Fedha za serikali ziko wapi?

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Jan 31, 2009
7,333
3,896
WAUNGWANA FEDHA ZOTE HIZI HAPA CHINI
ZIMEENDA WAPI, HAZINA WANASEMA HAKUNA PESA, WAKANDARASI WANAIDAI SERIKALI, MISHAHARA TANGU 2011 UANZE TABU, JE PROF NDULLU HAKUSEMA KWELI?

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), ina akiba ya dola za Marekani bilioni 3.8, kiwango ambacho haijawahi kuwa nacho katika historia yake na kikubwa kuliko nchi zote tano za Afrika Mashariki.

Mbali na hizo, dola za Marekani bilioni 1.5 zipo katika akaunti za Watanzania nchini na dola bilioni moja ziko katika benki nchini.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema fedha hizo za Serikali zinaweza kutosha kwa zaidi ya miezi sita katika kununua bidhaa nje na kulipia huduma mbalimbali.

“Kwa sasa hakuna nchi ya Afrika Mashariki yenye akiba ya fedha kama zetu na miaka miwili iliyopita akiba yetu ilikuwa dola za Marekani bilioni 2.2 hadi 2.3 tu, lakini sasa imeongezeka na tumeweka historia”, alisema Profesa Ndulu katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisema kwa mwaka jana, fedha zilizoingia nchini kutokana na mauzo ya nje ziliongezeka zaidi ambapo dhahabu iliingiza dola za Marekani bilioni 1.4 na kufuatiwa na utalii ulioingiza dola bilioni 1.3.

Miaka ya nyuma utalii ulikuwa ukiongoza kwa kuingiza fedha za kigeni.

Alitaja mauzo ya bidhaa za viwandani yaliingiza dola za Marekani milioni 900; bidhaa za kilimo zimeingiza dola za Marekani milioni 450 hadi 480 na huduma zilizotokana na bidhaa zilizopitia bandari za nchini zimeingiza dola milioni 380.

Kuhusu ukuaji wa uchumi, Profesa Ndulu alisema “robo ya kwanza ya mwaka jana, uchumi ulikua kwa asilimia saba na robo iliyofuatia ulikua kwa asilimia 7.1 na robo ya tatu ukakua kwa asilimia 6.2 na robo ya mwisho tunategemea utafikia asilimia saba.”

SOURCE: HABARI LEO LA TAREHE,3.2.2011
 
Back
Top Bottom