FFU Kumburuza Mwanafunzi anayevuja damu nyingi kwenye karandinga Je ni halali

Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,768
3,232
Machozi yamenibubujika nilipoona kwenye taarifa ya habari ya ITV saa mbili kwa askari wa FFU waliokuwa chuo kikuu wakimburura kijana ambaye wa kiume alikuwa anabubujikwa damu kichwani sijui kama yuko hai mpaka sasa manake alionyesha ameishiwa nguvu ameshikwa huku na huku akilazimishwa kutembea huku damu zikimvuja kwenye paji la uso
Nauliza IGP Mwema anaamini kweli haki ya wanafunzi kunyimwa mikopo na majambazi wa serikali ya CCM ni halali
IGP Mwema bila aibu anaitisha mkutukano wa kusafisha jeshi la polisi huku askari wake wa FFU wakitaka kuuwa mwanafunzi anayedai haki yake kwa njia ya maandamano bila silaha
IGP Mwema ni mzazi kwa vile watoto wake na wa shemeji yake Kikwete wana pata kila wakitakacho ndio maana anaona watoto wengine hawana haki ya kudai haki yao
Mkuu wa chuo Mkandara angekuwa mtoto wako anaburuzwa akitililikwa na damu nyingi kiasi hicho ungefurahi
My Take
Nawaombeni watanzania popote mlipo mukatae udhalimu wa jeshi hili la polisi linalouuwa wananchi kila siku acheni wanafunzi watoe kilio chao cha maana yanini munawaua na kuwatia vilema vya maisha huku watoto wenu mukiwasomesha na kuwatibia ulaya
 
Hivi Kwa nini hakukimbizwa kwenye Zahanati ya chuo enyi nyie polisi waauaji mnaotumiwa na chama cha magamba mutakuja kujuuta siku moja munatumika
 
Thanks God umeniepusha na laana ya kuwa Polisi wa Tanzania wanaotumiwa na mafisadi kukandamiza haki za wanyonge bila aibu!! Huyo mwema anafikiri kwa kutumia tumbo baasi!!
 
froida hujaona picha askari kumi wanamshikilia msichana 1 ud angalia Myinka blogspot
 
Kuwa Polisi au FFU ...Hukuwapi uwezo na mamlaka ya Kuudhalilisha Utu na Ubinadamu wa Mtanzania!!
 
froida hujaona picha askari kumi wanamshikilia msichana 1 ud angalia Myinka blogspot

Duh nimeona hiyo picha inasikitisha nchi gani hii hivi IGP Mwema anajua kuwa kibao kikigeuka atabururwa na kutupwa kwenye mitaro kosa lipi wanafunzi wamefanya zaidi yao kuonyesha kutokuridhika na mwenendo wa serikali ya serikali kufanya mambo yakutokuzingatia usawa wanajenga taswira gani kwa msichana kama huyo ukimfanyia mtu ukatili yeye anaweza akawa sugu na asijali kitu
 
yawezekana Polisi wengi si raia wa nchi hii Utawala kama huu hauna tofauti na wa Gadaffi umechukua raia wa nch jirani kutesa wananchi na kutukandamiza.. tukichoka zaidi tunajua familia zenu muendelee kuishi huko huko kambini asanteni itv wekeni picha zao waje kujibu nchi ikiwa huru ...

Iko wapi tume ya haki za binadamu Tanzania? NATO Tunaomba Msaada wenu
 
Hawa hakuna cha kuwaangalia usoni ni kuwachemshia maji ya moto tu wakisikia wamemwagiwa wawili huko mitaani watashika adabu. Upole umetuzidi mno ndio maana hata huyo sijui makando kando anatupelekesha.
 
Mukandala nini professor pekee hopeless aliyeawahi kuwa VC wa UDSM; anashindwa hata na Kuhanga ambaye hakuwa profesa. Wakati wa utawala wote wa Kuhanga, hakuna hata siku moja ambapo mwanafunzi alipigwa na polisi ingawa kulikuwa na migomo ya nguvu sana dhidi ya utawala wake miaka ya themanini na saba au themanini na nane hivi hadi kuhitimisha utawala wake. Chuo kilipoanza kuongoza na Professor Mmari kukawa na matumaini tena makubwa sana yaliyowapa hofu watawala wa anchi hadi kuamua kumwondoa. Baada ya hapo chuo kilianza kupoteza ladha kidogo kidogo na hadi hivi sasa kinanuka kabisa.
 
Polisi washatutangazia kuwa ni maadui wetu maandamano ya jana Lema alipotoka hatukuona fujo zaidi ya wao ndio waletao fujo ati wanafuata sheria ...

kama ni sheria zibadilishwe nadhani zilitungwa na wafanya fujo...

Muondoke uraiani nyie si wenzetu tena Niamini dini hutuna kwenye selikari yetu. Wacha ni sign out nikakimbizane na Dollars
 
Hawa polisi wenyewe si rizki, wamelegea ndo maana hawana ubavu wa kupambana na majambazi front.....!

Inabidi nikubaliane na wewe. Badala ya hawa polisi kupambana na majambazi, yanajikita kuvunja fuvu na kuwadhalilisha watoto wetu vyuoni - haohao ambao kesho watakuwa madaktari na kuwatibu hayo ma FFU na familia zao.

Waone aibu hawa wa..enzi wakubwa!

Kama yana nguvu sana yaende yakapambane na majambazi, siyo watoto.
 
Ukileta fujo unapewa dozi yako, msikae kulaumu polisi wakati wote, wao wanafanya kazi yao.
 
Polisi wa tanzania wamefunzwa kuvunja vichwa ili madaktari wapate kazi za kufanya. Bila shaka motive ni tuyatishe yaogope, kitu ambacho hakiwezi kuzaa matunda.
Upande mwingine yaweza kuwa askari polisi wetu ni watumiaji wazuri wa bange, ndio inayowabangua.
Au hawajui kazi wanayopaswa kuwa wakiifanya.
 
Polisi wa tanzania wamefunzwa kuvunja vichwa ili madaktari wapate kazi za kufanya. Bila shaka motive ni tuyatishe yaogope, kitu ambacho hakiwezi kuzaa matunda.
Upande mwingine yaweza kuwa askari polisi wetu ni watumiaji wazuri wa bange, ndio inayowabangua.
Au hawajui kazi wanayopaswa kuwa wakiifanya.
Hapo kwenye red ndio mwisho wao wakiugua hata upele then wakijipeleka kwa Hospital ndio safari yao Utasikia Kavimba Ngozi mara oh Ana kipanda uso .. n.k wacha waendelee kusumbua hawajui Mla huliwa
 
Back
Top Bottom