FIFA na FBI kuna ushirika gani?

Kangambili K

Member
Jan 16, 2016
17
17
Naomba kujua wana jamvi. Hivi FIFA hua naona inakataza kupeleka migogoro ya michezo mahakamani. Sasa nikama miezi3 sasa naskia juuu shirika la ujasusi la Marekani FBI kufuatilia tuhuma za rushwa FIFA na vigogo kadhaa kutoewa akiwemo rais wa Fifa. Nataka kujua uhalali wa FBI kuichunguza FIFA unatoka wapi na je Si ndio maswala hayo ya serikal kuingilia mambo ya Soka au kuna namna ya siasa?
 
FBI kwa sasa inachunguza hela za rushwa ambazo viongozi wa FIFA walilipwa ama na mashirika ya kimarekani, yenye uhusiano na Marekani au pesa za rushwa walizolipwa viongozi wa fifa zilizopitia bank za marekani. Pia kama kuna raia yoyote wa Marekani aliyeshiriki Katika kupokea, kutoa au kutakatisha pesa za rushwa zinazohusiana na fifa
Hii ni baada ya kumfuatilia jamaa mmoja Mmarekani kwa muda wa miaka kadhaa na kugundua alikuwa ana husika na kufanya deal za rushwa na viongozi wa bodi ya fifa na huyo jamaa baada ya kubanwa aliwauza wenzake wakati wa kupiga kura za world cup 2018 na 2022 ambapo baadhi walichukua hela kutoka Russia na Quatar bila kujua FBI wametegesha
 
Tatizo aliyekuwa rais Sepp blatter kujenga urafiki na Putin ndio FBI ikaingia. Yani isengekuwa hivyo hadi Leo blatter angekuwa rais.
 
hili zengwe tu baada ya Blatter kuwanyima kuandaa fainali nne za kombe la dunia(S.A Brazil Russia na Qatar) ndo visa vikaanzia hapo akiwa na mshirika wake mkuu uingereza.
 
FIFA - -Shirikisho la Mpria wa Miguu Duniani

FBI - Shirika la Upelelezi la Marekani.

Hakuna mahusiano.
 
Back
Top Bottom