Elections 2010 FemAct yataka meya Arusha ajiuzulu

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,172
FemAct yataka meya Arusha ajiuzulu


Na Gladness Mboma

SERIKALI imetakiwa kuufuta uchaguzi wa Meya Arusha na kuitisha uchaguzi mwingine huru ili wananchi wachague meya mwingine wanayemtaka, ikiwa ni pamoja na kumtaka aliyepo madarakani kwa sasa ajiuzulu ili kupisha
uchaguzi urudiwe kama alivyofanya Naibu wake Michael Kivuyo.

Pia wameitaka serikali iunde tume huru itakayowashirikisha wananchi, polisi, vyama vya siasa, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kushughulikia suala hili na kuwahakikishia wananchi wa Arusha kuwa tukio kama hili halitatokea tena.

Wito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Mashirika yapatayo 50 yanayotetea Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo na Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct).

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya ambaye alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya FeMAct alisema kuwa wanalaani ukiukwaji wa haki za binadamu, demokrasia na uvunjivu wa amani uliosababisha kuumizwa na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia mjini Arusha.

Alisema kuwa mashirika hayo yameshtushwa na vurugu na matumizi ya nguvu za dola dhidi ya raia waliokuwa katika harakati za kudai haki zao kupitia maandamano ya amani na mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama halali cha siasa jijini Arusha.

" Vurugu hizo ziliendana na unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa baadhi ya waandamanaji, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za kibinadamu na za wanawake,"alisema.

Alisema kuwa FemAct inalaani kitendo cha Halmashauri ya Jiji la Arusha kusimamia na kuendesha uchaguzi batili usiozingatia sheria kanuni na taratibu za uchaguzi ambao ulimpata Meya na Naibu wake Desemba 18 mwaka jana na kusababisha kutokea kwa vurugu hizo.

Bi. Mallya alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari na jeshi la Polisi watu wanne wamepoteza maisha na zaidi ya watu 30 kujeruhiwa vibaya wengi wao wakiwa ni watoto wadogo, wazee, walemavu na wajawazito.

Alisema kuwa FemAct inasikitika pia kuona siku nane baada ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgambo wa jiji waliwashambulia mamia ya wananchi hao waliokuwa wakiandamana, ambapo serikali imeendelea kukaa kimya bila kuunda tume au kuwachukulia hatua zozote wale wote waliosababisha vurugu hizo.

Pia FeMAct imedai kushtushwa na ukimya huo na maelezo yasiyojitosheleza na uzito wa kuchukua hatua za haraka ili kutenda haki kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutaka kutafuta suluhu na kurejesha demokrasia na haki miongoni mwa wananchi wa Arusha.

"FemAct tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi mabaya ya vyombo vya dola, hasa Jeshi la Polisi ambacho ni chombo cha ulinzi na usalama wa wananchi kugeuka na kuvunja sheria ya kuwazuia wananchi kutoa sauti zao na kupigania haki zao za msingi,"alisema.

Alisema kuwa wao kama sehemu ya jamii wanapinga mwenendo unaoweza kujengeka na kuonekana kama jambo la kawaida hapa nchini la kunyamazisha wananchi wasitoe sauti zao.

Bi. Mallya alisema kuwa tabia ya serikali kuzidi kuonesha ubabe katika matukio mbalimbali ya kudai haki nchini na kutolea mfano wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na UDSM.Alisema kuwa wakiwa kama wanaharakati wamelitaka jeshi la Polisi na serikali kuweka wazi muktadha na hali halisi ya tukio la Arusha, kuwataja na kuwachukulia hatua za kisheria walioshiriki kuvunja sheria na kutoa idadi kamili ya wananchi waliojeruhiwa na kupoteza maisha katika tukio hilo.

Bi. Mallya alisema kuwa kitendo cha kuendesha uchaguzi kwa ubabe ni kuikaba koo demokrasia, kukiuka haki za kibinadamu na kuwalazimisha wananchi viongozi wasiotaka.

