Fence ipi inafaa. Ya ukuta, yawavu au ya miti yenye miba?

Fence ya michongoma ndio ya kisasa.
Michongoma inawekwa pamoja na wavu.
Hii ni Spanish style na pia ni nzuri kwa ulinzi, afya na mandhari.
View attachment 60978

Hii safi kabisa inakidhi. Kuna msemo unasema Bwana asipoilinda nyumba wailindao wakesha bure. Maanake hata ungejenga ukuta wa zege na umeme siku ya siku wataingia tu! Wewe hakikisha siri za ndani haziwafikii vibaka na majambazi kwani wezi hawaji kwa kubahatisha.
Uzio wa miti safi.
 
michongoma inagharama sana hasa ya matunzo........ni bora ukuta utainccure cost ila ni wakati wa ujenzi pekee then unatulia ila michongoma gharama ya kuikatia na kuishape itakuandama milele
 
Una mali kiasi gani? Linganisha mali ulizonazo nyumbani zinazoibika na gharama ya fence utakayojenga, ni dhahiri madirisha yana grill piga gharama zake. Fedha zako weka benki. Siku hizi dili ni kuiba kwa kwa akili, kwa simu tu jamaa unawapa watakacho kwa hiari yako. Cha ajabu unakuta mtu amejenga nyumba, madirisha yote yana grill, anajenga na ukuta ya nini yote hayo?? Badala yake ni wewe mwenyewe unajiweka gerezani ukizuka moto fire brigade hawawezi kuingia kukuokoa, majambazi yakikuingilia utashindwa kupata msaada....

Nakushauri kwa kutunza mazingira na mandhari safi ni bora fence ya michomgoma na hata miti ya aina nyingine inapendeza. Twende na wakati.
 
Panda michongoma mkuu watu wa hewa ukaa watakulipa mapesa. Ukuta ni kwa waarabu

Mzee wa Payment for Ecosystem tumekupata naona umeangalia hii issue kibiashara zaidi kwani ina serve kama fence alafu mwisho wa siku unaingiza hela
 
michongoma inagharama sana hasa ya matunzo........ni bora ukuta utainccure cost ila ni wakati wa ujenzi pekee then unatulia ila michongoma gharama ya kuikatia na kuishape itakuandama milele

Mkuu, mheshimiwa Ginner amekupa ushauri mzuri. Weka ukuta na ndani ya ukuta weka bustani yako nzuri kuboresha mazingira na afya. Michongoma utaikata maisha yako yote; na chunga utakapokua mzee na kipato kimeliwa SSRA, michongoma itageuka kichaka cha wezi!
 
Back
Top Bottom