ndio kisa cha kuacha upadre akaambiwa achague chama chochote agombee, ndio akaenda CDM, na akashinda kwa 90%, Qorro alikoswa koswa kupigwa na wananchi siku ya kutangaza matokeo kwani Polisi walisaidia sana, maana alipata like 7% ya matokeo ya kura yote,.
Sasa hapa Wasira anadanganya watu na U calling ur self swty wa tigo unakurupuka, ur such an asshole.....
 
Hiki nacho ni kiingereza kweli ?Hivi lowasa aliamua kuacha kwa kushinikwa do we call him a defected PM ? Je si kwamba Slaa aliomba kuacha kazi za upadre kwa wakubwa wake na akakubaliwa ? Nini maana ya mtu ku defect ?

ile thread nyingine ya ufisadi wa slaa sikuoni kule, njoo sisi wazee tumlinde slaa!!
 
Back
Top Bottom