Fikiria kabla ya Kutema Big G kwa karanga za kuonjeshwa!

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Wepesi wa kutema Big G (chewing gum)kwa karanga za kuonjeshwa huwafikisha watu pabaya jamani.

Mtu una mpenzi anakupenda kufa. Unakutana na mtu siku moja tu anakupagawisha unaamua kumtema mpenzi wako wa zamani kisa umeona mtu mpya - Acheni hizo jamani.Limempata rafiki yangu mpenzi. Mshaurini afanyeje? Je naye ateme chips-zege kwa mshkaki wa kuonjeshwa?
 
Kwani kuna ubaya gani?
kama big G yenyewe imeisha utamu na umepata karanga chache lakini nzuri kuna haja gani kujiumiza meno mda wote?

Mwambie ale,akichoka ahamie sahani ingine
 
Umenichekesha sana Speaker lol!

Utahamia sahani ngapi?
 
miye mbona nimechanganyikiwa; sasa mtu akionjesha ikiwa tamu asile? au ateme? Lakini, hata kama ni tamu lakini ya muda si ya kudumu inatosha kumfanya mtu aache chakula cha kudumu? Nadhani hekima ndio iko hapo.
 
Ulichokua unatafuna kwa muda wote na ulichokwisha gharamia ni Big G ambayo umetema!Hamu yako wewe ni kutafunatafuna muda wote.
Utaonjeshwa tu! Kama tamu uingie gharama kununua za kutosha.Na je ukikuta siyo tamu na Big G ulishatema utakula nini?
 
Hiyo Big G ya halali (ndoa) au na yenyewe ni chakachuwa(kimada)?

Kama hakuna ndoa ni uzinzi tu, wote sawa, big g na karanga zake, owa haraka.
 
Ulichokua unatafuna kwa muda wote na ulichokwisha gharamia ni Big G ambayo umetema!Hamu yako wewe ni kutafunatafuna muda wote.
Utaonjeshwa tu! Kama tamu uingie gharama kununua za kutosha.Na je ukikuta siyo tamu na Big G ulishatema utakula nini?

kwa kweli katika mazingira hayo nitajikuta nakula jeuri yangu!! Kwa hiyo, hata kama Big G imeshautamu we ongeza sukari tu? alimradi bado inavutika na kupulizika bado ni big G!
 
Sijui nisimamie wapi lakini tuamue kiutu uzima..ladha ya Big G na karanga ni tofauti so far,hivyo km ukitema Big G kwa karanga ya kuonjesha hakikisha unamganda aliyekuonjesha till fuko la karanga linakwisha then experience utakayopata itakusaidia kuonja na flavour ngingine!..Hilo tu!
 
Hapo kuna options mbili nzuri tu;
1. Unaeza tema bigG yako uigandishe mkononi kwa muda, then unaonja karanga zako kisha unarudisha bigG yako mdomoni!
2. Unaeza tafuna vyote pande tofauti za meno..ila hii ni risky esp. kwa bigG yako!
chagua moja..
Nawasilisha!
 
Anayekuonjesha anataka uhamie kwake na siyo kuendelea kuonja tu. Bado hujatoa suluhisho

Kuigandisha mkononi sijui kama kiafya ni sawa! Kutafuna zote kwa wakati mmoja ni hatari utachakachua! Utakosa vyote

Ngoja tuendelee lupokea mawazo
 
bakia na Big G kwani utamu wa asili hauishaji laza hata kwa karne nenda rudi
 
Kwani kuna ubaya gani?
kama big G yenyewe imeisha utamu na umepata karanga chache lakini nzuri kuna haja gani kujiumiza meno mda wote?

Mwambie ale,akichoka ahamie sahani ingine

...kwakweli. Unatafuna 'bigijii' mpaka taya linakuuma bana? kwanza 'bigijii' inaletesha njaa tu! :tape:
 
Anayekuonjesha anataka uhamie kwake na siyo kuendelea kuonja tu. Bado hujatoa suluhisho

Kuigandisha mkononi sijui kama kiafya ni sawa! Kutafuna zote kwa wakati mmoja ni hatari utachakachua! Utakosa vyote

Ngoja tuendelee lupokea mawazo

Bora kuinatisha mkononi au kwenye tendegu la kitanda hata kama uko tempted :noidea:. Manake karanga za kuonjeshwa nazo huwa ni mbili au tatu tu,lol!Kama anavyosema mkjj,kama bigijii inapulizika tu,ongezea asali (sukari ita-affect elasticity hehehe)
 
Karanga nyingine taaaam ajabu, kama zile tunazokula mtaani zinapitishwa kwenye kikapu, halafu za moto saaana
 
Back
Top Bottom