Hali hiyo, ambapo wamekemea kwa nguvu zote na kwamba kamwe wananchi wa Tanzania hawatakubali tena kubebeshwa mzigo wa viongozi wasio na sifa za kuongoza.Bi. Mallya ameitaka pia serikali,vyama vya siasa na vyombo vya dola kutokuwanyamazisha wananchi, viongozi wa kijamii na dini wanaolizungumzia suala la Arusha kwani hivyo ni kinyume na demokrasia iliyoendelea na kukomaa nchini Tanzania.




1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Tatizo kubwa la Tanzania sasa hivi ni kwamba wasomi, wanaharakati, na baadhi ya viongozi wa dini ni watu ambao wanatoa matamko yanayoegemea upande wa upinzani. Nampongeza Professa Mwesiga Baregu kwa kuamua kuwa mwanachama wa chadema na kuamua kupoteza haki zake. Ningewaomba na wengine wafanye hivyo kwa maslahi ya umma kwa sababu wanatuchanganya sis wananchi wa kawaida. Kilichotokea Arusha kinaeleweka kuwa tatizo ni madiwani kususia uchaguzi shauri ya Chatanda kupiga kura. Chadema walifanya vurugu wakijua wanachodai si sahini. Hawa wanaharakati hawagusii maneno ya Slaa akiwaambia wafuasi wake kwenda polisi kuwatoa viongozi. Nyie wanaharakati, wasomi, na baadhi ya viongozi wa dini chukueni kadi za chadema ili mtakayosema tuwajuwe kuwa nyinyi ni wana chadema, la sivyo mnatuvuruga na taasisi zenu zinakosa credibility mbele ya wananchi. Mnazalilisha kazi zenu kwa kushabikia upande mmoja. Kwa hili la Arusha, Chadema wana kesi ya kujibu. Msipoteze malengo.
January 12, 2011 8:28 PM
 
Hivi Umeya wa Arusha ni kwa nini CCM inaung'ang'ania?
Kwa kuwa Arusha ni moja ya majiji hapa Tanzania,wanachohitaji ni kuwa na ushawishi katika jimbo hilo ili ifikapo 2015 waweze kuyachukua majimbo ya Arusha mjini,Arumeru mashariki na magharibi,na Monduli.Bila ya kufanya hivyo wanaweza kupoteza majimbo yote hayo!!
 
Kilichotokea Arusha kinaeleweka kuwa tatizo ni madiwani kususia uchaguzi shauri ya Chatanda kupiga kura. Chadema walifanya vurugu wakijua wanachodai si sahini. Hawa wanaharakati hawagusii maneno ya Slaa akiwaambia wafuasi wake kwenda polisi kuwatoa viongozi. Nyie wanaharakati, wasomi, na baadhi ya viongozi wa dini chukueni kadi za chadema ili mtakayosema tuwajuwe kuwa nyinyi ni wana chadema, la sivyo mnatuvuruga na taasisi zenu zinakosa credibility mbele ya wananchi. Mnazalilisha kazi zenu kwa kushabikia upande mmoja. Kwa hili la Arusha, Chadema wana kesi ya kujibu. Msipoteze malengo.
January 12, 2011 8:28 PM


Mkuu hapo ndipo na mimi ninaposhangazwa, wamekuwa kama vipofu kwa kuendeshwa na utashi wao binafsi kwa kushindwa kuangalia pande mbili na kutoa mawazo yao na si maamuzi
 
Tatizo ni kuwa katika kutenda haki lazima uchukue side. Kama watu wawili wanabishania jambo na mmoja yuko sawa na hakimu au mwamuzi akampa haki anayestahili haki je hapo atakuwa ameangukia upande mmoja au tuseme amechukua side!! Hebu jamani tujulisheni hivi kama CCM haikutetewa basi ni lazima haki haikutendeka. TUTUMIE COMMON SENSE!
 
Jeuri Mama Chitanda, ndio hao ASASI ZA KIRAIA (Mhimili wa nne katika serikali ya nchi yoyote duniani) kama haukupata kuwafahamu vema kwamba ni akina nani hao basi jaribu kuwadekekea kama ulivyodiriki kufanya kwa Mashehe na Maaskofu ndio utajua utamu wake.

Isitoshe kwa mujibu wa TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA za hapa hapa JF kwa Mzee Invisible ni kwamba mpaka hivi sasa MACHALII WA ARUSHA wamekwenda mpaka kule kijijini kwenu ulikozaliwa na wengine kule ulikowahi kupata jiko la kwanza kabla ya wao kurejea jijini Arusha kuleta salamu walichojifunza huko.
 
Tatizo ni kuwa katika kutenda haki lazima uchukue side.

Kama watu wawili wanabishania jambo na mmoja yuko sawa na hakimu au mwamuzi akampa haki anayestahili haki je hapo atakuwa ameangukia upande mmoja au tuseme amechukua side!! Hebu jamani tujulisheni hivi kama CCM haikutetewa basi ni lazima haki haikutendeka.

TUTUMIE COMMON SENSE!

Remember, occasionally sense are never common nor evenly distributed in away. Moreover I know of a lot others that always only rely on the help of the sixth sense / intuitive sense which is a kind of sense that only accessible in 2 out of every 1,000 persons.

Acha kuleta porojo hapa kama ndio umerejea leo katika sayari Tanzania uliza basi data za Arusha ujibiwe kuliko kujitia kujadili usiku wa giza!!
 
Tatizo ni kuwa katika kutenda haki lazima uchukue side. Kama watu wawili wanabishania jambo na mmoja yuko sawa na hakimu au mwamuzi akampa haki anayestahili haki je hapo atakuwa ameangukia upande mmoja au tuseme amechukua side!! Hebu jamani tujulisheni hivi kama CCM haikutetewa basi ni lazima haki haikutendeka. TUTUMIE COMMON SENSE!

Do you call urself a great thinker?, cmon man be in ur age, unawezaje kulinganisha hukumu ya mahakama na utashi wa maaskofu?,
Unajua kweli taratibu za manakama hadi kufikia kutoa maamuzi? unadhani zipo sawa na walizofanya maaskofu.
 
Ivi kwani wakirudia uchaguzi na wakazingatia kanuni zote si bado atashinda kama yeye ni halali? Nashangaa kwanini usirudiwe tu tumalize chokochoko tupate mshindi halali whoever that person is.


Mkuu hapo ndipo na mimi ninaposhangazwa, wamekuwa kama vipofu kwa kuendeshwa na utashi wao binafsi kwa kushindwa kuangalia pande mbili na kutoa mawazo yao na si maamuzi
 
Remember, occasionally sense are never common nor evenly distributed in away. Moreover I know of a lot others that always only rely on the help of the sixth sense / intuitive sense which is a kind of sense that only accessible in 2 out of every 1,000 persons.QUOTE]

Tunaposema common sense, tunajua fika it is not something common in easy meaning. Kama huweze kutumia common sense you are as good as dead. Inasikitisha kujua kuwa unajaribu kupotosha maana ya common sense. Hapa we do not refer kwa njia ya kupata ufahamu. Hapa ni issue ya what comes out of analytical mind. Si ngozi, pua, macho, masikio au ulimi au hiyo uliyoisikia sixth sense. Please use your common sense
 
Kama kweli sisi emu walishinda huo uchaguzi wa Meya kwa uhalali wa wingi wa kura, wanaogopa nini kurudia?? kwa nini wanang'ang'ania kwenda mahakamani??

Kumbe hata Mkuchika naye wale wale, kasema uchaguzi haurudiwi, hivi viongozi wa serikali ya ccm wana nia ya dhati kweli ya kuumaliza huu mgogoro?? Au wanaona raha watu kufa na kuumizwa na polisi kila wakati
 
Hivi Umeya wa Arusha ni kwa nini CCM inaung'ang'ania?

Mafisadi wakuu na viongozi wajuu serikali wanavitegauchumi visivyo halali hapo Arusha, na wanajua kama meya atatoka chama pinzani, basi siri nyingi zitafichuka na maslahi/miradi yao itakuwa hatarini.

Chunguza:
1: Kiwanda cha matairi General Tyre
2:Mzozo wa nyumba za AICC soweto
3: Viwanja vilivyo gawanywa Burka Estate.


Ukipata majibu yake, utajua ni kwa nini umeya wa arusha unang'ang'aniwa.
 
Back
Top Bottom