Ferry ya Kigamboni ni sawa na 'Mobile Bridge', sio Meli - Je, wanaovuka Selander nao walipie?

kichwat

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
1,819
587
Ndugu wana JF. Kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu upandishaji wa gharama za ferry Kigamboni. Wakati watu wengi wakijadili kuhusu nauli ya sh. 100 kwenda sh. 200, kiukweli gharama zilizopandishwa hasa ni za vitu vingine kama magari, maguta, etc.Pia, hoja halisi hapa ni ukweli kwamba kivuko cha Kigamboni ni sawa na 'mobile bridge' kuvusha watu mita mia 2 au 3 tu. Pantoni pale hazitumiki kama MELI kama ilivyo kwenye vivuko vya kule ziwa Victoria. Na kama ni halali kulipia guta sh. 1,800 kuvuka Kigamboni, basi ni bora tukaanzisha utaratibu huo pia kwa wenzetu wanaovuka madaraja mengine kuingia mjini (Selandar, Jangwani, Ubungo, etc.) na hata pale kwa Mkapa kuelekea Mtwara.Nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom