Fid Q vs Jo Makini

kuna haja likaandaliwa shinmdano moja wapande live jukwaani washindane
 
Joe Makini A.K.A Mwamba wa kaskazini...... Jamaa tuko zake ni kali mno tofauti na Fid Q ambaye anajifanya mmarekani!
 
Hao mabwana wote ni "wakali", na kwasasa ni kama mafahali wawili wasiopikika, kila mtu anakitaka "kiti".
Tatizo lao kubwa wote wanaimba kitu wasichokiamini, matokeo yake ni hawana hadhi sana mbele ya wafuatiliaji wa "real hiphop"

Kwanza wote wanalegeza sana, hawakazi kama ilipokuwa pale mwanzo mfano, msikilize Fid Q wa kipindi kile yupo na "heartfull Dodgerz" ie (wakina mapacha, Big 4 the geez, spado J, J murder na Sqeezer) huwezi kumlinganisha na Fid wa saiv. Joh makini wa saiv huwezi kumlinganisha na Joh makini wakipindi kile cha "hawapendi", "hao" kipindi hicho anatolewa na Prof Ludigo.

Kuthibitisha hilo, Fid Q alimkana mwanae wa toka enzi za utoto "Kiraka Rado".... hili lilinithibitishia u-blazameni wa Fid kwa kiasi kikubwa sana,

Kwenye Track ya "hao" Joh Makini aliziponda sana Tuzo za kill, na baadae alikataa hata kushirikishwa kwenye hizo tuzo ila baadae kuthibitisha kuwa alikuwa hajui anachopigania na wala alikuwa hajui anapigana na nani akageuka kuwa mpiga debe wa hizo tuzo tena hadi kushiriki kwenye ule wimbo mbovu wa "kill all star 2010".

Hoja kuu ya utetezi marazote imekuwa eti wasanii wetu ni njaa, hiyo kweli! Lakini huwezi kujiita mwanaharakati wakati hujazijua changamoto za hizo harakati zako, kwahyo hapo ni bora anyejitambulisha kama yeye ni **** toka mwanzo na akabaki na ufala wake hivyohivyo, kuliko hawa wanafiki.

Wote (Fid na Joh) wanataka tuwatambue kama ma-legend wa hiphop ya bongo, wakati hawana mpango unaofahamika wa kuacha legacy yoyote. Wameingia kwenye game wamakuta "hiphop haiuzi" ndio msemo unaokandamiza kazi zao, na wao wamejiunga kwenye huo wimbo eti kwa kususia kutoa album au kuzisambaza wao wenyewe kitu ambacho hakijaonyesha ukombozi kwa wadogo zao,

sawa basi wao wameshindwa kuanzisha harakati hizo za kimapinduzi ya soko lakini je wametoa support gani kwa wanaofanya hizo harakati mfano wa Sugu (au hata Kala Pina aliwahi kujaribu), si Joh wa Fid waliowahi kuunga mkono hizo harakati za hao watu kwa wazi wazi, wanogopa watabaniwa na watakula wapi..... ndio jibu! Basi hamna mkali hapo ni waganga njaa tu kama "bongofleva" wengine.

Ok msije mkaniambia natoka nje ya mada, lakini ni bora tufafanue vitu kwa undani japo kidogo katika kuonye kitu bora zaidi kuliko kushabikia kishabiki kila kitu unacholetewa.

Kwa kurudi kwenye swali, umezungumzia ukali katika maeneo ya "style", "lyrics" na "ryhmes".
Kwa sababu hawa ni watu ambao wametokea kwenye upenzi wa ndani sana wa hiphop, hivyo vitu wote wanavyo japo Fid ana-added advantage sababu ni anasoma sana vitabu hivyo mara zote anaonekana kumzidi Joh.

Papo hapo Joh anakitu "elimu ya mtaa" ambayo ni kitu muhimu sana kwenye hiphop, ndio maana mistari ya Joh inagusa sana watu wa mtaa, pia binafsi Joh amekuwa ananikuna sana coz marazingine amekuwa sio muoga kuuchana mfumo husika anaoona haujakaa poa ie "wasomi bado watumwa kwa wanasiasa....."track ya karibu tena kwenye show za joh".

Lakini ili kuutendea haki huu mjadala nadhani tungeangalia pia wanavyomeet "5 mic" kama element kuu za hiphop, wote wanapwaya sababu kuna makosa mengi yanatokana na mfumo wetu wa kimuziki, hivyo nyimbo zao zinakosa element za "dj", "graffit" na "black dancing"

Mwisho nimalizie tu kuwa hawa majaa kwangu hamna mkali ni wa kawaida sana ukiingia kwenye content ya track zao, wanaimba vitu vyepesi sana, nadhani nimeathirika na kusikiliza watu kama wakina;
"Hashimu Dodo (Bongo psychological)", "Salu-T", "Kwanza unit (Zavara na wenzake)", "Magazijuto", "Himamu Abas (underground souls)" "Kurasa", "A-bass", "Solo thang"...... hii kwa bongo tu, sasa ukisikiliza watu wa mtoni kama "Gangstarr (Guru), Rakim, Jeru, Nas, Rza na Gza, Pharaoh, Roots, Blackstar, Canbus nk nk nk..."

kwa sasa kuna vijana wanoka kwa "Duke", One, Stereo, Mpita, Nick Mbishi.
Mtaa bado una azina kubwa sana, wanaosema hiphop ime/inakufa inabidi wajikaze sana!
 
Joe Makini A.K.A Mwamba wa kaskazini...... Jamaa tuko zake ni kali mno tofauti na Fid Q ambaye anajifanya mmarekani!

kwani joh makini yeye anajifanya Mtanzania, na umetumia vigezo vipi kuongea hivyo, hata hivyo Asili ya hip hop ni Marekani, ndio maana fid q unamuona kama Mmarekani vile.
 
Namkubali the Don, aka Ngosha,
Kuna wakati Clouds waliwapambanisha Joh akaibuka kidedea, alipoukizwa inakuwaje ameshindwa kwa mara ya pili na ktk gazeti la kita ngoma alijibu hivi "inawezekana natumia nguvu kuwaelekeza watu sehemu nawao badala ya kuangalia ninapo elekeza wanaangalia kidole changu ninachoelekezea au pengine natumia sanaa ya ndani sana hivyo hawanielewi"
 
kibongo bongo mara nyingi ukali wa mtu hupimwa wakati ana hit songs wakati wa sasa ila kama unataka kuchukua tracks zote za nyuma mpaka sasa ni dharau kubwa sana kumfananisha Ngosha The Don na Jo....ila kwa yule aliyeenda off topic na kumuingiza Jay mo...anajua anachokisema!the boy upo katika level nyingine na utamtaka ubaya umpe shavu umsikie anavyoenda na topic...msikilize Jay mo ukisikia paa!na katika pini la N2N ndo utajua tofauti yake na watoto kama kina joh makini ambayo lyrics zao kila mstari hauna mantiki na mstari mwingine na neno mimi ndo linatawala katika verses zao....
 
FidQ anabaki kua msanii bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania kuanzia mashairi mpaka flows style...watanzania tatizo letu kubwa hatukai tukaskiliza mziki tunajua kuropoka ovyo bila kupima nawaombeni muende mkae chini msikilize nyimbo hizi afu nambieni nan mkali PROPAGANDA vs KARIBU TENA.,SWAGA DON vs KILIMANJARO...,AGOSTI 13 vs HAO....,MWANZA MWANZA vs NIaJE NI VIPI.... SHiMO LimEtEMa vs CHoCHOTE POPOTE
 
Daah sikuiona hii... naona mtu mzima Bello unaiangalia kwa mbali..

Gwalu umesema vyema sana lakini hujataka kutuambia ni nani unadhani yuko juu ya muashoki kati ya hawa wawili.

Kwa upande wangu mimi punch lines za Fid nazikubali sana sana. Kuna mdau amesema inawezekana mistari ya Fid mingi inatoka vitabuni, Mimi naamini Hip Hop ni harakati na kama unakua na artist ambao wanasogea mbele zaidi na kuzama vitabuni kisha kutuletea falsafa ni kwa nini tusipige saluti kwake.

Joh ni mkali lakini hana mistari ambayo unaweza sema kweli hapa hip hop imelala isipokua ana style. Kamwe Joh kwa mwendo anaotembea sasa hivi hatomuweza Fid. Ukisikiliza albam ya propaganda ya Fid utagundua huyu jamaa ni mbunifu, msomaji na ni fanani.

All in all hii kitu inayotengenezwa pale M lab ( Duke, Gondwe Brothers big up).. ambako unakutana na Niki Mbishi, Stereo, Goppela etc italeta mapinduzi ang'avu katika ulimwenngu wa hip hop
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom