Fedha za safari za JK zaibwa na watendaji

Kama ni kweli watakuwa wamefanya jambo la maana mkuu abaki nchini for a while maana amezidi

Hizi billoni tatu walikuwa wanazipiga kabla ya kufunga mwaka wa fedha ;wanajua sasa wakati wa bajeti zingine zitaingia kwahiyo walikuwa wanasafisha chungu!!
 
Mwalimu wangu kule Tosa boy aliwahi sema baada ya tuhuma kuwa anaiba chakula Kama baba ni mwizi, mama ni mwizi na watoto ni wezi, familia inakuwa ni ya wezi tu. Kwa maana hiyo Rais kama Rais ni mwizi basi si ajabu watoto nao wakawa wezi, maana Rais kama alivyo baba, asingekuwa mwizi, basi hata watumishi wa ngazi za chini(watoto) nao wasingekuwa wezi. Maoni yangu, kama wamesimamishwa ni bora tu wakaachiwa waendelee na kazi maana linchi linanukia harufu ya wizi tu.
The unseen is illustrated by the seen.
 
IKulu leo ama kesho itakuja na waraka kukanusha haya madai

Ha ha ha ha . Sa alva atakuwa anauandika muda huu. Halafu mi nafikiri hawa walishachukia kuwa mbona wao waishie vimishahara vya laki sita wakati mafisadi papa wapo wanapeta? Unajua nimegundua watu wengine wanaamua kuiba kwa hasira tuu. Hebu sasa kama yule Registrar wa serikali ana bilion 150 sasa tuseme nini? Ni mshahara na marupururpu gani amekusanya yafikie hapo? Haki ya nani hasira mbaya. Hii dubious income disparity ndiyo inaponza wengi.
 
Mwalimu wangu kule Tosa boy aliwahi sema baada ya tuhuma kuwa anaiba chakula Kama baba ni mwizi, mama ni mwizi na watoto ni wezi, familia inakuwa ni ya wezi tu. Kwa maana hiyo Rais kama Rais ni mwizi basi si ajabu watoto nao wakawa wezi, maana Rais kama alivyo baba, asingekuwa mwizi, basi hata watumishi wa ngazi za chini(watoto) nao wasingekuwa wezi. Maoni yangu, kama wamesimamishwa ni bora tu wakaachiwa waendelee na kazi maana linchi linanukia harufu ya wizi tu.
The unseen is illustrated by the seen.

Nimeipenda hii. Nyoka anazaa nyoka hawezi kuzaa kenge!!!! Ukipanda mahindi utavuna mahindi na si uwele!!! Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mlee mtoto njia ipasayo na hataisahau hadi uzeeni mwake!!!!
 
Hazijaibwa Ikulu zimeibwa mambo ya nje na Maafisa ambao sio wa Ikulu bali ni wa wizara hiyo.... mwanahalisi wametumia Ikulu kuuza gazeti lao. Fedha zilikuwa mikononi mwa wizara hiyo na ndio walikuwa walinzi wa fedha hizo sio Ikulu. Let be fair

MAMA POROJO, unataka tuwe 'fair' kwa nani na kwa lipi? How can we be fair to the thieves?
 
Ndio mwisho wa mwaka wa bajet walikua wanakombeleza chungu bahati mbaya kwao hawakuwashirikisha wenzao ndio maana imegundulika.
 
kazi kweli wameamua kujilipa kabla ya kusafiri au wamechoka kusafiri wameamua kuiba pesa ili wasiondoke kabisa nchini,by the way zingine si ndio zitatangazwa soon ktk bujei mpya na safari zitakuwa kama zamani
 
Sio mchezo mkuu hata wao wanaona jinsi 'VASCO DA GAMMA' anavyozichota hadi wanapata hasira.

Haswaaaaa, na ukiona hivyo wameiba kwa jeuri kwani wanajua siri nyingi za wakubwa wao wanavyokula, mtaona hawatafanywa kitu.
Huu ni upepo tu.
 
Bora zilivyoibwa Kwasababu Nkwere Amezidi kuzurura na safari zake zisizo na faida na Tanganyika yetu.
 
Ukiiba sasa wezi wengine wakajua unaiba sana, nao wanajua mchongo, watakuibia na wewe tu.


Utasikia kila siku wakilalamika Halmashauri wezi/mchwa wa fedha za serikali, wanajaribu kuficha madhambi ya setikali kuu.

Jaribu kujiuliza 3 bilioni ingekuwa H/mashauri Mwanry angetos povu mdomoni ni aje!!! Lrt us be rationally to ourselves and others, serikali kuu kwa maana wizara na Jumba kuu kuna ufusadi wa kufa mtu ila hausemwi tu kwa sababu wao ndo wasemaji wakuu na wanamajukwaa ya kuongelea.

Long live Tanzania, long live!!!
 
Inasikitisha sana
Ndio maaana huko ikulu kila mtu anapatakaeee, pesa zote hizo ni kwasafari tuu au na kwa mambo mengine?. Kwautashi wangu wa haraka bila kufanya utafiti akinifu, tunakoelekea kubaya na tena kubaya sana, halii hii inatisha kwa mtu anaye tafakari kwa kina na kibinaadamu. Hii kwa mfano naweza kusema watoto waingie kwenye chumba cha baba yao na kufungua kabati la kuifadhia pesa za baba yao na kuchukua fedha bila kupata ridhaa kutoka kwa mzazi, hiii ni mbaya machoni na kusikia. Kama wazazi wetu walio aminika nakupewa madaraka makubwa namna hii tena wenye kuhitaji uzalendo wa hali ya juu zaidi wanaweza kufanya hivyo sijui miaka ishirini ijayo kutakua na haligani Tanzania, nafikiri udhalimu wote utafanyika katika nchi hii, itakua zaidi ya pango la wanyang'anyi, fanya utakavyo hakuna wakukuuliza! INASIKITISHA KWELI KWELI!
 
Fedha za safari za JK zaibwa

MAOFISA watano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa "kwa ajili ya safari za rais," MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa za uhakika zilizopatikana ndani ya ikulu na wizara hiyo, zimesema kwamba maofisa hao, akiwemo Mkuu wa Itifaki, walifanikiwa kuchota Sh. 3 bilioni "kutoka benki moja nchini."


........................................................................

Source: Gazeti la Mwanahalisi:

itakua zilitumika kiintelijensia na hawajaambizana tu
 
Haswaaaaa, na ukiona hivyo wameiba kwa jeuri kwani wanajua siri nyingi za wakubwa wao wanavyokula, mtaona hawatafanywa kitu.
Huu ni upepo tu.


Ndiyo maana yake kwani wakithubutu kumwaga mboga na wao wanamwaga ugali WIN WIN situation hiyo.
 
Back
Top Bottom