Fikiri tena, kwanini?

nkyandwale

Member
Feb 8, 2011
64
14
Ni jambo la kawaida kwa jamii ya kizazi hiki kumzomea kiongozi anayetoa hoja ambazo hazina mshiko na kujaa pumba kwao.

Hivi karibuni kiongozi, na mshika bango la elimu aliipata homa ya zomeazomea na akatoa jasho hadi alitamani kufuta jasho kwa koti lake huko Dariasalama na aliondoka chuoni pale kwa ulinzi mkali.

Kipigo na wembe ule ule umempata Mkuu wa shule ya sekondari x ambaye amepata uhamisho kwenda shule y katika manispaa ya Sumbawnga ailikataliwa na wanafunzi wa shule y mbele ya bodi ya shule. Wanafunzi hao walimzomea na kutamka kuwa hawamtaki kwasababu shule yake ipo chini ya kiwango kitaaluma.

Kama haitoshi wale wanapokea amri na kutekeleza hawakusita kuwasambaza wanafunzi hawo kwa vitoa machozi na kamasi. Timu yetu inaendelea kufuatiliya hatima ya tukiyo hilo, kwani hayo yametokeya mnamo majira ya saa kumi na mbili jioni ya Ijumaa jana.

Enyi na wanazuoni na wanataaluma, kwa nini mnaendeleya kuwaweka kwapani wasiwo na uwezo wa kuyamudu madaraka? Fikiri tena!
 
pengine naweza sema ni kuongezeka kwa upeo wa uelewa.Lakini kabda ya kufikia hapo kuna mambo kadhaa ya kujiuliza juu ya hilo Je ni kweli ni sasa tu ndio kumekuwa na zomea zomea au hata zamani ilkuwapo ila habari zilikuwa si rahisi kusambaa.Pili kama ni inshara ya ukomavu wa uelewa kwa vijana lakini mbona tunaendelea lalamika kuwa kiwango cha elimu kinashuka?uelewa unawezekana bila elimu?
 
Pili kama ni inshara ya ukomavu wa uelewa kwa vijana lakini mbona tunaendelea lalamika kuwa kiwango cha elimu kinashuka?uelewa unawezekana bila elimu?

hilo la msingi zaidi kujiuliza.
Mimi naona ni kushuka kwa nidhamu. Uelewa huambatana na nidhamu. Mwenye uelewa huwa na nidhamu na mwenye nidhamu huwa na uelewa.
Sasa kama msomi unaona kuzomea ndio umesuluhisha tatizo basi uelewa wako ni mdogo sana na nidhamu imeshuka kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom