FFU wamvamia dereva na kuangusha daladala likiwa na abiria; mh Kombe tutafika ?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,872
21,950
Askari wa ffu arusha wamevamia gari moja mjini arusha
na kuanza kumchapa makofi dereva kabla ya kuanza kushikilia
msikano na kuaangusha gari kwenye mtaro....
Gari hilo t636 awx ilitokea leo hii....dereva wa gari anasema
alifika kituoni akawakuta maaskari watatu...akasema jamani kuna nafasi ya mmoja imebaki kusimamisha siwezi alipakia mmoja akaondoa gari yule aliengia ndani akapit mpaka kwa dereva na kuanza kumchapa makofi kwa nini amewacha wenzake...baadaye akangangania sterling ya gari likaangukia mtaroni

je mh kombe ni haki kweli wahuni kama hawa kuwepo jeshi la polisi

more info
angalia taarifa ya habari saa tano kamili itv
 
dawa ya hawa ni waanze kusomewa mashtaka. Tatizo ni moja, polisi ndo wasoma mashtaka. DUH! Jela inaendeshwa na wao. DUH! Kweli tupo mbali na maendeleo
 
Siyo kweli kwamba polisi ndio wanaoendesha mashtaka. Siku hizi polisi hawaendeshi mashtaka kwa sababu mtu huyohuyo hawezi kukufungulia mashtaka na kuendesha mashtaka. Siku hizi ni mawakili wa serikali ndo wanaendesha mashtaka Kama umeshika namba ya huyo askari itoe tuifanyie kazi.
 
Inasikitisha sana wasimamia haki ndo hao hao wavunja haki na tunaendelea kuwakumbatia.
 
askari wengi ni wavuta bangi kitendo alichofanya huyo afande ni cha kulaaniwa please sheria za jeshi zichukue mkondo wake
 
Haya mambo yanajitokeza sana, kwani wanajiona wao ndo wenye haki zote. Wakati mwengine wanaweza kukusimamisha na kukulazimisha uwapeleke watakako wao bila kufikiri kama ulikuwana shughuli zako, ukikataa basi ndo kibano kinaanza na penginepo unabambikizia kesi. HAWA ASKARI WA TZ WAMEKUWA KAMA OMBAOMBA WA LIFT. HIVI SEREKALI HAIJAWEKA UTARATIBU WA USAFIRI KUFANIKISHI MAJUKUMU YA HAWA WATU?
 
Mi nadhani suluhisho la uharamia huu ni askari kulipa nauli. Huwa sipati jibu napojiuliza ni sababu gani zinazomfanya askari asilipe nauli wakati analipwa mshahara kama watanzania wegine. Mwanafunzi alipe mfanyakazi asilipe, how?? Askari huyo huyo anampa mwanaye nauli, yeye anapanda bure!! Nahisi kuchanganyikiwa na hii serikali yetu.
 
Siyo kweli kwamba polisi ndio wanaoendesha mashtaka. Siku hizi polisi hawaendeshi mashtaka kwa sababu mtu huyohuyo hawezi kukufungulia mashtaka na kuendesha mashtaka. Siku hizi ni mawakili wa serikali ndo wanaendesha mashtaka Kama umeshika namba ya huyo askari itoe tuifanyie kazi.

source mh? Ni sheria ipi imebadilisha hili?
 
Mi nadhani suluhisho la uharamia huu ni askari kulipa nauli. Huwa sipati jibu napojiuliza ni sababu gani zinazomfanya askari asilipe nauli wakati analipwa mshahara kama watanzania wegine. Mwanafunzi alipe mfanyakazi asilipe, how?? Askari huyo huyo anampa mwanaye nauli, yeye anapanda bure!! Nahisi kuchanganyikiwa na hii serikali yetu.

kwani kuna sheria inayokataza askari kulipa nauli au ndio uoga wa makonda kudai nauli?au labda ni ubabe wa askari?
 
hawa askari wanajua nidhamu na sheria za kazi zao?wanalinda usalama wa raia au wanalinda maslahi yao?inabidi sheria ifuate mkondo wake bila kuegemea upande mmoja
 
hatutaweza kuvumilia upuuzi kama huuu....baya zaidii askari wanaonyeshwa wako peace kama dk 2 zijazo wanaenda kumwona RAIS awaboreshe maisha yao.....
ama ndio ile ATI FFU NI WALE VIPOFU WA SHULE YAANI DARASA LA SABA NDIO WANAMISHIWA KULE WAKAWE WAKATILI ZAIDI.....mmmmhhhh kazi ipo
 
Askari wa ffu arusha wamevamia gari moja mjini arusha
na kuanza kumchapa makofi dereva kabla ya kuanza kushikilia
msikano na kuaangusha gari kwenye mtaro....
Gari hilo t636 awx ilitokea leo hii....dereva wa gari anasema
alifika kituoni akawakuta maaskari watatu...akasema jamani kuna nafasi ya mmoja imebaki kusimamisha siwezi alipakia mmoja akaondoa gari yule aliengia ndani akapit mpaka kwa dereva na kuanza kumchapa makofi kwa nini amewacha wenzake...baadaye akangangania sterling ya gari likaangukia mtaroni

je mh kombe ni haki kweli wahuni kama hawa kuwepo jeshi la polisi

more info
angalia taarifa ya habari saa tano kamili itv

nchi yetu nzuri sana hii, mwenye nguvu mpishe apite, ila na sisi sijui tunajua sana sheria au upole mimi hata sielewi, kwanini abiria wasingemkamata huyo askari nao wamchape na kumpeleka polisi? Hata kama angeachiwa na polisi wenzie lakini angalau abiria wangekuwa wamefanya jukumu lao. Nadhani baadhi ya abiria walikuwa wanacheka ukute!
 
Back
Top Bottom