Ficha na kufichua mafaili kwenye Windows 7 na XP(Hidden files)

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
Kwa Video ya Mada hii Tembelea HAPA


Source:AfroIT.com

Ufanyaji kazi wa mitambo endeshi(Operating Systems) unafanana sana na ule wa mwanadamu,kwa mfano,wengi wetu tumezoea au kuwa na tabia ya kutenganisha mambo yetu.Kuna baadhi ya mambo ni binafsi(siri) ambayo
p_2441513.jpg
hakuna mtu anayetakiwa kuyajua au kuona wakati mengine huwa yanakuwa wazi kwa wenye mamcho waone na wenye masikio wasikie.Hii inasaidia sana usalama na usafi katika maisha.Si umewahi kusikia "Jamaa ni msafi,hana scandal".

Hii ni sawa na kwenye kompyuta,ndani ya kompyuta kuna aina mbili ya mafaili,kundi la kwanza ni yale yanayotumika na mtambo endeshi wakati kundi la pili ni yale yanayotumika(wa) na mtumiaji.

Sasa ili kuhakikisha hakuna mvurugano wa mambo,kompyuta huficha mafaili yanatumiwa na mtambo endeshi ambayo mtumiaji hana haja kubwa kushughulika nayo,nimesema hivi kwakuwa,kuna baadhi ya mafaili ya mtambo endeshi haswa yale yanayopatikana kwenye mzizi ambapo mtambo umesimikwa huwa yanaonekana,hii ni kwa sababu kuna wakati mtumiaji huitaji kuwasiliana na sehemu za ndani za mtambo endeshi kwa ajili ya mabadiliko kadhaa.

Kutokana na kitendo cha kompyuta kuficha baadhi ya mafaili ya mtambo endeshi,hali hii huweza kuathiri hata baadhi ya mafaili ya mtumiaji,ndio sababu kuna wakati unaweza ona baadhi ya mafaili yako hayaonekani na kuanza kupanic,nani ameyafuta.

horoscope_compatibility.jpg
Kuna sababu nyingi mbazo zinaweza kupelekea hili,zikiwmo kushambuliwa na virusi au minyoo,vilevile baadhi ya mabadiliko ambayo hufanywa na mtumiaji hupelekea muitilafiano na utendaji wa kompyuta kitu kinachopelekea kompyuta kulificha hilo faili.Hii hutokea sana kwenye kamera na usb.

Sasa baada ya kuongea kwa sana juu ya sababu na mtindo mzima wa ufichaji wa mafaili,sasa tuangalie ni jinsi gani unaweza kuficha au kufichua faili kwenye kompyuta yako.Nitakuelezea kwenye mitambo endeshi ya aina mbili,nitaanza na Windows 7 halafu nitamalizia kwenye Windows XP Professional.

1.Kuficha na kufichua mafaili kwenye Windows 7


Katika Windows 7,mpangilio wa mafaili kidogo umetofautiana na matoleo ya zamani,mambo yamekuwa rahisi zaidi.Ili kufanikisha hili fuata hatua zifuatazo.

i) Fungua MyComputer au faili lolote lile kwenye kompyuta,juu kabisa kushoto chagua Organise,kisha chagua "Folder and search options".

organise.jpg


ii) Kutafunguka kidirisha kipya,bonyeza sehemu iliyoandikwa "View".

view.jpg


iii) Ukishabofya View,kutafunguka kajisehemu kingine ambacho kina vijiboksi kibao,sasa angalia kijiboksi kilichoandikwa "Hidden files and Folders",kibofye mara mbili(double clicks).

clicks.jpg



MUHIMU: Hii ni kwa wale ambao kilikuwa hakijafunguka,kama kilisha funguka basi huitajiki kufanya lolote na ruka kwenda hatua ya chini.

iii)Baada ya hatua ya tatu,au kama kilikuwa kimeshafunguka,utaona machaguo mawili moja ni "Don't show hidden files" na lingine ni "Show hidden files" utachagua chaguo ambalo unalitaka.Lakwanza ni kama unataka kutoyaonesha mafaili yote yaliyofichwa wakati la pili ni kinyume chake.

show.jpg




2.Kuficha na kufichua mafaili kwenye Windows XP


1) Kwa wale wanaotumia windows XP,hatua zinafanana sana na zile za Windows 7,isipokuwa hatua ya kwanza kwenye windows XP unatakiwa kwenda kwenye Tools->Folder Options badala ya organise kama ilivyokuwa kwenye Windows 7.


tool%20option%20XP.jpg


ii) Kwenye hatua ya pili,na kuendelea zinafanana kwa silimia tisini na tisa kama kwenye Windows 7 isipokuwa uonekano,utaona kwenye windows XP kuna vitu vimeongezeka mbele ya view,ila kwa sasa achana navyo.

view%20XP.jpg


Muhimu: Hatua zinazofuatia zote zinafanana na za kwenye Windows 7,hivyo baada ya kukamilisha hatua ya kwanza kwenye Windows XP,fuata maelekezo ya kwenye Windows 7 kwa hatua zilizobakia kwani ni mulemule.

Kuondoa au kuingiza faili husika kwenye maficho.


Hadi sasa nimekuelezea jinsi ya kuondoa au kuficha mafaili yote kwenye mficho,sasa chukulia mfano sitaki kufichua mafaili yote kwenye kompyuta,ila nataka kuondoa faili moja lisiwe kwenye mficho,nitafanyaje?
Kufanikisha hili au kinyume chake(kuficha faili moja) ni rahisi mno,chukulia unataka kuondoa faili moja toka kwenye mficho(kulifanya lionekane),unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo.

i) Fichua mafaili yote yaliyopo kwenye mficho kama nilivyokuoelezea hapo juu

ii) Nenda kwenye faili au folda unalotaka kulificha/fichua,bonyeza properties.

iii) Kutatokea kidirisha kipya,chini kabisa utaona kuna sehemu iliyoandikwa "Hidden". Sasa basi kama unataka kuficha faili basi weka alama ya vema na kama unataka kuliondoa toka mafichoni ondoa alama ya vema.

hidden.jpg

Hadi hapo utakuwa umemaliza kuficha au kufichua faili toka mafichoni kiurahisi zaidi.
Je umeipenda makala hii? Mtumie rafiki yako kwa kubonyeza kicha za juu.
 
Kama tukishirikiana kwa pamoja tunaweza,kwani ukiuangalia kwa undani utagundua kuwa hatuna contents za teknolojia kwa kiswahili hii hupelekea utata wa kujifunza kwa wote,tumezamilia hili.Tunaenda kwa hatua tukimaanisha hadi tunamaliza hatua ya mwisho basi tutakuwa na mada za kutosha.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom